December 01, 2014

  • shindano la Ndovu Golden Experience lapata mshindi wake wa pili




    shindano la Ndovu Golden Experience lapata mshindi wake wa pili
    MSHINDI wa pili ya shindano la Ndovu Golden Experience Amand Kimario amewapiga kumbo washiriki wenzake katika shindano hilo na kujinyakulia nafasi ya kutembelea hifadhi ya Selous mwakani.

    Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt ambao ndio waratibu wa shindano hilo Pamela Kikuli alisema, lengo la kuandaa shindano hilo ni kwa ajili ya kuwapa fursa Watanzania kutembelea hifadhi na kujivunia utalii wao wa ndani.

    Pamela alisema, mshindi huyo amepatikana baada ya kuchezeshwa droo ambapo yeye aliwabwaga wenzake waliojitosa katika shindano hilo, ambapo atatarajiwa kuwa na mwenzake ambaye wataongozana katika hifadhi hiyo.

    Alisema, kwa kutambua bia yao ya Ndovu inabebwa na nembo ya mnyama Tembo, wanatumia nafasi hiyo kumlinda mnyama huyo kama kampeini yao inavyosema 'Ndovu Defance', ili kunusuru mauaji yake.

    "Utalii ni sekta muhimu sana katika kukuzauchumi wa Tanzania, ila utalii mkubwa unaofanyika hapa Tanzania ni wa wageni wa nje, hivyo basi tunaamini kwa kuendeleza kampeini yetu hii ya Ndovu Golden Experience, inayoendeshwa kwa kutumia namba za chini ya kizibo, itawapa fursa muhimu watanzania kujivunia utalii wao,"alisema Pamela.

    Aidha Pamela alisema, baada ya kumalizika kwa droo ya shindano hilo Disemba 18, washindi wataenda kutembelea hifadhi hiyo Januari mwakani huku wao Ndovu wakigharimia malazi, chakula pamoja na usafiri na kuwataka watanzania kuhakikisha wanatumia vyema fursa hiyo kwa kuandika namba chini ya kizibo kwenda namba 15499 au katika mtandao wa www.ndovuspecialmalt.com.
    Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli (kulia) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa kuchezesha droo ya pili ya kampeni ya "Ndovu Golden Experience" ya kusaka washindi wa kutembelea hifadhi ya Selous.Amandi Kimario mkazi wa Mbezi alishinda katika droo hiyo.Kushoto ni mwakilishi kutoka bodi ya kubahatisha nchini, Humudi Abdulhussein.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.