December 05, 2014

  • Rais Mugabe wa Zimbabwe asema 'Sing'atuki ng'o!' madarakani


    Rais Mugabe wa Zimbabwe asema 'Sing'atuki ng'o!' madarakani

    Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amelaumu watu fulani ndani ya chama tawala cha ZANU-PF kwamba wanapanga kumng'atua mamlakani.

    Akihutubia kongamano la chama hicho, Mugabe amesema kuwa kuna majaribio ya kuwahonga wajumbe kumpinga kama kiongozi, lakini wajumbe hawawezi kupokea hongo.


    Kwa hilo amesema kuwa atapambana na rushwa ndani ya chama na kukabiliana na maafisa wa chama ambao kazi yao ni kutoa hongo.Wanachama wengi wa chama hicho wangali ni wafuasi sugu wa Rais Mugabe


    Hasira ya Mugabe iliokana na madai ya njama ya kumuua yaliyotolewa dhidi ya naibu wake Joyce Mujuru. Hata hivyo Mujuru alikanusha madai hayo ambayo yamekuwa yakimuandamana.

    Mugabe alisema kutokuwepo kwa Bi Mujuru kwenye mkutano huo wa chama kunaonyesha kuwa anaogopa.


    Kadhalika Mugabe amesema Mujuru ni mwizi anayepanga kumuondoa mamlakani kwa kushirikiana na maafisa wengine wa chama.Maelfu ya wajumbe wa chama walihudhuria kongamano hilo mjini Harare


    Chama tawala cha Zimbabwe kinakumbwa na vita vya ndani kwa ndani kuhusu ni nani atakayerithi nafasi ya Mugabe ambaye ana miaka 91 na ameilongoza taifa hilo tangu lijinyakulie uhuru.

    Vilveile kiongozi huyo ametupilia mbali dhana ya kujiuzulu akisema ni upuzi .


    Hivi karibuni afisa mwingine mkuu wa chama tawala, Robert Gumbo aliambia BBC kwamba Mugabe amwenye umri wa miaka 90 amegeuza chama tawala na kukifanya mali yake binafsi.
    Bi Joyce Mujuru amedaiwa kupanga njama ya kumuua Mugabe ili achukue mamlaka kutokla kwake.


    Bwana Gumbo alisema kuwa lengo kuu la Mugabe ilikuwa kuendeleza uongozi wa chama kwa niaba ya mke wake Grace.

    Bi Mujuru ambaye amekanusha madai hayo alionekana kama mtu ambaye anegchukua uskani wa chama kutoka kwa Mugabe ambaye walipigania naye uhuru wa nchi hio kutoka mikononi mwa watwala wazungu. 

    CHANZO: BBC SWAHILI


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.