July 12, 2014

  • NYALANDU AIFANYIA KAZI VIDEO YA MCH MSIGWA


    NYALANDU AIFANYIA KAZI VIDEO YA MCH MSIGWA
    nyalandu_013cf.jpg
    Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza kufuta vitalu vyote vilivyokuwa chini ya Kampuni ya Green Miles Safaris Ltd kutokana na kukiuka sheria za uwindaji nchini, huku akiifuta Idara ya Wanyamapori. amuzi huo wa Serikali, umekuja siku chache baada ya Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa kuonyesha video inayoihusisha kampuni hiyo na ukiukaji wa sheria na taratibu za uwindaji.Awali, Msigwa ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii alitoa madai hayo Mei 14, mwaka huu wakati wa uwasilishwaji wa bajeti ya wizara hiyo mjini Dodoma.Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri Nyalandu pia alitangaza kuifuta Idara ya Wanyamapori na kuunda Mamlaka ya Wanyamapori ili kuimarisha ufanisi katika sekta hiyo."Kufuatia tuhuma zilizowasilishwa bungeni kwa njia ya ushahidi wa DVD na Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Peter Msigwa Mei 14, 2014… Kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni ya 17(1) na 8(2), Nafuta umiliki wa vitalu vyote vilivyo chini ya Kampuni ya Green Miles Safaris Ltd," alisema Waziri Nyalandu. Alivitaja vitalu hivyo kuwa ni Lake Natron GC East, Gonabis/ Kidunda- WMA na MKI- Selous.


    "Hatua hii pia inafuta vibali vyote vya uwindaji vilivyotolewa katika msimu huu wa uwindaji. Hii iwe onyo kwa kampuni za uwindaji wa kitalii nchini kwa ukiukaji wa sheria, kanuni na taratibu za uwindaji," alisema Nyalandu.

    Aliongeza,  baada ya kupata tuhuma hizo aliiagiza Idara ya Wanyamapori kufuatilia na kumhoji Mkurugenzi wa Kampuni ya GreenMiles Safaris Ltd, ndipo walipobaini makosa ya kampuni hiyo.

    Aliyataja makosa hayo yaliyokiuka Sheria ya Wanyamapori namba 5 ya 2009 kuwa ni pamoja na wageni wa kampuni kuwinda wanyama wasioruhusiwa wakiwemo nyani na ndege kinyume na kifungu cha 19 (1 na 2)  na kuchezea watoto wa pundamilia na ngiri kinyume na kifungu cha 19 (1).

    "Kufukuza wanyamapori kwa magari na kisha  kuwapiga risasi wakiwa ndani ya magari kinyume cha sheria,"  alisema Nyalandu.
    Akizungumzia hatua hiyo, Msigwa alisema ni ushahidi kuwa kambi ya upinzani bungeni inasema ukweli


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.