1. Ndugu Wanahakati.
2. Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Wasalaam.
Mtoto MELINA amakumbwa na matatizi makubwa sana. Anahitaji msaada wetu sote kama Watanzania na wapenda haki.
Melina ambaye amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi) ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar baada ya kujeruhiwa vibaya usoni na kichwani na bosi wake YASINTA RWECHUNGURA ambaye ni mwanasheria mkubwa nchini anahitaji msaada wako.
SIKU 730 au miaka miwili ya unyama na ukatili uliombatana na vipigo mfululizo, vimempa wakati mgumu katika maisha mtoto wa miaka 15, Melina aliyefika katika Jiji la Dar es Salaam mwaka 2012 akitokea kijijini Ishozi- Kiziba, Kagera kwa lengo la kufanya kazi za ndani, yaani 'hausigeli'.
Katika tukio la hivi karibuni na la kusikitisha, lilijiri Ijumaa iliyopita nyumbani kwa mwanamke huyo YASINTA RWECHUNGURA, Boko-Magengeni jijini Dar ambako Melina alikuwa akifanyia kazi.
Binti huyo ambaye wakati anafika jijini Dar alikuwa na miaka 12, licha ya umri wake kuwa mdogo alifanya kazi kwa bidii ili mshahara wake uweze kuwasaidia wazazi wake ambao hawajiwezi kimaisha kule kijijini.
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika, Melina alichukuliwa na bosi wake huyo kwa makubaliano ya mshahara wa shilingi 40,000 kwa mwezi huku shilingi 20,000 zikitumwa nyumbani kwao Kagera kwa wazazi wake.
"Lakini katika hali ya kushangaza, bosi wake alikuwa hampi zile shilingi 20,000 kama makubaliano yao yalivyokuwa akisema kwamba anamtunzia kuepuka matumizi mabaya.
"Ikaelezwa kuwa, akiwa ndani ya kazi, binti huyo alijikuta akipata mateso makubwa kama vile kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili kwa madai ya kukosa, kufanya kazi vibaya au tofauti na maelekezo," kilisema chanzo.
Akizungumza kwa uchungu na maumivu makali akiwa hospitalini hapo, Melina anaanza kwa kusema:
"Nimechoka sana ndugu zanguni, nimeteseka sana, nisaidieni nirudi kwetu Kagera. Kosa dogo napigwa na blenda na nyaya za kompyuta. Ndiyo maana sehemu mbalimbali za mwili hadi kichwani nina makovu kama hivi".
"Mara hii ya mwisho nilipigwa na kwanja la kufyekea ndiyo majeraha haya. Wakati akinitesa bosi wangu alikuwa akiniambia hakuna wa kumtisha. Nisaidieni jamani, miaka miwili ya mateso mfululizo sasa nataka kurudi kwa wazazi wangu japokuwa hawana uwezo tutaishi hivyohivyo tu. "
Mtoto huyo ana makovu (majeraha yaliyopona) 73 kichwani na mwilini mwake ambayo yote yanadaiwa yalitokana na adhabu ya mashambulizi ya kudhuru mwili ingawa haikubainika kama ni kutoka kwa bosi wake huyo au la!
Mnamo tarehe 11 Juni, mwaka huu (2014), saa 3 usiku, Melina alipelekwa katika hospitali binafsi iliyopo Mbezi, Dar akiwa na majeraha makubwa kichwani. Aliambatana na wanawake watatu, Mama Betty, Mama Winnie na mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Rwechungura (Anasemekana ndiye bosi wake).
Kwa kutotaka kuonekana kama wanahusika na huyo motto, walisema kuwa wao ni majirani wanaoishi karibu na binti huyo na walifika hospitalini hapo kwa lengo la kumsindikiza na kujua nini kinaendelea. Swali kama wao hawaishi nae bali ni majirani, je huyo anayeishi nae alikuwa wapi wakati mtoto anapata maswaibu hayo? Na kwanini hawakutaka kutoa namba zao za simu wapoombwa na daktari?
Daktari aliyekuwa zamu usiku huo inasemekana kuwa alishtushwa na hali ya Melina kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi usoni na kichwani.
Daktari kwa kutaka kujua zaidi kilichotokea ndipo akapasua jipu kwamba alikuwa amepigwa na bosi wake na kwamba hata makovu mengine ni majeraha yaliyopona ambayo yalitokana na kipigo cha mara kwa mara.
