Na Immaculate Makilika- MAELEZO
WADAU wa elimu nchini wanatarajiakuwa na kongamano ambalo litakuwa likijadili juu ya uboreshaji wa elimu nchini.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kongamano la Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Job Chaula amesema kuwa kongamano hilo litasaidia kutafuta mbinu kuhusu nini kifanyike kuboresha zaidi elimu ya Tanzania.
Dkt. Chaula ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa kongamano kubwa linalotarajiwa kuleta ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili sekta ya elimu nchini.
Amesema kuwa sio wakati wa Watanzania kulalamikia Serikali na badala yake wanapaswa wajitume ili kubadilisha hali iliyopo.
Dkt Chaula ameongeza kuwa elimu ya Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi, kama vile mtazamo wa hasi wa baadhi ya jamii wa kupenda kuwaoza mabinti wao wakiwa na umri mdogo na hivyo kuwanyima fursa ya elimu.
Naye Katibu wa Kamati ya Kongamano la Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Maulid Nkungu amesema kuwa pamoja na changamoto hizo zinazoikabili Sekta ya elimu nchini,Serikali imekuwa ikijitahidi kuboresha elimu nchini.
Amesema kuwa ni wakati wa wadau kushirikiana na Serikali kuboresha elimu kwa kuweka nguvu za pamoja katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zitakabili elimu nchini.
Kongamano hilo litafanyika mkoa wa Dar es salaam litakalofanyika tarehe 5/7/2014 Ubungo plaza .
Kauli mbiu ya kongamano hilo ni "Elimu Tanzania,nini kifanyike".
0 comments:
Post a Comment