Mkuu wa Magereza                  Mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza,                  Hamis Nkubas akifanya mahojiano maalum Ofsini kwake na                  Waandishi wa Habari kutoka Vyombo vya Habari vya Habari                  Leo, Daily News, Michuzi Media na Gazeti la Tanzania                  Daima. Waandishi haowameanza ziara leo Desemba 15, 2014                  ambapo watatembelea katika miradi mbalimbali ya                  uzalishaji mali inayotekelezwa kwa mafanikio na Jeshi la                  Magereza.
                                          Viti vya Ofisi ambavyo                  vimetengenezwa katika Kiwanda cha Samani Arusha cha                  Jeshi la Magereza. Viti hivyo vitatumiwa katika Ofisi za                  Jimbo kwa Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri                  Muungano wa Tanzania.
                                          Viatu vya ngozi                  vinavyotengenezwa kwa ustadi mkubwa katika Kiwanda cha                  Viatu vya ngozi cha Gereza Kuu Karanga Moshi kama                  vinavyoonekana katika picha.
                                          Waandishi wa Habari                  wakiangalia vya ngozi vinavyotengenezwa katika Kiwanda                  cha ngozi cha Gereza Kuu Karaga Moshi(wa pili kushoto)                  ni Mwandishi kutoka Daily News, Bw. Fining Simbeye(wa                  tatu kushoto) ni Mwandishi kutoka Gazeti la Tanzania                  Daima, Bw. Edson Kamkara.
                                          Mkuu wa Magereza                  Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa                  Magereza, Venant Kayombo(wa tano kushoto) akiwa katika                  picha ya pamoja na Waandishi wa Habari kutoka Magazeti                  ya Daily News, Tanzania Daima, Habari Leo pamoja na                  Globu ya Michuzi(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la                  Magereza).
          
0 comments:
Post a Comment