March 02, 2016

  • KIJANA AJICHINJA UTUMBO WAKE KWA WEMBE KISA KANYIMWA CHAKULA NA MKEWE



    KIJANA AJICHINJA UTUMBO WAKE KWA WEMBE KISA KANYIMWA CHAKULA NA MKEWE

    Kijana mwenye umri wa miaka 30, amefanya tukio la kushangaza kwa kujipasua tumbo kwa wembe na kuukatakata vipande utumbo wake.Tukio hilo lilitokea Februari 28, katika Wilaya ya Kakonko, Kigoma. Mkazi huyo wa Kijiji cha Kinonko, Furaha John alifikia uamuzi huo baada ya jaribio la kujinyonga kwa kutumia kamba kushindikana.John ambaye anaelezwa kuwa ni mfanyabiashara wa pombe za kienyeji, aliamua kujiua kutokana na hasira za kudhulumiwa Sh35,000 na pia kunyimwa chakula na mkewe. Akisimulia mkasa huo, John ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kibondo, alisema alirejea nyumbani akiwa na hasira za 'kurushwa' fedha zake na mfanyabiashara mwenzake.Alisema nyumbani nako alikutana na tukio la kunyimwa chakula na mkewe, jambo lililomuongezea hasira na kuona bora afe. "Yaani nilitoka kazini nimekasirika baada ya mwenzangu kunidhulumu fedha zote za mauzo ya siku hiyo, nafika nyumbani mke wangu naye akaninyima chakula. Nikaona ni bora kufa kwa sababu sina haja ya kuendelea kuishi," alisema.Mashuhuda wa tukio hilo walisema John alifikishwa hospitali pamoja na vipande viwili vya utumbo alivyovikata, lakini madaktari walivitupa baada ya kuharibika kwa kukaa nje ya tumbo kwa muda mrefu. Baba mzazi wa kijana huyo, Juma Nkonkoili alisema kitendo hicho kimeisikitisha familia kwa sababu si jambo la kawaida mtu kujitoa utumbo na kuanza kuukatakata mwenyewe kwa lengo la kujiua."Tulimkimbiza kituo cha Afya Kakonko baada ya kumfunga tumbo kwa nguo kuzuia usimwagike chini, huku vipande viwili vya utumbo wake tukivihifadhi kwenye mfuko wa rambo, ndipo madaktari walipotushauri kumuwahisha hospitali ya wilaya," alisema Nkonkoili.<Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Adam Jonathan alisema madaktari walifanikiwa kuokoa maisha ya mgonjwa huyo baada ya kumfanyia upasuaji kurekebisha utumbo wake.Alisema walitupa vipande viwili vyenye urefu wa futi nne ambavyo mgonjwa huyo alivikata tumboni mwake baada ya kuharibika.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.