Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema, Mhe. John Mnyika, ameeleza kuwa hawahusiki na mauaji hayo bali ni propaganda zinazoenezwa ili kuwasahaulisha wananchi juu ya suala la katiba linaloendelea. Mnyika alieleza kuwa wanaoeneza habari hizo ni wale ambao wanataka kuizuia Chadema na Ukawa kwa ujumla kuendelea na harakati za kupigania katiba ya wananchi ikiwemo kufanyika maandamano ya kitaifa iwapo Rais Kikwete hataingilia kati kulisimamisha zoezi la katiba mpya.
0 comments:
Post a Comment