July 01, 2014

  • ALGERIA YAPIGWA 2-1 NA UJERUMANI NA KUTOLEWA KOMBE LA DUNIA

     
     
     
     

    Mesut Ozil akishangilia baada ya kuifungia Ujerumani bao la pili
    AFRIKA imetolewa kabisa katika Kombe la Dunia baada ya wawakilishi wake waliobakia Algeria, kufungwa mabao 2-1 na Ujerumani katika mchezo wa 16 Bora usiku huu Uwanja wa Beira-Rio mjini Porto Alegre.
    Ni hitimisho la siku nyingine mbaya kwa Waafrika, baada ya awali, wawakilishi wengine waliofika hatua hiyo, Nigeria kutolewa na Ufaransa kwa mabao 2-0.Maana yake, Cameroon, Senegal na Ghana zinabaki kuwa timu zenye mafanikio zaidi miongoni mwa nchi za Afrika kwenye Kombe la Dunia kwa kuweza kufika Robo Fainali za michuano hiyo. Simba Wasiofungika walianza 1990 Italia, Simba wa Teranga wakafuatia 2002 Korea na Japan na Nyota Weusi wakamalizia 2010 Afrika Kusini. 
    Dakika 90 za mchezo kati ya Ujerumani na Algeria zilimalizika timu hizo zikiwa hazijafungana, lakini katika 30 za nyongeza mabao ya Andre Schurrle 92 na Mesut Ozil 119 yaliwafuta kabisa Waafrika katika Kombe la Dunia 2014 Brazil, mapema zaidi kuliko fainali zilizopita Afrika Kusini.
    Abdelmoumene Djabou aliifungia Algeria bao la kufutia machozi dakika ya mwisho kabisa, Ujerumani ikienda Robo Fainali.
    Kikosi cha Ujerumani kilikuwa; Neuer, Mustafi/Khedira dk70, Mertesacker, Boateng, Howedes, Lahm, Ozil, Schweinsteiger/Kramer dk109, Kroos, Gotze/Schurrle dk46 na Muller.
    Algeria: M'Bolhi, Mandi, Belkalem, Halliche/Bougherra dk98, Ghoulam, Lacen, Mostefa, Feghouli, Soudani/Djabou dk100, Taider/Brahimi dk79 na Slimani.
    Andre Schuerrle of Germany scores his team's first goal past goalkeeper Rais M'Bolhi of Algeria
    Andre Schuerrle akiifungia Ujerumani bao la kwanza dhidi ya kipa Algeria, Rais M'Bolhi
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.