July 14, 2014

  • TANZANITE ONE WAKABIDHI MSAADA WA SHILINGI MILIONI 42 KWENYE SHULE YA MSINGI NEW VISION



    TANZANITE ONE WAKABIDHI MSAADA WA SHILINGI MILIONI 42 KWENYE SHULE YA MSINGI NEW VISION
    Hiyo ndiyo mfano wa hundi ya shilingi milioni 42 iliyotolewa na kampuni ya TanzaniteOne kwa shule hiyo ya New Vision ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ambapo ina wanafunzi 400 kati yao 67 ni watoto yatima (kushoto) ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya TanzaniteOne Halfani Hayeshi.
     Katibu Tawala wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Elias Ntiruhungwa akionyesha picha iliyochorwa na mwanafunzi wa shule ya msingi New Vision, Gift Junior baada ya shule hiyo kukabidhiwa msaada wa sh42 milioni na kampuni ya TanzaniteOne kulia ni Mkurugenzi wa shule hiyo Recho Robinson Mneney.
     Mchungaji wa KKKT, Usharika wa Imanueli, Dayosisi ya Meru, Ernest Mola, ambaye pia ni Mwenyekiti wa bodi ya shule ya msingi New Vision akisoma risala ya shule hiyo kwenye hafla ya shule hiyo kukabidhiwa sh42 milioni na kampuni ya kuchimba madini ya TanzaniteOne.

     Ofisa wa Polisi Jamii Tarafa ya Moipo Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, As/Insp Amiry Mlemba akiwa kwenye tafrija ya shule ya msingi New Vision ya Mji mdogo wa Mirerani kukabidhiwa sh42 milioni na kampuni ya kuchimba madini ya TanzaniteOne.

     Wanafunzi wa shule ya msingi New Vision wakishuhudia tukio la shule hiyo kukabidhiwa sh42 milioni na kampuni ya TanzaniteOne.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.