Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

Showing posts with label Michezo. Show all posts
Showing posts with label Michezo. Show all posts

July 18, 2014

  • TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO





    TAAFRIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO


  • NAHODHA WA UJERUMANI ASTAAFU KUCHEZEA TAIFA



    NAHODHA WA UJERUMANI ASTAAFU KUCHEZEA TAIFA

    Nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani Philipp Lahm amestaafu kucheza soka la kimataifa, baada ya kukiongoza kikosi chake na kushinda Kombe la Dunia nchini Brazil.Beki huyo wa Bayern Munich, ambaye pia anaweza kucheza kama kiungo, ameichezea Ujerumani mara 113.Lahm, 30, ataendelea kucheza Bayern Munich, ambapo amesaini mkataba hadi mwaka 


    2018. Habari za kustaafu kwake kuichezea timu ya taifa zimethibitishwa na chama cha soka cha Ujerumani DFB.

    Lahm alianza kuichezea Ujerumani Februari 2004 walipoichapa Croatia 2-1, na amestaafu kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Argentina katika fainali ya Kombe la Dunia.


  • DEL BOSQUE ATHIBITISHA KUENDELEA KUIFUNDISHA HISPANIA LICHA YA KUVURUNDA KOMBE LA DUNIA 2014


    DEL BOSQUE ATHIBITISHA KUENDELEA KUIFUNDISHA HISPANIA LICHA YA KUVURUNDA KOMBE LA DUNIA 2014
    Del Bosque confirms he will                  remain as Spain boss
    VICENTE del Bosque amevunja ukimya kuhusu hatima yake kwa kuweka wazi kuwa bado ana nia ya kuendelea kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Hispania mpaka fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2016.
    Hispania iliboronga na kushindwa kutetea ubingwa wa dunia waliotwaa mwaka 2010 nchini Afrika kusini ambapo katika fainali za mwaka huu nchini Brazil walitolewa hatua ya makundi wakifungwa mabao 5-1 na Uholanzi na 2-0 dhidi ya Chile.
    Licha ya timu yake kufanya vibaya mwezi uliopita, Del Bosque amesisitiza kuwa hana nia ya kujiuzulu na anafurahi kuendelea kuisaidia Hispania.
    "Tunaweza kufanya mengi mazuri na kurudi kwenye mstari," kocha huyo mwenye miaka 63 aliwaambia waandishi wa habari nchini Hispania.
    "Tutajitahidi kutetea ubingwa wetu wa mataifa ya ulaya. Mabadiliko ya mfumo sio lazima, badala yake tunatakiwa kuendelea na mfumo wetu kwa kuongeza mabadiliko kidogo".
    Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid aliyemrithi Luis Araggones baada ya ubingwa wa fainali za Euro 2008, aliiongoza Hispania kwa mafanikio katika fainali za mataifa ya ulaya za mwaka 2012 na za kombe la dunia mwaka 2010.
    "Nimekuwa katika mawasiliano na shirikisho wakati huu mgumu na wamefikiria kuwa mafanikio ya miaka sita iliyopita ni muhimu zaidi kuliko matokea mabaya katika mechi mbili," alisema Del Bosque ambaye mkataba wake unaisha mwaka 2016.
    "Shirikisho lina mtazamo chanya na wanathamini kazi yangu. Tunajiona imara na tutaendelea kufanya kazi yetu kama awali".

    "Tunajipanga vizuri  na tutafanya baadhi ya mabadiliko katika timu yetu kama tulivyofanya siku za nyuma".


  • July 13, 2014

  • KOCHA WA UJERUMANI AONYA, ASISITIZA REKODI MPYA KOMBE LA DUNIA LEO



    KOCHA WA UJERUMANI AONYA, ASISITIZA REKODI MPYA KOMBE LA DUNIA LEO
    Kocha Joachim Low, amesisitiza Ujerumani haimhofii Lionel Messi hata kidogo katika mechi ya fainali dhidi ya Argentina, leo.
    Lakini akasisitiza kuwa, Ujerumani itaweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya Ulaya kuchukua Kombe la Dunia katika ardhi ya Bara la Amerika Kusini.



