Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/15.
Alisema bodi hiyo ilikwama kuwalipa baadhi ya wanafunzi walioanza mafunzo kwa vitendo Julai mwaka huu kutokana na uhaba wa fedha.
Aliongeza kuwa, hadi sasa vyuo vitano ndivyo ambavyo wanafunzi wake hawajapatiwa fedha hizo, lakini hadi mwishoni mwa wiki hii, fedha hizo zitakuwa zimeingizwa kwenye akaunti zao.
Alivitaja vyuo hivyo kuwa ni Chuo cha Tumaini Makumira Arusha (TUMA), Chuo cha Mtakatifu Stefano Moshi (SMMUCO), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Mtakatifu Agustine Mwanza na Chuo cha Theophil Kisanji (TEKU), ambapo jumla yao wapo wanafunzi 9,946.
Katika hatua nyingine, Mwaisobwa alisema hadi wanafunga maombi ya mikopo Julai 31 mwaka huu, wamepokea maombi ya mikopo 58,037 kati ya hiyo, wavulana 37,689 na wanawake 19,592," alisema.
0 comments:
Post a Comment