Habari zinazidi kudai kuwa, daktari huyo aliendelea kuokoa maisha ya Melina kwa kumshona nyuzi karibu kumi na mbili katika maeneo yaliyopasuka lakini kutokana na hali ya majeruhi kuwa mbaya, ilibidi aende kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi cha Kawe.
"Polisi walikwenda nyumbani kwa mwanasheria huyo, lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida walikuta nyumba haina mtu tena ikiwa wazi kwa usiku huo.
"Inasemekana katika wale wanawake watatu waliompeleka Melina hospitali, mtuhumiwa alikuwepo ila alitoroka baada ya polisi kuonesha nia ya kumkamata.
"Hali ya Melina ilizidi kuwa mbaya. Alfajiri ya Juni 12, mwaka huu ilibidi ahamishiwe kwenye Hospitali ya Mwananyamala ambapo alipokelewa na kupewa matibabu. Hali ikazidi kuwa mbaya, akahamishiwa Muhimbili.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kwamba, mtuhumiwa alitoroka lakini Jumamosi iliyopita alitiwa mbaroni maeneo ya Mbagala jijini Dar es salaam, tayari amefikishwa mahakama ya mkazi kinondoni. Kesi ya jinai namba 226/2014, itatajwa tena tarehe 1 Julai, 2014.
OMBI:
1. Wanaharakati nyote mnaombwa kuhudhuria siku hiyo ya tarehe 1 Julai, 2014 ili kumtia moyo huyo mtoto nakumfariji. Mtoto anahitaji msaada wa kisheria, ikiwemo na fedha za kujikimu.
2. Kurudishwa shule na kupata mfadhili wa kulipia masomo
3. Kumchangie mama mzazi wa huyo MELINA aweze kuja hapa Dar Es Salaam ili akamuguuze mtoto wake, ili mtoto aweze kuwa na amani na utulivu kwani kwa sasa hivi ana wasiwasi mkubwa mno kwa kuwazakuwa Yule mbaya wake atamfuata hospitalini na kuweza kumdhuru
TAARIFA ZA KUSIKITISHA
1. Mtuhumiwa kwa kushirikiana na ndugu zake wamemrubinu baba mtoto huyo, toka afike Dar es salaam hajawahi kuwasiliana na wajomba wa mtoto Melina ambao ndiyo yaliwasiliana na huyo jamaa kumjulisha aliyotokea huku
2. Inasemekana kuwa mipango inafanyika kuweza kupoteza ushaidi kwa namna yoyote iwayo. Mtoto ana wasiwasi sana na kila wakati anaomba wajomba zake wamtoe hospitali
3. Pia inasemekana YASINTA RWECHUNGURA kwa kutumia watu Fulani, na ambao walikwenda hospitali wakajitambulisha kwa baadhi ya madaktari kuwa wanahitaji waelewane nano (kuwaonga) ili wayamalize kimyakimya. Hapa maanake hayaeleweki. Kwa upande wa madaktari waliyoelezwa mambo hayo na ndugu zake huyo YASINTA RWECHUNGURA walikataa jambo la eti kuelewana nao. Maswali wametanda kwenye vichwa vya ndugu zake huyo motto MELINA, kuwa je, 1) usalama wa mtoto huyo utalindwa na uongozi wa hospitali ya Muhimbili? 2) Je, uongozi wa juu wa Muhimbili una taarifa hizo? 3) Je, huyo baba wa motto huyo ambaye ametoka nyumbani kagera bila kumshirikisha mamake motto ana nia njema? Kwani inasemekana mipango ilifanywa na ndugu zake YASINTA RWECHUNGURA yakumfuata huyo bwana huko kijijini na kuongea nae kutaka wayamalize.
4. Baba mtoto huyo amejificha au amefichwa na wabaya wa mtoto wake, swali je, nae anahusika? 1) Kwanini baada ya kupokea taarifa ya yaliyokea kwa motto wake aliamua kufanya vikao vya siri na ndgu zake YASINTA RWECHUNGURA na kuamua kutomtaarufu mke wake na kuamua kuja huku Dar es salaam kisirisiri?
Wanahakati tunawaomba mfuatilie kwa karibu suala hili na vilevile mlisimamie MELINA awe salama na apate haki stahili yake.
Tazama picha zake akiwa hospitali alikolazwa.
TUNAOMBA MSAADA WENU.

chanzo: www.wanawakelivetv.com
0 comments:
Post a Comment