Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

October 31, 2014

  • BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI LACHOCHEA UBORA WA UTENGENEZAJI SAMANI NCHIN



    BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI LACHOCHEA UBORA WA UTENGENEZAJI SAMANI NCHIN

    Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Dk Anacleti Kashuliza (wa pili kulia) akiweka saini makubaliano ya ushirikiano kati ya FCDL na TAWOFE katika kuboresha utengenezaji wa samani nchini. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu (wa kwanza kulia) anayeshuhudia makubaliano hayo.


    NA SAID MKABAKULI
    KAMPUNI ya Furniture Centre (FCDL), na Shirikisho la Watengenezaji Samani Nchini (TAWOFE), wamesaini makubaliano (MoU) kuongeza ubora wa bidhaa za samani zinazotengenezwa nchini na kuzifanya zipate soko ndani na nje ya nchi.
    Makubaliano haya yamekamilika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ikiwa ni mwendelezo wa Tathimini iliyofanywa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani, katika kuiwezesha sekta ya Samani nchini kupitia vikundi na makampuni ya ndani.
    Tathimini hiyo ya Baraza ya mwaka 2008, ilijikita katika kubaini mahitaji na changamoto zinazoikabili sekta ya samani hapa nchini. Baraza liliweza kuandaa warsha iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali na ambapo matokeo ya tathmini hiyo yaliwasilishwa. Wadau kutoka sekta ya umma na binafsi walishiriki katika mrejesho wa tathmini hiyo na wao pia kuchangia maoni zaidi kwa ajili ya kuiboresha.
    Washirika hao walisaini makubaliano hayo katika  hafla iliyoshuhudiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji wa Uchumi na Uwekezaji), Dk Mary Nagu.
    Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dk Anacleti Kashuliza, alisema pamoja na kuwepo kwa fursa kubwa ya soko la samani hapa nchini bado ushiriki wa vikundi na makampuni ya ndani katika soko hilo ni mdogo sana kulinganisha na samani zinazoagizwa kutoka  nje ya nchi.
    Alisema tunatoa wito kwa taasisi za Umma na Binafsi  ziunge mkono jitihada hizi kwa kununua samani toka kwa watengenezaji samani  wa ndani na ili kuwapa ushirikiano zaidi utakaowezesha kuimarisha sekta ya samani zitengenezwazo ndani ya nchi.
    Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAWOFE, Bw Fredrick Waibi, alielezea makubaliano kati ya FCDL na TAWOFE ni mkakati mzuri utaomjengea uwezo fundi seremala kuweza kutengeneza bidhaa zitakazoweza kukubalika kimataifa, kuongeza tija kazini na kupunguza umaskini kati ya mafundi seremala.
    Naye Mkurugenzi Mkuu wa FCDL, Bw Shafik Bhatia, alisema kama wadau muhimu wa samani nchini wameona umuhimu na wanajivunia  kushirikiana na Tawofe katika kuboresha huduma za samani nchini .


  • UN YAOKOA MAISHA YA WATOTO 3000 ZANZIBAR


    UN YAOKOA MAISHA YA WATOTO 3000 ZANZIBAR
    DSC_0152Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari wa Zanzibar kwenye ofisi ndogo za mashirika ya Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar kuhusiana na mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na kushoto ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu.


