March 01, 2016

  • Benki ya NBC yazindua kitengo kipya cha kuhudumia wateja maalum (Private Banking) mkoani Mwanza



    Benki ya NBC yazindua kitengo kipya cha kuhudumia wateja maalum (Private Banking) mkoani Mwanza
    Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Mwanza, Elinser ​Nyange (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitengo maalumu cha kuhudumia wateja maalum (Private Banking) katika tawi la Benki ya NBC mkoani Mwanza hivi karibuni. Kushoto ni Meneja wa NBC wa tawi hilo, Godhard Hunja na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maluum wa NBC, Ashura Waziri. Hiki ni kitengo cha tatu kuanzishwa baada ya vingine viwili katika matawi ya Sea Cliff na Corporate ya jijini Dar es Salaam.
    Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri (kulia), akimpa maelezo Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mwanza, Elins​er Nyange (katikati) kuhusu huduma za kibenki za NBC wakati wa uzinduzi rasmi wa kitengo kipya cha kuhudumia wateja maalum (Private Banking) katika tawi la NBC jijini Mwanza. Hafla hiyo ilifanyika mjini Mwanza hivi karibuni. Anayeangalia ni Meneja wa tawi hilo, Godhard Hunja. Hiki ni kitengo cha tatu baada ya vingine viwili kuzinduliwa katika matawi ya Sea Cliff na Corporate ya jijini Dar es Salaam.
    Meneja wa Benki ya NBC tawi la Mwanza, Godhard Hunja (kushoto), akifafanunua jambo kwa Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mwanza, Elins​er​ Nyange (k​ulia) na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalum, Ashura Waziri akiangalia wakati wa uzinduzi rasmi wa kitengo kipya cha kuhudumia wateja maalum (Private Banking) katika tawi hilo. Uzinduz​i huo ulifanyika mjini Mwanza hivi karibuni.
    Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Mwanza, Elinser​Nyange (wa pili kulia) akifanya mahojiano wa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.