December 14, 2014

  • TUZO KWA WANAMICHEZO BORA WA MWAKA MICHEZO MBALI MBALI ZATOLEWA


     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Waziri wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dr. Finella Mukangara (katikati) Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Abdilah Jihadi Hassan (kulia) wakiwa na Mwandishi wa Habari Salim Said Salim na Mama Fatma Karume wakiwa katika Hafla ya utoaji wa tunzo kwa wanamichezo bora kwa mwaka 2013/2014 katika ukumbi wa  Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam
     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi tunzo ya Heshma     Mama Fatma Karume mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Karume tunzo hiyo imetelolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)  kwa kutambua mchango mkubwa wa Mzee Karume kwenye michezo, ikiwa ni pamoja na kujenga majengo ya klabu za Yanga na Simba na mambo mengine mengi. Hafla hii ilifanyika  katika  ukumbi wa  Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
     Mama Fatma Karume mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Marehemu Mzee Abeid Karume  akiwa ameishikilia  tunzo ya Heshma baada ya kukabidhiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika hafla maalum ya utoaji wa tunzo hiyo  katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam
     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake fupi kwa wanamichezo mbali mbali katika hafla ya utoaji wa tunzo kwa wanamichezo bora  2013/2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam jana ambapo tunzo ya heshma ilitolewa kwa Mama Fatma Karume mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar  Marehemu Mzee Abeid Karume 
     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipomkabidhi Tunzo Mwanamichezo bora wa jumla wa Mwaka Sheridah Boniface wakati utoaji wa tunzo zilizoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Taswa katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam (kushoto)Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa Habari za Michezo TASWA Bw.Juma Pinto
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bara Dr. Finella Mukangara ,Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Abdilah Jihadi Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na wanamichezo waliopta tunzo zilizotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo katika ukumbi Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.