Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amevitaka vikosi vya taifa hilo vijiandae kutumia silaha za nyuklia "wakati wowote", vyombo vya habari vya serikali nchini humo vimesema.
Ameambia viongozi wa kijeshi kwamba North Korea itabadilisha hali yake ya kijeshi na kuwa tayari hata kutekeleza mashambulio ya kuzuia hatari, shirika la habari la KCNA limesema.
Lakini licha ya madai hayo, bado haijabainika taifa hilo limepiga hatua gani katika kuandaa silaha zake za nyuklia.
Umoja wa Mataifa umewekea taifa hilo vikwazo vikali zaidi baada ya Prongyang kufanya majaribio ya nyuklia na makombora ya masafa marefu.
Baada ya kuwekewa vikwazo, Korea Kaskazini ilijibu kwa kufyatua makombora sita ya masafa mafupi baharini.
KCNA imesema Kim alikuwa akizungumza wakati wa zoezi la kijeshi Alhamisi. Inaaminika huo ulikuwa wakati ambao makombora hayo yafyatuliwa.
Alisema Korea Kaskazini "lazima iwe tayari kufaytua silaha za nyuklia wakati wowote" kwa sababu maadui wanaitishia Korea Kaskazini.
"Katika wakati huu wa hatari ambapo Wamarekani … wanahimiza vita na maafa kwa nchi nyingine na watu wengine, njia pekee ya kulinda uhuru wetu na haki ya kuendelea kuwepo ni kuimarisha uwezo wetu wa nyuklia," amenukuliwa akisema
0 comments:
Post a Comment