July 15, 2014

  • NAIBU WAZIRI WA MAJI, MAKALLA AWANASA WEZI WA MAJI DAR NA KUTANGAZA KUFILISI MALI ZAO.



    NAIBU WAZIRI WA MAJI, MAKALLA AWANASA WEZI WA MAJI DAR NA KUTANGAZA KUFILISI MALI ZAO.

    Meneja Mkuu wa Kampuni ya ufyatuaji matofali ya Ujenzi Solutions, ya Kimara kwa Msuguri, Dar es Salaam, Rahim Hamis na mfanyabiashara wa kampuni isiyo na jina, Credo Rajab (kulia) wakiwa chini ya uliznzi wa Polisi huku wakiwa wamevishwa pingu baada Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla kuamuru kuwakamata alipokagua viwanda vyao vya ufyatuaji na kugundulika kuwa wanatumia maji isivyo halali kwa kujiunganishia kwenye bomba kuu la Mamlaka ya Maji Safi na Taka Dar  ws Salaam (DAWASA).  Makalla ambaye alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya upanuzi wa Matambo wa Maji wa Ruvu Juu, Mlandizi, mkoani Pwani , pia alifanya msako wa kushitukiza kwa kampuni hizo.
    Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia) akijaribu kuendesha katapila la Kampuni ya Ujenzi ya VA Tech Wabag Ltd, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya upanuzi wa Mitambo ya Maji ya Ruvu Juu, Mlandizi, mkoani Pwani .Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa na Meneja Mradi wa kampuni hiyo, Pintu Dutta.
    Askari wa FFU wakilinda doria katika kiwanda cha ufatuaji tofali cha Ujenzi Solutions, Kimara Dar es Salaam
    Moja ya mabomba linalodaiwa kuunganishwa kiholela kwenye bomba kuu la Ruvu Juu linaloleta maji  mjini na kampuni ya Ujenzi Solutions eneo la Kimara
    Makalla akizungumza mbele ya Lori la Maji lililokamatwa likijazwa maji yanayodaiwa kuwa ya Dawass, katika kiwanda cha matofali cha Ujenzi Solutions.



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.