Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba (kulia), akizungumza na wajumbe wapya wa kamati ya kitaifa ya matumizi salama ya bioteknojia ya kisasa wakati akiizindua rasmi Dar es Salaam leo katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI). Kushoto ni Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Utafiti na Maendeleo, Hussein Mansour.
Msimamizi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph Ndunguru (kushoto), akitoa mada kuhusu zao la muhogo na changamoto za magonjwa yanayolishambulia.
Baadhi ya wanakamati hao wakiwa ukumbini katika hafla
hiyo ya uzinduzi.
Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa bize wakati wa uzinduzi huo.
Wajumbe wa kamti hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mazingira, Dk. Julius Ningu (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo wa uzinduzi
Mkutano ukiendelea.
Waziri Makmba (kulia), akiwaongoza viongozi wengine kutembelea maabara ya kisasa ya utafiti ya MARI. Kutoka kushoto ni Msimamizi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph Ndunguru, Kaimu Mkurugenzi Utafiti na Maendeleo, Hussein Mansour na Profesa Raphael Chibunda.
Picha ya pamoja na Waziri Makamba.
Msimamizi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph Ndunguru (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri Makama na wajumbe wa kamati mpya jinsi maabara ya kisasa ya utafiti ya MARI inavyofanya kazi.
Mimea mbalimbali inayofanyiwa utafiti ikiwa katika chupa maalumu katika maabara hiyo.
Mbegu ya migomba iliyooteshwa baada ya kufanyiwa utafiti katika kituo hicho cha MARI.
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba ameitaka kamati ya kitaifa ya matumizi salama ya bioteknojia ya kisasa kutengeneza mpango kazi utakaosaidia kuharakisha shughuli zao na kuisaidia serikali.
Makamba alitoa mwito huo wakati akizindua kamati hiyo mpya katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI) jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
"Tengenezeni mpango kazi wenu ili serikali iufahamu na kuweza kuwasaidia kifedha endapo utakwama badala ya kukaa bila ya kuwa na dira na kusubiri kufanya mikutano yenu ya kupitisha jambo fulani mara tatu katika kipindi cha miaka nane" alisema Makamba.
Alisema kamati hiyo ni ya muhimu sana katika utoaji wa maamuzi kuhusu masuala ya matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa na kukuza uelewa kwa wajumbe wa kamati hiyo na wananchi kwa ujumla.
Alisema Tanzania ni nchi mwanachama wa mkataba wa bioanuai wenye malengo makuu matatu, Hifadhi ya bioanuai, matumizi endelevu ya bioanuai na mgawanyo sahihi wa faida zitokanazo na matumizi yake.
Alisema Tanzania iliridhia mkataba huo mwezi Machi, 1996 ili kushirikiana na Jumuia ya Kimataifa katika kutekeleza malengo yaliyotajwa.
Alisema alisema changamoto kubwa ya teknolojia hiyo ya bioteknolojia ya kisasa bado kuna wasiwasi kuhusu athari zinazoweza kutokea ambazo ni mzio, kujitokeza kwa magugu sugu, saratani, usugu wa dawa kwa matibabu ya magonjwa, wakulima kutegemea mbegu za kununua kila na madhara mengine ambayo kwa sasa hayajawa bayana.
Msimamizi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph Ndunguru alisema wamejipanga kujenga kituo kikubwa cha utafiti kitakacho gharimu dola za Marekani 556,000.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Hassan Mshinda alisema ili wakulima waweze kufanikiwa katika kilimo chao ni vizuri wakawa wanazingatia ushauri wa wataalamu ambao wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali ambazo huwapelekea wao kwa matumizi ya kilimo.
0 comments:
Post a Comment