Mpendwa Baba                yetu, Joseph Mturi Mahemba
        Hatimaye siku, Miezi imepita hadi hii                leo ambapo imetimia Miaka miwili (2) tangu ulipotutoka                ghafla usiku ule wa siku ya jumatano ya tarehe moja ya                Mwezi Agosti, 2012 na kutuachia huzuni kubwa.
         Japokuwa haupo nasi hapa duniani                lakini tupo nawe kiroho kwa kuendeleza mema yote                uliyotufundisha na kutuasa. 
        Tunakukumbuka kwa Upole, Upendo,                Busara na Ukarimu uliokuwa nao kwa familia na Marafiki.                Mwongozo na matendo yako yataendelea kuwa dira kwetu.
        Daima unakumbukwa sana na Mkeo Rose                Joseph, dada  zako Theresia, Karaghita, Wankuru na Mnaga,                wanao wapendwa Michael, Mkami, Niwa, Sagana, Mary,                Geofrey, Nyakaho, Lecardia na Pricilla, na wajukuu zako                wote.
        Ibada Maalum ya Maombi itafanyika                tarehe 03/08/2014 Saa 2.00 asubuhi kwenye kanisa katoliki                la Mt Maurus Kurasini, Dar es Salaam.
               Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake                libalikiwe.
        
0 comments:
Post a Comment