August 14, 2014

  • MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AFUNGUA MKUTANO WA SITA WA VYUO VIKUU MJINI ARUSHA



    MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AFUNGUA MKUTANO WA SITA WA VYUO VIKUU MJINI ARUSHA LEO
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Mkutano wa Sita wa Vyuo Vikuu uliofanyika leo Agost 12-2014 katika Hoteli ya Naura Spring mjini Arusha. Mkutano huo umewakutanisha washiriki mbalimbali wakiwemo, wanazuoni, wanasayansi, watunga sera na wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Senegal, Canada, Ujerumani, maofisa wa Benki ya Dunia na wadau mbalimbali wa maendeleo. Lengo la Mkutano huo ni kujadili nafasi ya Elimu ya Juu katika utekelezaji wa Malengo ya Milenia (MDGs)
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Sita wa Vyuo Vikuu uliofanyika leo Agost 12-2014 katika Hoteli ya Naura Spring mjini Arusha.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia vitabu vya aina mbali mbali alipotembelea mabanda ya maonesho yaliyoandaliwa na Vyuo Vikuu baada ya kufungua Mkutano wa Sita wa Vyuo Vikuu wenye lengo la kujadili nafasi ya Elimu ya Juu katika utekelezaji wa Malengo ya Milenia (MDGs) Mkutano huo umefunguliwa leo Agost 12-2014 katika Hoteli ya Naura Spring mjini Arusha.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijadiliana jambo na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Sita wa Vyuo Vikuu wenye lengo la kujadili nafasi ya Elimu ya Juu katika utekelezaji wa Malengo ya Milenia (MDGs) Mkutano huo umefunguliwa leo Agost 12-2014 katika Hoteli ya Naura Spring mjini Arusha. (Picha na OMR)


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.