  • July 12, 2014

  • FIFA YATANGAZA WATAKAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA



    FIFA YATANGAZA WATAKAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA
    Fifa imetangaza orodha ya majina 10 watakaowania tuzo ya mchezaji bora katika michuano ya Kombe la Dunia - 2014 Golden Ball.
    Wachezaji watatu wametoka Argentina, Angel Di Maria, Javier Mascherano na Lionel Messi. Mahasimu wao wa siku ya Jumapili Ujerumani, imetoa wachezaji wanne, Mats Hummels, Toni Kroos, Phillip Lahm na Thomas Muller.
    Wengine ni James Rodriguez kutoka Colombia, Neymar wa Brazil na Arjen Robben wa Uholanzi.
    Fifa pia imetangaza majina ya watakaowania tuzo ya golikipa bora wa michuano hiyo. Keylor Navas wa Costa Rica, Manuel Neuer wa Ujerumani na Sergio Romero wa Argentina watawania tuzo hiyo.
    Wakati huohuo Memphis Depay wa Uholanzi, Paul Pogba na Raphael Varane wa Ufaransa wamechaguliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora chipukizi katika Kombe la Dunia.
    Washindi watatangazwa baada ya mchezo wa fainali siku ya Jumapili





  • July 09, 2014

  • In pictures: Brazil in shock over Germany defeat


    Brazil's 7-1 thrashing by Germany in the World Cup semi-final on Tuesday has sent shockwaves through the country, leaving fans of the host nation crushed.
    Brazilian fans react at the end of the semi-final football match between Brazil and Germany at on 8 July 2014.
    Brazil suffered their worst-ever World Cup defeat and first home loss in 12 years.
     Brazil fans watch the first half on Copacabana Beach during the 2014 FIFA World Cup semi-final match between Brazil and Germany on 8 July 2014
    Brazilians gathered in their thousands at Copacabana Beach in eager anticipation of the match...but the carnival atmosphere was not to last.
    Brazil fans watch the first half on Copacabana Beach during the 2014 FIFA World Cup semi-final match between Brazil and Germany on 8 July 2014 in Rio de Janeiro, Brazil.
    Fans were left stunned after Germany went 5-0 up in the first 29 minutes of play.
    Brazilian supporters react after defeat in the semi-final football match between Brazil and Germany on 8 July 2014
    Many had already left the Belo Horizonte stadium by the start of the second half.
    A Brazilian fan reacts while watching the 2014 FIFA World Cup semi-final match between Brazil and Germany on a public screen on the streets of Rio de Janeiro, Brazil on 8 July 2014
    For football fans and pundits in Brazil - a country built on sporting pride - the defeat came as a bitter shock.
    Crying Brazil fans while watching the first half on Copacabana Beach during the 2014 FIFA World Cup semi-final match between Brazil and Germany on 8 July 2014
    Smiles turned to tears on Copacabana Beach as Germany scored again and again.
    An emotional Brazil fan reacts after being defeated by Germany 7-1 on 8 July 2014
    After Tuesday's defeat, some Brazil fans have questioned whether hosting the tournament had been worth the cost.
    Brazilian supporters react after defeat in the semi-final football match between Brazil and Germany on 8 July 2014
    Dejected fans hung around the streets of Belo Horizonte in the hours after the game.
    Front pages of German newspapers showing photos from the FIFA World Cup 2014 semi-final football match between Germany and Brazil on July 9, 2014 in Berlin.
    German newspapers hailed the historic result. The front page of Bild, the biggest-selling paper in Germany, reads: "7-1. No words for it!"
    Football fans celebrate with a mock World Cup trophy in Duesseldorf, western Germany,on 8 July 2014
    A different atmosphere in Duesseldorf, Germany, where fans celebrated their team's victory into the early hours.
  • MANENO ALIYOTAMKA LUIZ FELIPE SCOLARI BAADA YA KUFUNGWA 7-1 NA UJERUMANI



