July 13, 2014

  • TBS KUPEWA KIBALI CHA KUAJIRI WAFANYAKAZI 200



    TBS KUPEWA KIBALI CHA KUAJIRI WAFANYAKAZI 200

    Serikali  inatarajia kutoa vibali vya kuajiri  wafanyakazi 200 katika Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na zaidi ya asilimia 95 ya wafanyakazi hao wataongeza nguvu katika kutayarisha na kusimamia viwango vya ubora. 
    Hayo yalisemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda, juzi wakati wa kufungua mkutano wa siku mbili wa  Baraza la Wafanyakazi wa shirika hilo mjini Morogoro.Waziri Kigoda alisema Serikali inatambua umuhimu wa shirika hilo  hapa nchini hususan katika kuchangia uchumi wa nchi, kusimamia afya, usalama na ustawi wa watu, kusaidia kuwalinda walaji, kuchangia biashara za ndani na nje ya nchi na kusimamia ushirikiano wa Kimataifa katika nyanja za viwango. Kwa mujibu wa Waziri huyo, changamoto kubwa zinazolikabili shirika hilo ambazo ni pamoja na uhaba wa watumishi,  vifaa vya maabara,  fedha za maendeleo na matumizi ya kawaida, uelewa mdogo wa umma na Jumuiya ya Wafanyabiashara juu ya dhana nzima ya viwango na ubora. 
    "Changamoto hizi Serikali inazifanyia kazi na kwa mwaka ujao wa fedha kwa maana 2014/2015 ,Serikali inatarajia kuongeza wafanyakazi 200 ambao wengi wao watasaidia katika kuweka na kusimamia viwango," alisema.Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBS, Profesa Cuthbert Mhilu, alisema kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 , TBS ilipewa vibali vya kuajiri wafanyakazi 45 na mwaka huu wa fedha wa 2014/2015 inatarajia  kupewa vibali vya kuajiri wafanyakazi wapatao 200 , zaidi ya asilimia 95 ya wafanyakazi hao wataongeza nguvu katika kutayarisha na kusimamia viwango vya ubora.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.