Gwiji: Mourinho (kushoto) alimleta Drogba Chelsea mwaka 2004 kutokea klabu ya Marseille.
NDOTO ya Didier Drogba kurudi tena Chelsea inatarajia kukamilika wiki hii.
Mazungumzo ya kumpa mkataba wa mwaka mmoja wa ukocha na mshambuliaji wa akiba yamekuwa yakiendelea vizuri na kuelekea kukamilika na gwiji huyo wa darajani mwenye miaka 36 ataungana na kocha wake wa zamani, Jose Mourinho.Inafahamika kuwa Drogba ameshawatumia ujumbe baadhi ya wachezaji wenzake wa zamani wa Chelsea akieleza kuwa anarudi darajani.
Nyota huyo mwenye miaka 36 amezivutia klabu kadhaa nchni Qatar, wakati Juventus wakipambana namna ya kuinasa saini yake.
Chelsea inataka kupunguza wachezaji wenye umri mkubwa kwenye kikosi chake, lakini inatambua mchango wa Drogba nje na ndani ya uwanjani.
Wanaamini kuwa uzoefu wa mshambuliaji huyo utakuwa na ushawishi mkubwa katika benchi la ufundi na atatoa msaada kwa nyota mpya, Diego Costa.
Chelsea wametumia vizuri majira haya ya kiangazi na wataendelea kuongeza wachezaji, lakini wamempoteza Samuel Eto`o na Demba Ba, wakati Romelu lukaku anaweza kujiunga na Everton licha ya awali kuwepo kwa mipango ya kumrudisha.
Kuwa kocha mchezaji kutasaidia kwenda na sheria ya matumizi ya fedha kwasababu mshahara wake utaingia kwenye bajeti ya makocha.
Drogba alisaini kwa mara ya kwanza Chelsea miaka 10 iliyopita na kuondoka mwaka 2012.
Kuthibitisha kuondoka kwake, Drogba aliiambia tovuti ya klabu kuwa: "Nataka kumaliza tetesi zote na kuthibitisha kwamba naondoka Chelsea. Yamekuwa maamuzi magumu kwangu kufanya na ninajivunia kwa kile tulichopata".
"Lakini muda wa changamoto mpya kwangu umefika. Kama sehemu ya timu nimesaidia sana na kushinda kila kombe lililowezekana".
Drogba alipokuwa akiwashukuru mashabiki wa Chelsea katika mchezo wake wa mwisho ndani ya dimba la Stamford Bridge.
0 comments:
Post a Comment