    Na Mwandishi wetu, Zanzibar
    Zaidi ya watoto 3000 waliokuwa wakikabiliwa na utapiamlo nchini Zanzibar sasa wapo katika hali nzuri baada ya Umoja wa Mataifa (UN)kwa kushirikiana na wadau wengine kufanikisha programu ya kusaidia kukabili utapiamlo mkali kwa watoto hao.
    kauli hiyo imetolewa katika mkutano wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari uliofanyika hivi karibuni ambapo UN ilielezea mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni.
    Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kwamba Umoja huo ukiadhimisha miaka 69 ya uwepo wake imefurahishwa na maendeleo yaliyopatikana katika maeneo ambayo ilikuwa imejikita kusaidia kukabili umaskini,kuhakikisha utawala bora na kusaidia jamii.
    Alisema pamoja na kuendeleza na juhudi za kukabiliana na utapiamlo katika visiwa vya Pemba pia Umoja huo umefurahishwa na hatua zilizofikia katika kukabiliana na vifo vya mama na mtoto na kusema ni wajibu kuhakikisha watoto hawana matatizo ya utapiamlo kwani wao ndio msingi wa taifa la sasa na lijalo.
    Alisema hata hivyo upo umuhimu wa kuendelea na washirika wengine wa maendeleo kuona kwamba tatizo la utapiamlo la visiwa vya Pemba kwa watoto linamalizwa.
    DSC_0177Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akielezea kufurahishwa kwake na Serikali Tanzania kwa kupigia hatua katika kutoa ajira nyingi kwa walimu kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
    Alisema pamoja na mafanikio hayo Umoja wa Mataifa unaendelea na ujenzi wa uwezo kwa baraza la wawakilishi ili kuhakikisha kwamba baraza hilo linawezesha kuwepo kwa sheria nzuri na bora na zinazotekelezeka ambazo hazikwazi kukua kwa demokrasia na ustawi wa jamii.
    Aidha alisema kwa kuzingatia kwamba mwaka huu mwishoni kuna uchaguzi wa serikali za mitaa na pia uchaguzi mkuu mwakani pamoja na kura ya maoni ya katiba, Umoja huo unaendelea kufanyakazi na Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kwa kuiwezesha kitaalamu kuweza kufikisha elimu ya uraia kwa wananchi.
    Aidha katika masuala ya utawala bora Umoja wa Mataifa unashirikiana na taasisi za sheria kwa ajili ya kufanya mabadiliko katika mfumo wa sheria za watoto ili kuwepo na usalama mkubwa kwa watoto hasa kutokana na utamaduni uliopo visiwani kwa sasa.
    Aidha alisema kwamba yamepatikana mafanikio makubwa katika sekta ya tiba na kuzuia maambukizi ya Ukimwi na kuondokana na unyanyapaa.
    DSC_0121Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Zanzibar, Talib Ussi akiuliza swali kwenye mkutano huo.
    Aliwahimiza waandishi wa habari kuwa daraja la kuelezea mafanikio na pia changamoto zinazotokana na program za Umoja wa mataifa zilizolenga kusaidia maendeleo ya wananchi wa Zanzibar.
    Alisema matokeo ya program ya kusaidia maendeleo ya Tanzania (UNDAP) ndiyo yatakayotumika kutengeneza UNDAP 2 ambayo inatarajiwa kuanza katikati ya mwaka 2016.
    Katika mkutano huo ambapo waandishi walipata nafasi kubwa ya kuuliza masuala yanayohusu shughuli za Umoja wa Mataifa Zanzibar, Bara na duniani kwa ujumla Alvaro alizungumzia pia umuhimu wa Umoja wa Mataifa katika dunia inayobadilika.
    Alisema pamoja na madhumuni ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, baada ya vita kuu ya dunia ya pili mwaka 1945 ya usalama na kujenga uchumi baada ya kuharibiwa na vita yapo palepale, mabadiliko katika utendaji kwa lengo hilo hilo la usalama na maendeleo ni dhahiri.
    Alisema mathalani malengo ya millennia (MDGs) ambayo yalisanifiwa kwa lengo la kuleta maendeleo duniani katika demokrasia, utawala bora na ustawi wa jamii, bado yanatakiwa kuimarishwa kupitia mpango mpya wa maendeleo SDGs wenye lengo la kutokomeza umaskini uliotopea duniani ifikapo mwaka 2030.
    DSC_0060Afisa Habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni.
    Alisema ni matumaini yake kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana na UN katika kuhakikisha kwamba mafanikio katika MDGs yanaendelezwa na pia kukamilisha yale ambayo hayakufikiwa kwa lengo la kutokomeza umaskini uliotopea ifikapo mwaka 2030.
    Alisema mafanikio ya UNDAP kwenye utawala bora, ustawi wa jamii na uondoaji umaskini na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania, ni matokeo ya ushirikiano kati yake ya mamlaka mbalimbali nchini Tanzania na kwamba UN itaendelea kushirikiana na mamlaka hizo kuhakikisha maendeleo ya kuwezesha amani na usalama na ukuaji wa uchumi yanapatikana.
    Naye Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema lengo la kukutana na waandishi wa habari wa Zanzibar lilikuwa kuangalia mafanikio na namna ambavyo program za Umoja wa Mataifa katika visiwa vya Zanzibar zinafanyakazi.
    Alisema kwamba shughuli za Umoja wa Mataifa visiwani humo zinaweza tu kujulikana kwa wananchi kwa kupitia waandishi wa habari ambao wanakuwa wanajua Umoja huo unafanya nini na wapi.
    DSC_0063Mkutano kati ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari wa Zanzibar ukiendelea.
    DSC_0131Mwandishi wa habari wa TBC, Kulthum Ally, akiuliza swali kuhusiana namna Umoja wa Mataifa unavyoweza kuwasaidia Wanawake wa Zanzibar kupata nafasi za uongozi sawa na wanaume.
    DSC_0192Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (waliokaa katikati), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) pamoja na Meneja wa Baraza la Habari Zanzibar, Suleiman Omar (kushoto) katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wa Zanzibar.


