July 18, 2014

  • DEL BOSQUE ATHIBITISHA KUENDELEA KUIFUNDISHA HISPANIA LICHA YA KUVURUNDA KOMBE LA DUNIA 2014


    DEL BOSQUE ATHIBITISHA KUENDELEA KUIFUNDISHA HISPANIA LICHA YA KUVURUNDA KOMBE LA DUNIA 2014
    Del Bosque confirms he will                  remain as Spain boss
    VICENTE del Bosque amevunja ukimya kuhusu hatima yake kwa kuweka wazi kuwa bado ana nia ya kuendelea kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Hispania mpaka fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2016.
    Hispania iliboronga na kushindwa kutetea ubingwa wa dunia waliotwaa mwaka 2010 nchini Afrika kusini ambapo katika fainali za mwaka huu nchini Brazil walitolewa hatua ya makundi wakifungwa mabao 5-1 na Uholanzi na 2-0 dhidi ya Chile.
    Licha ya timu yake kufanya vibaya mwezi uliopita, Del Bosque amesisitiza kuwa hana nia ya kujiuzulu na anafurahi kuendelea kuisaidia Hispania.
    "Tunaweza kufanya mengi mazuri na kurudi kwenye mstari," kocha huyo mwenye miaka 63 aliwaambia waandishi wa habari nchini Hispania.
    "Tutajitahidi kutetea ubingwa wetu wa mataifa ya ulaya. Mabadiliko ya mfumo sio lazima, badala yake tunatakiwa kuendelea na mfumo wetu kwa kuongeza mabadiliko kidogo".
    Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid aliyemrithi Luis Araggones baada ya ubingwa wa fainali za Euro 2008, aliiongoza Hispania kwa mafanikio katika fainali za mataifa ya ulaya za mwaka 2012 na za kombe la dunia mwaka 2010.
    "Nimekuwa katika mawasiliano na shirikisho wakati huu mgumu na wamefikiria kuwa mafanikio ya miaka sita iliyopita ni muhimu zaidi kuliko matokea mabaya katika mechi mbili," alisema Del Bosque ambaye mkataba wake unaisha mwaka 2016.
    "Shirikisho lina mtazamo chanya na wanathamini kazi yangu. Tunajiona imara na tutaendelea kufanya kazi yetu kama awali".

    "Tunajipanga vizuri  na tutafanya baadhi ya mabadiliko katika timu yetu kama tulivyofanya siku za nyuma".


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.