Kijana huyo omba omba tishio akipelekwa kituo cha polisi pamoja na kisu anachotumia kutishia wananchi wakati akiomba pesa
Askari polisi wakiwa wamembana lilivyo kijana huyo omba omba
Hapa akiwa eneo la Miyomboni akipelekwa kituoni
OMBA omba hatari anayeomba kwa nguvu kwa kutumia kisu kwa wananchi wanaomnyima msaada wa pesa amekamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Iringa kufuatia msako mkali dhidi yake.
Tukio la kukamatwa kwa kijana huyo lilitokea leo majira ya saa 5 asubuhi katika eneo la Posta mjini Iringa baada ya kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa mji wa Iringa hasa wanawake ambao wamekuwa wakifukuzwa kwa kisu na kijana huyo omba omba baada ya kumnyima pesa.
Mmoja kati ya wanawake ambao wamepata kutishiwa kuchomwa kisu na kijana huyo aliyetajwa kwa jina la Mohamed Iddy Chengula (18) Bi Amina Said mkazi wa Mkwawa alisema kuwa ni zaidi ya mara mbili amenusurika kuchomwa kisu na kijana huyo omba omba .
Alisema kuwa mji wa Iringa una omba omba wengi ila mbinu hiyo anayotumia kijana Mohamed ya kutembea na kisu na kuomba kwa kutishia kisu ni mpya kutokea mjini hapa na ni omba omba pekee ambae kwa mwonekano haonyeshi kama ni omba omba anaonyesha ni kijana mtanashati mzuri ila vitendo vyake ndivyo vimekuwa tishio kubwa kwa wananchi.
Huku vijana wauza magazeti eneo la Posta walidai kuwa ni mara kadhaa wamekuwa weakishuhudia mbinu chafu za kijana huyo ambazo wao wanafananisha na unyang'anyi na sio omba omba wa kawaida .
Kwani walisema haiwezekani kama ni omba omba kweli kutembea na kisu na pindi anaponyimwa pesa anachomoa kisu na kutaka kumchoma yule aliyemnyima pesa na wakati mwingine huwafukuza hasa wanawake .
Vijana hao walisema tukuo la leo kwa omba omba huyo kutishia kumchoma mtu kisu mbele ya askari hao ndilo ambalo limefanikisha kukamatwa kwake .
Hata hivyo askari hao walionyesha ukomavu mkubwa wa kiaskari katika kumkamata ombaomba huyo ambae alikuwa akitishia kuwachoma kisu kabla ya kumdhibiti kisawa sawa na kumpeleka kituo cha polisi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Peter Kakamba pamoja na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo alitaka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi wanapoona matukio ya watu kama hao kwani ni hatari katika jami
0 comments:
Post a Comment