    MANENO ALIYOTAMKA LUIZ FELIPE SCOLARI BAADA YA KUFUNGWA 7-1 NA UJERUMANI
    Luiz Felipe Scolari, kocha wa Brazil
    "Ni wakati mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kazi yangu ya ukocha na siku mbaya zaidi katika maisha yangu ya soka. Lakini maisha yanaendelea. Nani anawajibika kwa matokeo haya? Ni mimi, ni mimi. Lawama za matokeo haya mabaya zinaweza kutuhusisha wote, lakini mtu aliyeamua timu ya kucheza na mbinu nilikuwa mimi.
    Lilikuwa chaguo langu. Tulijitahidi kufanya kila tuwezalo, tulicheza kwa kiwango chetu cha mwisho-lakini tumeishia dhidi ya timu kubwa ya Ujerumani. Hatukukata tamaa na kurudi nyuma. Tuliparaganyika na kupaniki baada ya kufungwa bao la kwanza na kila kitu kiliharibikia hapo. Hata Ujerumani hawawezi kuelezea ilitokeaje-lakini ni kwasababu ya ujuzi wao na unatakiwa kuheshimu hilo.

    Tunatakiwa kujiunza jinsi ya kukabiliana nalo. Ujumbe wangu kwa watu wa Brazil ni huu. Tafadhali watusamehe kwa kiwango hiki. Ninaomba radhi kwasababu hatujaweza kufika fainali-na tutajitahidi kushinda mechi ya nafasi ya tatu. Bado tuna sababu ya kucheza."


  • UJERUMANI YAICHAPA BRAZIL 7-1 NYUMBANI KWAO NA KUTINGA FAINALI



    UJERUMANI YAICHAPA BRAZIL 7-1 NYUMBANI KWAO NA KUTINGA FAINALI
    BrazilUJERUMANI imetinga Fainali ya Kombe la Dunia, baada ya kuwafumua wenyeji, Brazil mabao 7-1 katika mcheo wa Nusu Fainali uliofanyika Uwanja wa Mineirao mjini Belo Horizonte, Brazil.No way back: Oscar and Fred stand            ready at the centre circle with little hope of getting back            into the game
    Ujerumani inaingia Fainali kwa mara ya kwanza baada ya miaka 12- mara ya mwisho ilifungwa na Brazil katika fainali zilizoandaliwa kwa pamoja na Korea Kusini na Japan na sasa watamsubiri mshindi wa kesho kati ya Argentina na Uholanzi.



    Hadi mapumziko, tayari Ujerumani walikuwa mbele kwa mabao 5-0 yaliyofungwa na Toni Kroos mawili, Miroslav Klose, Thomas Muller na Sami Khedira. Brazil ilionekana wazi kuathiriwa na pengo la kuwakosa wachezaji wake tegemeo, beki na Nahodha Thiago Silva anayetumikia adhabu ya kadi za njano na mshambuliaji Neymar ambaye ni majeruhi, ambao nafasi zao zilizibwa na Bernard na DanteHistoric: The strike that made              hm the record holder.
    Ujerumani ilipata bao lake la kwanza dakika ya 11, mfungaji Thomas Muller baada ya makosa ya safu ya ulinzi ya Brazil.
    Miroslav Klose akafunga la pili dakika 23 baada ya kuukuta mpira uliopanguliwa na kipa Julio Cesar kufuatia shuti lake mwenyewe na kuandika bao lake la 16 kwenye Fainali za Kombe la Dunia akiweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye fainali hizo, akimpiku Mbrazil, Ronaldo Lima.Disbelief: Fernandinho,                  Maicon and David Luiz look bemused following Germany's                  fifth goal of the evening
    Toni Kroos akaifungia Ujerumani bao la tatu na la nne dakika za 24 na 26, kabla ya Sami Khedira kufunga la tano dakika ya 29. 
    Kipindi cha pili, kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari alianza na mabadiliko, akiwatoa Fernandinho na Hulk na kuwaingiza Paulinho na Ramires, wakati mwenzake wa Ujerumani, Joachim Loew alimpumzisha Hummels na kumuingiza Mertesacker.Too easy! Eight Brazilians                  stand in the box as Muller finds space to guide the ball                  goalwards
    Mabadiliko hayo kidogo yaliiongezea uhai Brazil na kupeleka mashambulizi langoni mwa Ujerumani, lakini wakaishia tu kukosa mabao ya wazi.
    Ujerumani ikafunguka tena na kwenda kufunga mabao mawili zaidi, yote Andre Schurrle aliyeingia dakika ya 58 kuchukua nafasi ya Klose akimtungua kipa Julio Cesar dakika ya 69 na 79. Running riot: Germany scored                  four goals in six first-half minutes during Tuesday's                  semi-final against Brazil
    Brazil ilianya tena mabadiliko, Fred akimpoisha Willian dakika ya 69, wakati Ujerumani nayo ilimpumzisha Khedira nafasi yake ikachukuliwa na 
    Draxler dakika ya 76.
    Mesut Ozil alipata nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 89, lakini akapiga nje na Brazil wakafanya shambulizi na kushitukiza na kujipatia bao la kufutia machozi lililofungwa na Oscar dakika ya 90.
    Wachezaji na mashabiki wa Brazil waliangua vilio baada ya mchezo huo, huku Wajerumani wakiangusha pati la maana uwanjani


