Shirika la umeme nchini TANESCO limesema kwa sasa limejiimarisha kimfumo na kiutendaji ili kuhakikisha wateja wake wote wanapata huduma bora za umeme na kwa wakati bila usumbufu wowote huku mfumo katika vituo vyote vya kuuzia umeme ukiimarishwa.
Wakati nchi kwa sasa ikiwa mguu sawa kuelekea kwenye kipato cha kati yenye uchumi wa viwanda, nishati ya umeme wa uhakika ndiyo inayoweza kutimiza ndoto hiyo ya nchi, lakini TANESCO wanasema wamejipanga vema kimfumo tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Miongoni mwa mipango mikuu ya kurahisha huduma ya utaoji wa nishati hiyo ya umeme,ni pendekezo la kufutwa kwa gharama za huduma kwa wateja, yaani SERVICE CHARGE,huku tatizo la baadhi ya vituo vya kuuzia umeme kushindwa kutoa huduma ipasavyo nalo likiwa tayari limekwisha kushughulikiwa.
Afisa huyo mwandamizi wa TANESCO makao makuu amewatoa hofu watanzania kuhusu nishati hiyo huku akisema ni lazima ya shirika hilo kuona ndoto ya tanzania yenye viwanda inatimia ikiwa na umeme wa uhakika.
Wananchi wanasema mipango ya uondoaji wa gharama za huduma kwa wateja ni neema kwao kwani itawaondolea gharama nyingi walizokuwa wakitumia kununua umeme.
0 comments:
Post a Comment