Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto) akifungua rasmi mafunzo yanayowakutanisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yanayoendelea mjini Morogoro. Aliyekaa upande wa kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gidion Kasege.
Mmoja wa wawezeshaji Profesa Pius Yanda kutoka Kituo cha Taaluma ya Mabadiliko ya Tabianchi kilichopo chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha mada wakati wa mafunzo hayo
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa na wawezeshaji kwa nyakati tofauti tofauti
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira Mhandisi Gidion Kasege (kulia) na Afisa Mazingira Mkuu na Mratibu wa Mradi wa EMA-ISP Bw. Theodore Silinge kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa
Afisa Mazingira Mkuu na Mratibu wa Mradi wa EMA-ISP kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw. Theodore Silinge akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
Mtaalamu kutoka Idara ya Nishati iliyopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Nyaso Makwaya akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwasilisha mada kuhusiana na mikakati ya Wizara katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gidion Kasege (kulia) akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (aliyekaa kulia kwake) ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo yanayowakutanisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yanayoendelea mjini Morogoro.
Washiriki wa mafunzo ya Mabadiliko ya Tabianchi yanayoendelea mjini Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (wa nne kutoka kushoto waliosimama mstari wa mbele) mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo
0 comments:
Post a Comment