December 23, 2014

  • ‘NIMEKUJA KUFANYA MAPINDUZI YA KIUCHUMI NDANI YA YANGA’- DR TIBOROHA


    'NIMEKUJA KUFANYA MAPINDUZI YA KIUCHUMI NDANI YA YANGA'- DR TIBOROHA

    TIBO
    Katibu mkuu wa YANGA Dr Tiboroha akizungumza na waandishi wa habari,pembeni yake ni Jerry Muro mkuu wa idara ya mawasiliano ya klabu hiyo 

    Katibu mkuu mpya wa YANGA Jonas Tibohora aahidi makubwa kwenye klabu hiyo, Katibu mkuu huyo mpya leo amezungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani.
    DrJonas Tibohora amesema anataka kuiongoza Yanga kujiendesha kiuchumi, katika mpango wake huo anataka kuanza kutengeneza kikosi imara cha ushindani ikiwa ni pamoja na kutengeneza mifumo bora ya soka la vijana klabuni hapo
    Lengo kubwa la kuwekeza kwenye timu za vijana ni kujalibu kupunguza ghalama za kununua wachezaji kutoka nje,pia amesema sasa ni muda wa klabu hiyo kunufaika na nembo ya klabu hiyo kibiashara.



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.