Mahmoud Ahmad Arusha
Serikali Mkoani Arusha Imewataka wakazi wa Mkoa huo Kuhakikisha kuwa wanaendelea kudumisha Amani,Umoja na Mshikamano sanjari na kujitolea katika kufanikisha shughuli za kimaendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na katibu Tawala wa mkoa huu Addo Mapunda wakati akiongea na wanahabari ofisini kwake ambapo alisisitiza
wakazi wa mkoa huu kufuata sheria kanuni na taratibu za nchi ikwemo usafi wa mazingira.
Aliwatahadharisha wananchi hao kutofuata mkumbo na kujihusisha na ushabiki wa baadhi ya vyama vya siasa ambavyo vimekuwa vikiendesha siasa za chuki,udini na uhasama jambo ambalo limekuwa likiwagawa wananchi katika makundi na kupelekea uwepo wa vitendo vya uvunjifu wa amani.
"napenda kuwakukumbusha wananchi wa mkoa wa Arusha kuwa suala la maendeleo sio la Serikali pekee bali ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa nashiriki kikamilifu katika shughuli za kujiletea maendeleo"alisema Mapunda.
Akizungumzia shule za Sekondari za Kata amesema kuwa Serikali imejipanga kikamilifu na tayari umaliziaji wa majengo ya maabara na vyumba vya madarasa uko katika hatua za mwisho kabisa kukamilika na kuwataka wananchi kuepukana na dhana potofu kuwa shule za Kata hazina viwango vizuri vya ufaulu wa wanafunzi.
Mapunda amesema kuwa Mkoa wake umejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani ambaye atakosa kujiunga na shule kwa uhaba wa vyumba vya madarasa kwani mkoa umejipanga kikamilifu kukabiliana na changamoto hiyo.
Kuhusu suala la uchaguzi wa serikali za mitaa alisema kuwa anashukuru uchaguzi huo umekwenda kwa mafanikio na kuwa wananchi walipewa fursa zxa kuwachaguwa viongozi wanaowataka.
"Kikubwa ni wananchi kupewa fursa za kuwachagua viongozi
wanowataka bila ya kuwepo shinikizo hali ambayo imekuwa ikichangia uvunjifu wa Amani ndio maana umeona mkoa huu hauna matukio ya uvunjifu wa amani kama ilivyokuwa kabla"
0 comments:
Post a Comment