August 11, 2014

  • MH. RIDHIWANI AZINDUA MRADI WA MAJI MBALA


    MH. RIDHIWANI AZINDUA MRADI WA MAJI MBALA
    Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akizindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Mbala kata ya Vigwaza.kushoto ni askofu mkuu wa Jimbo la Mashariki ya kanisa la Waadventista wasabato,Askofu Mark Malekana.

    Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akifungua maji kwenye bomba mara baada ya kuzindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Mbala kata ya Vigwaza.
    Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizindua mradi wa maji kwenye Kijiji cha Mbala hapa anaonekana akifungua maji kwa ajili ya kunyweshea mifugo.
    Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akinamama wa jamii ya kimasai baada ya kuzindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Mbala kata ya Vigwaza wilayani bagamoyo.

    Na John Gagarini, Bagamoyo

    IMEELEZWA kuwa maendeleo ya Tanzania yataletwa na Watanzania wenyewe na si kutegemea misaada mbalimbali toka kwa wafadhili wa kutoka nje ya nchi kama baadhi ya watu wanavyofikiri.

    Hayo yalisemwa jana kwenye Kijiji cha Mbala wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na askofu mkuu wa kanisa la waadventista wa Sabato Kanda ya Mashariki, Mark Malekana wakati wa uzinduzi wa mradi wa kisima cha maji kilichojengwa na wamuni wa kanisa hilo wa Manzese Jijini Dare s Salaam.

    Askofu Malekana alisema kuwa Watanzania wanapaswa kuhakikisha wanaanzisha miradi ya maendeleo kwa ustawi wananchi na si kutegemea kila kitu kutoka kwa wafadhili.

    "Ustawi wa nchi untegemea wananchi wenyewe kwani siyo kila jambo kuwategemea wafadhili hasa wale wan je lakini tukifanya wenyewe inaonyesha uzalendo na watu kuipenda nchi yao lazima tubadili mtazamo na kuanza kufadhili miradi sisi wenyewe," alisema Askofu Malekana.

    Aidha alisema kuwa kanisa hilo mbali ya kutoa huduma za kiroho pia imekuwa ikitoa huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na miradi ya maji, elimu na afya ambapo kanisa hapa nchini linamiliki vituo vya afya 34, shule za msingi 11, sekondari 15 na Chuo Kikuu kimoja.

    Kwa upande wake mgeni rasmi katika uzinduzi wa kisima hicho cha maji pamoja na sehemu ya kunyweshea mifugo, Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete changamoto ya maji ni kubwa na ailikuwa ikisababisha migogoro.

    Ridhiwani alisema kuwa migogoro hiyo inatokana na pande mbili baina ya wafugaji na wakulima ambapo maji wanayokunywa watu yamekuwa yakinyweshewa mifugo hali ambayo inasababisha migogoro baina ya pande mbili hizo.

    "Tunawapongeza waumini hawa wa Manzese kwa kuona umuhimu wa kuchimba kisima hicho ambacho kitasaidia kukabiliana na changamoto hiyo ya upatikanaji wa maji kwenye Kijiji hicho na vijiji jirani," alisema Ridhiwani.

    Alisema kuwa mbali ya changamoto hiyo pia wafugaji wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa majosho pamoja na madawa ya mifugo hali ambayo inasababisha vifo vya mifugo hiyo ambayo ni tegemeo kwa wafugaji katika kuendeshea maisha yao.

    Akisoma risala kuhusiana na mradi huo mkaguzi wa mali za kanisa hilo William Gomera alisema kuwa mradi huo mara utakapokamilika utasaidia kupunguza tatizo la maji kwenye eneo hilo la kijiji hicho na umegharimu kiasi cha shilingi milioni 76 na ulianza mwaka 2009. Mradi huo mbali ya kujengwa na waumini hao pia mradi wa maendeleo wa umoja wa mataifa (UNDP) hapa nchini, Taasisi ya Third Millenium Peace Initiative Foundation (TMPIF), Renewable Energy Development Company of Tanzania Ltd (REDCOT)


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.