July 15, 2014

  • MRADI WA MIL 700/- WA MATUMIZI YA RASILIMALI ENDELEVU USAMBARA WAANZA


    MRADI WA MIL 700/- WA MATUMIZI YA RASILIMALI ENDELEVU USAMBARA WAANZA
    DSC_0008
    Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko, (kulia) akisalimiana na Mtendaji wa Kata ya Mnyuzi, Bw. Gosbert Ishengoma mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za kata hiyo wilayani Korogwe. Katikati ni Afisa Usafi na Mazingira wa Wilaya ya Korogwe, Bw. Frederick Linga.

    Na Mwandishi wetu, Korogwe
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limezindua mradi wa mamilioni katika eneo la hifadhi Usambara Mashariki, kwa mafunzo kwa wakazi waliomo na wanaozunguka hifadhi ya Usambara Mashariki.

    Mradi huo ambao umelenga kuwainua wanavijiji kiuchumi huku wakitunza mazingira umepata fedha kutoka Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Kimataifa la Korea ( KOICA).
    Mradi huo unaotekelezwa katika vijiji 19 vinavyozunguka Hifadhi Hai ya usambara mashariki ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai(GEBR).

    Mradi huo utawawezesha wananchi kwenye vijiji hivyo kutumia raslimali zao kwa namna endelevu. Mradi huo unaojulikana kama "Green Economy in Biosphere Reserves (GEBR)",wenye thamani ya shilingi milioni 700 utapunguza ukataji miti na kulinda hifadhi kwa kutumia raslimali kwa busara zaidi.

    Mradi huo unatarajiwa kuwezesha wananchi wa maeneo hayo kupunguza umaskini kwa kutumia raslimali zilizopo kwa busara na wakati huo huo kuhifadhi mazingira.
    DSC_0012
    Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko, akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi za kata ya Mnyuzi mara baada ya kuwasili wilayani hapo kwa ajili ya kuzindua mradi wa mamilioni katika eneo la hifadhi Usambara Mashariki, na kuendesha mafunzo kwa wakazi waliomo na wanaozunguka hifadhi ya Usambara Mashariki.




  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.