August 21, 2014

  • Waziri Mkuu kuwa mgeni rasmi mashindano ya Kimataifa ya Wushu


    Waziri Mkuu kuwa mgeni rasmi mashindano ya Kimataifa ya Wushu
    Na Daud Manongi, WHVUM

    Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mashindano ya Kimataifa ya mchezo wa Wushu (Kung fu) yatakayofanyika hapa nchi kuanzia tarehe 30 hadi 31 katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

    Hayo yamebainishwa na Rais wa Chama cha Mchezo wa Wushu nchini Mwalami Mitete alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

    Katika taarifa yake Mwalami alisema kuwa mashindano hayo yatajumuisha vilabu vyote vya mchezo huo hapa nchini ambapo alitaja idadi yake kuwa 23 na kuongeza kuwa kutakuwa na timu shiriki kutoka nchi mbalimbali zikiwemo China, Kenya, Uganda, Zimbabwe, Ethiopia, Libya na Iran.

    "Tunatarajia kufanya mashindano ya Kimataifa ambayo yatajulikana kama 2nd Wushu Competition na yatafanyika kuanzia tarehe 30 na 31 kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni katika viwanja vya Mnazi Mmoja". Alisema Mwalami.

    Kwa upande wake Mwakilishi wa Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Michael Kagondela amesema kuwa ni fursa nzuri kwa wadau wa michezo hapa nchini hasa wa mchezo wa Wushu kwa kuaandaa mashindano makubwa yanayoshirikisha timu kutoka sehemu mbalimbali kwani kufanya hiyvo kutaongeza hamasa kwa wanamichezo wa Tanzania kujifunza kutoka kwao Aidha Kagondela ameupongeza umoja wa wafanyabiashara wa China hapa nchini kwa hatua yao ya kudhamini mashindano hayo na kuomba wadau wengine wajitokeze katika kusaidia kukuza michezo hapa nchini.

    Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Liu Pong mshindano hayo kufadhiliwa na Jumuiya ya wafanyabiashara wa China hapa nchini ni matunda ya ushirikiano wa muda mrefu baina ya Tanzania na China na kuongeza kuwa michezo ni njia ambayo itaendeleza uhusiano huo.

    Hii ni mara ya pili kwa chama hicho kuandaa michuano mikubwa ya mchezo huo baada ya awali kuandaa michuano ya taifa iliyohusisha klabu pekee za Tanzania iliyofanyika Ufukwe wa Coco mwaka 2011.
    Tanzania International
    Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania wa pili kutoka kulia Bw.Liu Pong akiongea na wanahabari hawapo pichani kuhusu mashindano ya kimataifa ya mchezo wa WUSHU yatakoayofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja mwezi wa nane jijini Dar es Salaam mwaka huu.
    Mwakilishi wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Michael Kagondela watatu kutoka kulia akiongea na wanahabari hawapo pichani kuhusu mashindano ya kimataifa ya mchezo wa WUSHU yatakoayofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja mwezi wa nane jijini Dar es Salaam mwaka huu
    Rais wa Chama cha WUSHU nchini wapili kutoka kushoto akiongea na wanahabari hawapo pichani kuhusu mashindano ya kimataifa ya mchezo wa WUSHU yatakoayofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja mwezi wa nane jijini Dar es Salaam mwaka huu


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.