March 02, 2016

  • TAMASHA LA PAMOJA TUNAFANIKISHA KUSHIRIKISHA WANAWAKE NA WANAUME MACHI 5 MWAKA HUU.



    TAMASHA LA PAMOJA TUNAFANIKISHA KUSHIRIKISHA WANAWAKE NA WANAUME MACHI 5 MWAKA HUU.
     Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Trumark Tanzania, Agnes Mgongo akizungumza na waandishi wa habari jijiniDar es Salaam leo kuhusiana na kufanyika kwa tamasha la pamoja tunafanikisha linanaloandaliwa na kampuni ya Trumark litakalo fanyika Machi 5, mwaka huu katika ukumbi wa Kingsolomon Namanga jijini Dar es Salaam. Agnes amesema kuwa  kutakuwa na burudani zitakazotolewa na Barnaba na Classic Band, Bi. Patricia Hillary na mchekeshaji maarufu MC Pilipili, wakisindikizwa na wasanii chipukizi.
    Aidha TruMark inawashukuru wahamasishaji na wadhamini wa maadhimisho haya, ambao ni Vayle Springs, Mummy's Exclusive Shop, Flexible Entertainment, Marie Stopes Tanzania, King Solomon Hall, King Solomon Events, Mono Accessories, CSI Tanzania, MagicFM na Channel Ten.  
    Mwanamziki wa zamani wa Taarabu, Patricia Hilary akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa katika tamasha la Pamoja tunafanikisha linaloandaliwa na Kampuni ya TruMark kuwa atatumbuiza kwa nyimbo zake za zamani za Taarabu kama wimbo wa ewe njiwa utaimbwa laivu na mwanamziki huyo. Kulia ni Mratibu wa Tamasha la pamoja tunafanikisha wa kampuni ya TruMark, Azavery Phares.
    KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

    KAMPUNI ya TruMark yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam imeandaa tamasha la kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani la Pamoja Tunafanikisha, litakalofanyika Dar es Salaam, kwenye ukumbi wa King Solomon, Namanga, Machi 5,2016 ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ndiye atakayekuwa mgeni rasmi tamasha hiyo litawashirikisha wanaume na wanawake ili kufurahia mafanikio ya wanawake.

    Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa TruMark, Agnes Mgongo, amesema kampuni yake imeandaa tamasha hilo kwa kuwa kumekuwa na matukio mengi ya mafanikio kwa wanawake nchini Tanzania, ambayo bado wanaume hawajashirikishwa ipasavyo kuyatambua na kuyafurahia mafanikio hayo kwa kiwango kinachoridhisha.

    "Ni kweli, wapo wanawake wengi wenye mafanikio hapa nchini, lakini bado kuna changamoto nyingi, mojawapo ikiwa uchache wa ushiriki wa wanaume katika, kwanza, kufanikisha mafanikio hayo na, pili, kufungua fursa nyingi zaidi ili wanawake wengi zaidi waweze kuwa sehemu ya mafanikio hayo, kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii, kama vile sekta za fedha, elimu, sayansi, teknolojia, kilimo, viwanda, taaluma na biashara," amesema.

    Kwa kutambua hilo, Agnesy amesema yeye na timu yake kabambe ya TruMark wameamua kuandaa adhimisho la kusheherekea Siku ya Wanawake Duniani ambapo mwaka huu, adhimisho hilo linaambatana na kaulimbiu ya kimataifa linalotutaka watu wote, wanaume na wanaume, kushirikiana kuharakisha harakati za kumwezesha msichana na mwanamke kufikia malengo na mafanikio yake, linalosema "PamojaTunafanikisha".

    Mwaka huu, maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, chini ya mwamvuli wa 'PamojaTunafanikisha' kampuni ya TruMark inaona fahari kubwa kuandaa sherehe hii ambayo ni jukwaa muhimu kwa taifa letu, katika kuhakikisha wanawake wanakuwa sehemu mojawapo ya kuchangia pato la taifa na maendeleo ya nchi.

    "Kila mtu mahali alipo kwa nafasi yake ni kiongozi wa kuleta chachu ya Maendeleo, hivyo basi, haina budi kila mtu, mahali popote, ashiriki vyema na kutimiza wajibu wake huo, huku tukisaidiana kwa pamoja kuanzia ngazi ya familia hadi taifa," amesema.

    Agnesy amewashukuru Marie Stopes Tanzania ambao, kwa ushiriki wao, wameamua kutoa huduma ya bure ya upimaji na ushauri wa njia zote za uzazi wa mpango, upimaji wa saratani ya mlango wa uzazi kwa washiriki wote watakaofika kuhudhuria adhimisho hilo la Pamoja Tunafanikisha.

     Amewaomba wanaume kushiriki kwenye tamasha hili la Pamoja Tunafanikisha ili kwa pamoja jamii nzima iweze kufanikisha, sio tu mafanikio ya wanawake, lakini pia kuwawezesha kupata fursa zote za mafanikio, ikiwa ni pamoja na kutafuta fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.

    Adhimisho hilo, ambalo litafanyika kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga, Dar es Salaam, Jumamosi, tarehe 5 Machi 2016, litakuwa na burudani zitakazotolewa na Barnaba na Classic Band, Bi. Patricia Hillary na mchekeshaji maarufu MC Pilipili, wakisindikizwa na wasanii chipukizi.

    TruMark inawashukuru wahamasishaji na wadhamini wa maadhimisho haya, ambao ni Vayle Springs, Mummy's Exclusive Shop, Flexible Entertainment, Marie Stopes Tanzania, King Solomon Hall, King Solomon Events, Mono Accessories, CSI Tanzania, MagicFM na Channel Ten.
    Imetolewa na TruMark Limited | +255-718-969 731 | +255-716-676 665 | info@trumark.co.tz.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.