Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Bw. John Hocking ambaye ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa (United Nations Mechanism for International Criminal Tribunals), iliyorithi shughuli za iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR). Bw. Hocking alitembelea Wizarani tarehe 10 Julai, 2014 kwa ajili ya kujadiliana na Mhe. Membe masuala mbalimbali ikiwemo mpango wa kuanza ujenzi wa Makao Makuu ya Mahakama hiyo katika eneo la Lakilaki Jijini Arusha.
Bw. Hocking akiagana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria wizarani hapo, Balozi Irene Kasyanju
0 comments:
Post a Comment