Muimbaji maarufu wa mashairi nchini, Mrisho Mpoto Jumamosi Machi 5, 2016 atazindua video ya wimbo wake mpya Sizonje katika ukumbi wa Golden Jubilee jijini Dar es Salaam. Akizungumza na mwandishi wetu, Mpoto alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Mh. Waziri, wa Habari, Utamaduni, SanaanaMichezo Nape Nnauye.
Alisema kuwa kabla ya uzinduzi huo kutakuwa na mjadala kuhusu 'KufeliElimuSioKufeliMaisha' ila kinachotakiwa ni kutokata tamaa. Ikiwa na kauli mbiu ya INUKA ENDELEA. Alisema kuwa katika mjadala huo watu mbalimbali maarufu wakiwemo wasanii, wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Wahadhiri pamoja na wadau mbalimbali wa elimu watazungumza kuhusu suala la elimu. Mbali na watu hao pia wanatarajiwa kuwepo wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya Kiswahili katika kidato cha nne pamoja na baadhi ya wale, ambao hawakufanya vizuri ili kupata uzoefu wao na kujua ninikifanyike ili kusonga mbele.
Aliwataja baadhi ya wasanii na watu wengine maarufu watakao zungumza siku hiyo ni pamoja na Ruge Mutahaba, AY, Said Fella, Niki wa Pili, Babu Tale, George Kavishe, Miss Tanzania Lilian Kamazima, Mbunge wa MikumiP rofesa Jay, Gardner G. Habash, Shilole, Ommy Dimpoz na Mwana FA.
Alisema onesho hilo litafanyika katika ukumbi huo kuanzia saa 3:00 asubuhi. Alisema kuwa video ya wimbo Sizonje ni elimu tosha ya Kiswahili, hivyo ni muhimu mjadala wa Kiswahili ukafanyika siku hiyo yauzinduzi wake ili kuibua mjadala wa kitaifa.
Alisema kuwa wanafunzi walio fanya vibaya katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana ni wengi kuliko wale waliofaulu, hivyo ni muhimu kuwatia moyo ili kuhakikisha hawakati tamaa na badala yake wanasonga mbele na kuhakikisha wanafanya vizuri katika maisha.
0 comments:
Post a Comment