July 14, 2014

  • Taarifa Maalum Kwa Umma Kutoka Wizara ya Maji:Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe leo anatarajia kwenda nchini India ili kutoa shukrani kwa serikali ya nchi hiyo pamoja na kuishawisihi serikali ya nchi hiyo kupanua ufadhili na mikopo yake katika miradi ya maji nchini Tanzania.



    Taarifa Maalum Kwa Umma Kutoka Wizara ya Maji:Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe leo anatarajia kwenda nchini India ili kutoa shukrani kwa serikali ya nchi hiyo pamoja na kuishawisihi serikali ya nchi hiyo kupanua ufadhili na mikopo yake katika miradi ya maji nchini Tanzania.
    Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe
    ---
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
    WIZARA YA MAJI  
     
    Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe leo anatarajia kwenda nchini India ili kutoa shukrani kwa serikali ya nchi hiyo pamoja na kuishawisihi serikali ya nchi hiyo kupanua ufadhili na mikopo yake katika miradi ya maji nchini Tanzania.

    Katika ziara huyo, Prof. Maghembe ataongozana na, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwasa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mbogo Futakamba, Mkurugenzi wa Uratibu Programu Joseph Kakunda pamoja na Mkurugenzi wa Huduma ya Maji Mijini Mhandisi Justus Rwetabula.  

    Akizungumza ofisini kwake, Mkurugenzi wa Uratibu Programu Wizara ya Maji, Joseph Kakunda alisema, lengo la safari hiyo ni kutoa shukrani kwa serikali ya India, kuelezea mwenendo wa miradi ya maji inayotekelezwa na makandarasi ya India na kuiomba serikali ya India kupanua wigo wa misaada yake katika sekta ya maji nchini. 

    "Lengo la safari hii ni kwenda kuishukuru serikali ya India kwa misaada yake katika sekta ya maji nchini, pia kwenda kujadili namna miradi ya maji inayojengwa na wakandarasi wa India jinsi inavyotekelezwa kwani zipo kampuni za India zinazotekeleza miradi ya maji kwa ufanisi na pia zipo zinazosuasua na mwisho kuiomba serikali ya India ipanue wigo wake katika kuisaidia sekta ya maji nchini" Alisema Kakunda.

    Katika ziara hiyo, Waziri Maghembe na msafara wake watakutana na Waziri wa Rasilimali za Maji wa India na Viongozi wa juu wa Wizara hiyo nchini humo. Pia atakutana na viongozi wakuu wa kampuni ya ujenzi ya WAPCOS kwenye makao makuu ya kampuni hiyo.

    Kadhalka Waziri Maghembe na msafara wake watakutana na viongozi wa juu wa Wizara ya Fedha wa India pamoja na Idara ya Mikopo kwa nchi zinazoendelea.

    Baada ya hapo msafara huo utakutana na Uongozi wa Mamlaka ya Majisafi Jijini New Delhi kwa ajili ya kupata uzoefu wa namna Mamlaka za maji za miji zinavyoendeshwa.

    Msafara huo unatarajiwa kurudi Dar es Salaam Jumamosi, tarehe 19/07/2014 ili kuendelea na shughuli nyingine za kulijenga Taifa.
     Serikali ya India imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Tanzania katika sekta ya maji kwa miaka mingi sasa. Ushirikiano wao umeanza tangu mwaka 1975 kwa kuwajengea uwezo wahandisi wa maji nchini.

    Kwasasa India inafadhili miradi kadhaa ya maji nchini ukiwemo mradi wa maji wa Chalinze na upanuzi wa mradi wa maji wa Ruvu juu chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).


    Imetolewa na;

    ATHUMANI SHARIFF

    COMMUNICATION OFFICER
    MINISTRY OF WATER 
     Contacts; 0713881647



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.