  • TABATA FC YAINGIA ROBO FAINALI YA LIGI YA DK. MWAKA SPORTS EXTRA NDONDO CUP BAADA YA KUIFUNGA SIFA POLITAN KWA PENALTI 4-3



    TABATA FC YAINGIA ROBO FAINALI YA LIGI YA DK. MWAKA SPORTS EXTRA NDONDO CUP BAADA YA KUIFUNGA SIFA POLITAN KWA PENALTI 4-3
     Wachezaji wa timu za Boom FC na Vijana ya Ilala wakisalimiana kabla ya mchezo wao wa hatua ya 16 Bora ya michuano ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup 2014 uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
     Kikosi cha timu ya Vijana ya Ilala kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na Boom FC katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
    Kikosi cha timu ya Boom FC kikiwa katika picha ya pamoja.
     Mashabiki wa timu ya Boom FC, wakipiga ngoma wakati timu yao ikicheza na Vijana ya Ilala.
    Nahodha wa timu ya Vijana Ilala (kushoto) akisalimiana na mwenzake wa Boom FC, kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup.
    Mshambuliaji wa timu ya Vijana Ilala, Matola Selemani, kushoto akiwania mpira na winga wa timu ya Boom FC, Nambongo Hussein katika mchezo wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup.
    Mshambuliaji wa timu ya Boom FC,Issac Tesha (katikati) akijaribu kufunga  bao katika Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup 
    Winga wa timu ya Boom FC, akiwatoka mabeki wa timu ya Vijana ya Ilala katika mchezo wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup. 
    Beki wa timu ya Vijana Ilala Ramadhani Yasini, (kushoto) akiwania mpira na mshambuliaji wa timu ya Boom Ally Kondo, katika Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup.     
    Baadhi ya wadau wa  Soka wakifuatilia mechi kati ya Tabata FC na Sifa Politan kwenye Uwanja wa Bandari.  
    Kiungo mshambuliaji wa timu ya Sifa Politan, Mathayo Edward (kulia) akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa timu ya Tabata FC, katika Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Bandari Dar es Salaam. Tabata ilishinda kwa Penati 4-3.    
     Mashabiki wa timu ya  Sifa Politan wakishangilia timu yao.
     Mashabiki wa timu ya Tabata FC wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga Sifa Politan kwa mikwaju ya penalti 4-3.
     Kipa wa Sifa Politan akiruka bila mafanikio kujaribu kuokoa penalti iliyopigwa na Kudura Shaban wa Tabata FC. 
    Heka Heka katika lango la timu ya BOOM FC.
     Mashabiki  soka wakifuatilia pambano la Sifa Politan na Tabata FC kwenye Uwanja wa Bandari.
    Wadau wa Soka wakifuatilia pambano la Sifa Politan na Tabata FC kwenye Uwanja wa Bandari.
     Mashabiki  soka wakifuatilia pambano la Sifa Politan na Tabata FC kwenye Uwanja wa Bandari.
     Mashabiki wa timu ya Tabata FC wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga Sifa Politan kwa mikwaju ya penalti 4-3.
    Mashabiki wa timu ya Tabata FC wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga Sifa Politan kwa mikwaju ya penalti 4-3.


  • MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 31.1O.2O14




    MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 31.1O.2O14
    .
    .
    26_b456f.jpg
    25_1b2fd.jpg


    24_85b3a.jpg


    27_65c72.jpg
    28_a51ca.jpg



  • October 30, 2014

  • TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI



    TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
    DSC00217
    MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA YASSINI HEZRON (14) MKAZI WA KIWIRA ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.235 AFB AINA YA M/CANTER LILILOKUWA LIMEBEBA MATOFALI LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE FREDY MPONDO KUSHINDWA KUPANDA MLIMA NA KISHA KURUDI NYUMA NA KUANGUSHA MATOFALI NA KUSABABISHA KIFO KWA TINGO HUYO.
    AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 29.10.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO MAENEO YA NEW LAND BAR, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA TUKUYU/KYELA. CHANZO CHA AJALI NI GARI HILO KUSHINDWA KUPANDA MLIMA NA KURUDI NYUMA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

    KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] KUZITOA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
    TAARIFA ZA MISAKO:
    JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. OTHAZ ANGOLILE (18) 2. SAMSON MWANGOMILE (46) 3. FORD SAMSON (20) NA 4. BARAKA JOSEPH (23) WOTE WAKAZI WA AIRPORT JIJINI MBEYA WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI AINA YA BOSS NA RIDDER PAKETI 108.
    WATUHUMIWA WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 29.10.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA MTAA WA AIRPORT, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI WA POMBE HIZO NA TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
    KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA/KUUZA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
    Imesainiwa na:
    [AHMED Z. MSANGI – SACP]
    KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.