Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima (kulia) akimsikiliza Ofisa wa Jeshi la Polisi Inspekta Rukia Kibwana wa Kitengo cha Maadili na Malalamiko Makao Makuu alipokuwa anatoa maelezo kuhusiana na kitengo hicho kinavyofanya kazi zake, wakati wa Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. aibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima (kushoto) akiisikiliza Bendi ya Jeshi la Polisi (Steel Band) wakati ilipokuwa inatoa burudani katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO), Injinia Omary Bakari (kulia) akimfafanulia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima, jinsi SIDO inavyofanya kazi zake wakati wa Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.aibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima (kulia) akimuuliza swali Ofisa wa Jeshi la Magereza kuhusiana na gharama na jinsi samani za ndani zilivyoweza kutengenezwa. Naibu Waziri Silima alitembelea Mabanda mbalimbali katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Ofisa wa Idara ya Uhamiaji, Tatu Burhani (kulia) akimpa maelezo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima jinsi idara hiyo inavyowahudumia wananchi mbalimbali wanaotembelea banda la idara hiyo katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima (wapili kushoto-waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wizara yake wanaohudumia wateja mbalimbali wanaotembelea Wizara hiyo na Taasisi zake katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
0 comments:
Post a Comment