Kutoka kulia ni Mhe. Balozi Dr. Batilda S. Burian akifanya mazungumzo ofisini kwake na Mkurugenzi Mkuu Mpya wa taasisi ya Shelter Afrique Bw. James Mugerwa(Katikati) ambaye aliambatana na afisa wake Bw. Vipya Harawa(Kushoto) ambaye ni Mkurugenzi wa masuala ya ushirikiano katika taasisi hiyo.
======= ======= ======= =======
Bw. James Mugerwa, Mkurugenzi Mkuu Mpya wa Taasisi ya Shelter Afrique yenye makao yake makuu hapa jijini Nairobi alimtembelea Mhe. Balozi Batilda ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha kutokana na kuchaguliwa kwake hivi karibuni kuwa Mkurugenzi Mpya wa Taasisi hii muhimu ambayo imekuwa ikijishughulisha na utoaji wa mikopo nafuu kwa nchi wanachama wake kwa ajili uendelezaji wa miji na makazi bora nafuu, ambapo Tanzania ni moja ya nchi mwanachama katika taasisi hii.
Mhe. Batilda ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UN-Habitat na UNEP yenye makao yake makuu hapa Nairobi.
Katika mazungumzo, Bw. Mugerwa alitoa shukrani za pekee kwa Tanzania kwa jinsi ambavyo imekuwa ikitoa ushirikiano mkubwa kwa Taasisi hii na kuahidi kudumisha na kuendeleza ushirikiano ambao umekuwepo.
Kwa upande wa Mhe. Balozi Batilda sambamba na kumpongeza Bw. Mugerwa kwa kuchaguliwa kwake kuongoza taasisi hii muhimu, alitoa shukrani za pekee kutokana na mikopo nafuu ambayo imekuwa ikitolewa na taasisi hii kwa Tanzania kwenye sekta ya uendelezaji wa makazi nafuu ikiwa ni pamoja na kumhakikishia kumpa ushirikiano wa Tanzania katika kutekeleza majukumu yake. Bw, Mugerwa ameahidi kuitembelea Tanzania siku za karibuni kwa ajili ya kuendeleza na kukuza ushirikiana ambao umekuwepo baina ya Tanzania na Taasisi hii.
Imetumwa na
Kiyavilo A. Msekwa
ICT Officer
Tanzania High Commission,
Nairobi, Kenya
0 comments:
Post a Comment