Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma akimvisha kofia ya ukamanda Profesa Peter Msolla baada ya kuteuliwa kuwa Kamanda wa UVCCM wilaya ya Kilolo sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Kidabaga.
Mbunge wa jimbo la Kilolo,Profesa Peter Msola akila kiapo cha kuwa kamanda wa UVccm mbele ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma.
Mbunge wa jimbo la Kilolo,Prof Peter Msola akiwaapisha makamanda wa vijana ccm katika wilaya ya Kilolo sherehezz ilizofanyika katika uwanja wa Kidabaga.
Na Denis Mlowe,Kilolo
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Sadifa Juma Hamis ametoa rai kwa vijana kuepuka kutumika katika kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini Tanzania kwa kutumika na baadhi ya vyama vya siasa na kuhatarisha amani ya Taifa.
Sadifa alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Kidabaga wakati akiwahutubia wananchi wa Kidabaga kata ya Bomalang'ombe wilayani Kilolo wakati wa kusimikwa kwa mbunge wa jimbo la Kilolo Prof. Peter Msola kuwa kamanda wa umoja wa vijana CCM wa wilaya ya hiyo.
Alisema kuwa amani ambayo tunajivunia ipo siku itatoweka na iwapo vyama vya siasa vitaacha kufanya kazi yake ya kisiasa kwa kunadi sera za vyama vyao na kueneza chuki dhidi ya serikali kama ilivyo hivi sasa kwa baadhi ya vyama kuendesha siasa za chuki na kuwatumia vijana kuvuruga amani yetu.
" Nawaombeni sana vijana wa kuendelea kuonyesha mfano kwa vijana bora katika kudumisha amani iliyopo na kamwe msije iga siasa vya vyama vya upinzani siasa ya kufanya vurugu ..... hiyo ni siasa mbaya sana na itakuja kuliweka Taifa katika umwagaji damu ambao hakika itakuwa ngumu sana kuweza kuishi tena kama mwanzo" alisemaSadifa
Alitoa mfano kuwa kuna ushahidi kwa nchi jirani unaonesha madhara ya kuichezea amani na kuongeza kuwa ni rahisi sana kupoteza amani na umoja lakini ni vigumu sana kuirejesha na kuwataka vijana kuacha kuandamana kwa kuiga tu kwa kuwa umeambiwa fanya jambo hilo
Mbali ya kuwataka vijana kuacha kutumiwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa Sadifa aliwataka viongozi wa vyama vya siasa kutowatumia vijana hao katika kuvuruga amani pia aliwataka vijana kutokubali siasa chafu zenye chembe ya vurugu kwa watanzania na kuongeza kuwa sehemu yoyote yenye amani na utulivu, yapo maendeleo kwa sababu wananchi wanafanya shughuli za maendeleo kwa uhuru
Kwa upande wake Kamanda mpya wa umoja wa vijana Ccm wilaya ya Kilolo, Prof Peter Msola aliwataka vijana kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuondokana na umaskini katika wilaya hiyo na kuwataka kushirikiana katika kudumisha amani iliyopo nchini Tanzania.
Alisema moja changamoto kubwa inayowakabili vijana na ambayo kwa kushirikiana nao atahakikisha inafanyiwa kazi kwa kutumia fursa mbalimbali zinazowazunguka ni ajira kwa kuwa fursa hizo zinaweza kuwa katika sekta ya biashara, kilimo na ushauri kwa kupitia vikundi vya maendeleo.
Alisema ardhi na hali ya hewa nzuri ya wilaya ya Kilolo inaweza kuwaongezea fursa ya ajira vijana wa wilaya hiyo.
0 comments:
Post a Comment