Luiz Felipe Scolari, kocha wa Brazil
"Ni wakati mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kazi yangu ya ukocha na siku mbaya zaidi katika maisha yangu ya soka. Lakini maisha yanaendelea. Nani anawajibika kwa matokeo haya? Ni mimi, ni mimi. Lawama za matokeo haya mabaya zinaweza kutuhusisha wote, lakini mtu aliyeamua timu ya kucheza na mbinu nilikuwa mimi.
Lilikuwa chaguo langu. Tulijitahidi kufanya kila tuwezalo, tulicheza kwa kiwango chetu cha mwisho-lakini tumeishia dhidi ya timu kubwa ya Ujerumani. Hatukukata tamaa na kurudi nyuma. Tuliparaganyika na kupaniki baada ya kufungwa bao la kwanza na kila kitu kiliharibikia hapo. Hata Ujerumani hawawezi kuelezea ilitokeaje-lakini ni kwasababu ya ujuzi wao na unatakiwa kuheshimu hilo.
Tunatakiwa kujiunza jinsi ya kukabiliana nalo. Ujumbe wangu kwa watu wa Brazil ni huu. Tafadhali watusamehe kwa kiwango hiki. Ninaomba radhi kwasababu hatujaweza kufika fainali-na tutajitahidi kushinda mechi ya nafasi ya tatu. Bado tuna sababu ya kucheza."
0 comments:
Post a Comment