July 04, 2014

  • KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AMFAGILIA MBUNGE FILIKUNJOMBE KWA KUFANUIKISHA MAENDELEO LUDEWA , AMPONDA DIWANI KWA KUUKWEPA MWENGE


    KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AMFAGILIA MBUNGE FILIKUNJOMBE KWA KUFANUIKISHA MAENDELEO LUDEWA , AMPONDA DIWANI KWA KUUKWEPA MWENGE

    Mmoja kati ya  wakimbiza mwenye Kitaifa  kulia akimpongeza mbunge Deo Filikunjombe kwa kasi yake kubwa ya maendeleo jimboni

    Mwenge  wa Uhuru  ulipowasili wilaya ya  Ludewa  eneo la Madope mpakani mwa Njombe na Ludewa
    Mbunge wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe akiwa ameushika  vema mwenge wa  Uhuru wakati wa Risala ya  utii ya wananchi wa Ludewa   kwa Rais Dr Jakaya  Kikwete  ikisomwa katika  viwanja  vya mkesha eneo la Manda  Picha na Francis Godwin Blog)
    Watoto wea  kijiji cha Mlangali  wakifurahi  kushika  mwenge wa Uhuru
    Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Rachel Kassanda akimpongeza mwanamke mwenye ulemavu wa macho Bi Regina Kayombo  kwa  ujenzi wa nyumba ya  kisasa

    Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru taifa Rachel Kassanda akionya  utumiaji wa madawa ya kulevya  huku mmoja kati ya askari akichochea bangi iliyoteketezwa na kiongozi huyo wilayani Ludewa
    Mwananchi wa Ludewa mjini akishiriki kukimbiza Mwenge baada ya  kuzindua ujenzi wa barabara ya lami mjini Ludewa
    Vijana  wakimbiza mwenge  kitaifa  wakiondoka eneo la Manda leo asubuhi
    kiongozi wa mbio za mwenge  wa Uhuru Kitaifa Rachel Kassanda wa  tatu kulia akiruka kwa ukakamavu na  askari wengine wakati wa mbio hizo wilayani Ludewa
    Mwenge wa Uhuru  ukikimbizwa katika barabara  inayojengwa kwa kiwango cha  lami  mjini Ludewa

    Bi Ragena Kayombo akiwa ameshika mwenge wa Uhuru
    Bw Khamis Kayombo akiwa ameshika  mwenge wa Uhuru
     Mtoto Sabina  Kayombo wa Mlangali Ndani  akiwa ameshika mwenge wa Uhuru 
    ....................................................................................................................
      Na Francis Godwin Blog -Ludewa 
    KIONGOZI  wa  mbio  za  mwenge  wa  uhuru  kitaifa Rachel Kassanda amempongeza mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe kwa  jitihada mbali mbali  za kimaendeleozinazofanyika katika  jimbo  hilo  na  huku akimshambulia  diwani  wa kata la Mlangali Faraja Mlelwa (Chadema) kwa kushindwa  kushiriki  mbio za mwenge katika kata yake.

    Alisema kuwa miradi 7  yenye  thamani ya  zaidi ya Tsh bilioni 3 ambayo mwenge wa Uhuru mwaka 2014  unaipitia  katika jimbo la Ludewa na  wilaya ya Ludewa kuwa ni miradi mikubwa ambavyo ni  wazi mbunge  wa jimbo  hilo Filikunjombe amefanya kazi kubwa hasa ukilinganisha na majimbo mengine ambayo miradi  yake haifikii thamani  hiyo .

    Kiongozi   huyo alitoa pongezi  hizo  leo   wakati wa  kuzindua nyumba ya bora ya mkazi wa Mlangali Ndani Khamis Ignas Kayombo .
    Kiongozi  wa mbio za mwenge kitaifa Rachel Kassanda  akimpongeza  mbunge wa jimbo la LudewaDeo Filikunjombe kwa kanzi nzuri ya  kuwaletea wana Ludewa maendeleo
    Alisema  kuwa  mbio  za  mwenge  wa  Uhuru  zimekuwa  zikihamasisha  maendeleo  katika maeneo  mbali mbali na viongozi  wapenda  maendeleo  wakiwemo wabunge na madiwani hawana budi kushiriki mbio  hizo kama  ambavyo  wananchi  wana  wamekuwa  wakifanya .

    Kwani alisema  hata kama  diwani  huyo alikuwa na majukumu yake  binafsi hakupaswa kuwakimbia  wananchi  wake  ambao wamejitokeza kuupokea  mwenge  na  kuwa  kitendo cha  diwani kushindwa  kushiriki ni  wazi  kuwa ni diwani asiyependa maendeleo  katika eneo lake.
    Mbunge wa jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe kulia akimtazama mwandishi wa TBC Bw Msigwa wakati akiendelea kukusanya habari za mwenge
    "Ndugu  zangu  watanzania  na  wananchi  wa Mlangali wilaya ya  Ludewa kwanza  napenda kumpongeza mbunge  wenu Deo Filikunjombe natambua jitihada mbali mbali za kimaendeleo ambazo amekuwa akizifanya ndani ya  jimbo la Ludewa na nje ya jimbo kwa maana ya mchango  wake  mkubwa katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania  ila ninapenda kuwaeleza  wazi  kuwa ni  viongozi  wachahe wa  kisiasa ambao  wamekuwa  wakiacha posho bungeni na kushiriki mbio za mwenge kama ilivyo kwa Filikunjombe ninampongeza sana  ila kama kiongozi wa  mbio za mwenge sijapendezwa na kitendo  cha diwani wenu kushindwa kufika hapa  leo "

    Hata  hivyo alisema wananchi hawana  sababu ya kuendelea  kuwasikiliza viongozi  wa vyama vya siasa ambao  wamekuwa  wakipinga mbio  za mwenge kwani  mwenge wa Uhuru si mwenge wa chama  cha siasa ila  upo kwa ajili ya  watanzania  wote na ni  sehemu ya kudumisha mshikamano  wetu na kuenzi amani yake pamoja na kuhamasisha maendeleo miongoni mwetu.
    Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Rachel Kassanda akiwa na Bw Khanmis Kayombo na mkewe baada ya  kuzindua nyumba yao ene la Mlangali Ndani

    Hivyo kiongozi yeyote wa kisiasa ni lazima  kuendelea  kuenzi mshikamano  wetu na kushiriki katika mbio  hizo ambazo  zilihasisiwa na baba wa Taifa hayati Julius Nyerere ambae kwa sasa kanisa la RC limepata  kumtangaza kuwa miongoni mwa  watakatifu kutokana na mchango  wake mkubwa wa  kuliletea taifa  hili uhuru wake.
    Pia  alisema kuwa  wapinzani  wanaosema Mwenge wa Uhuru  umepitwa na wakati na wakiingia madarakani watauweka katika jumba la makumbusho  hawana nia njema na nchi  hii na kuwataka  watanzania  kuwapuuza watu hao na ikibidi  watu  hao kwenda  kumwomba radhi mjane wa baba wa Taifa Maria  Nyerere ambae kitendo  cha  wao  kuusemea  vibaya mwenge  huo ni sawa na kumtukana baba wa Taifa


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.