  • July 05, 2014

  • STARS YA MART NOOIJ YATUA NCHINI KUTOKEA GABORONE




    STARS YA MART NOOIJ YATUA NCHINI KUTOKEA GABORONE

     Na Baraka Mpenja, Dar es salaam


    TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa stars  inatarajia kutua nchini kesho (julai 6) mwaka huu ikitokea nchini Botswana ili kuendelea na programu nyingine ya mazoezi.
     Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iliweka kambi ya wiki mbili, mjini Gaborone kwa ajili ya kujiwinda na mechi dhidi ya Msumbaji kuwania kupangwa hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika, AFCON mwakani nchini Morocco.
     Mechi hiyo muhimu kwa kocha wa Stars, Mholanzi, Mart Nooij itapigwa katika dimba la Taifa, julai 20 mwaka huu na wiki mbili baadaye mchezo wa marudiano utapigwa mjini Maputo nchini Msumbiji.
     Ikiwa ni sehemu ya kujipima ubavu, Stars ilicheza mechi ya kirafiki siku za karibuni na wenyeji wao Botswana na kuchapwa mabao 4-2.
     Mabao ya Taifa stars yalifungwa na Khamis Mcha `Vialli` na John Raphael Bocco `Adebayor`.
     Hata hivyo, matokeo hayo yalimfanya kocha Nooij ajue makosa ya kikosi chake na kuyafanyia kazi kabla ya kukabiliana na Black Mambas.
     Katika kambi ya Gaborone, Taifa stars ilimkosa winga wake machachari, Mrisho Khalfan Ngassa `Anko` aliyesafiri kwenda kufanya majaribio katika klabu ya Free State Stars inayoyoshiriki ligi ya Afrika kusini.
     Kocha Nooij alimuita Ngassa ili acheze mechi ya kirafiki na Botswana, lakini ilielezwa kuwa nyota huyo alikaidi na kwenda kufanya majaribio katika klabu hiyo inayonolewa na Mbelgiji Tom Saintfiet.
     Taarifa za uhakika zinasema kuwa Nooij amemuengua Ngassa kuelekea mchezo dhidi ya Msumbiji na tayari nyota huyo yupo nchini baada ya kumaliza majaribio yake Afrika kusini ambapo alifuzu, lakini uhamisho wake bado ni tatizo.
     Msumbiji wana historia ya kuiharibia Taifa stars katika mechi muhimu, hivyo ni muhimu kwa kocha kukisuka kikosi chake pamoja na watanzania kuisapoti timu yao.
     Stars ilifanikiwa kufuzu raundi ya pili ya hatua ya awali baada ya kuifunga Zimbabwe bao 1-0 katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam na kulazimisha sare ya 2-2 mjini Harare nchini Msumbuji.
     Msumbuji wao walishinda mabao 5-0 mjini Maputo na kutoka suluhu pacha ya bila kufungana dhidi ya Sudani Kusini ugenini.
     Mshindi wa jumla katika mechi hiyo atafuzu hatua ya makundi  ya kusaka tiketi ya kucheza AFCON mwakani nchini Morocco.


  • GIGGS AWA DAKTARI WA SAYANSI...HESHIMA YAKO MKONGWE!



    GIGGS AWA DAKTARI WA SAYANSI...HESHIMA YAKO MKONGWE!
    Honour: The Manchester                        United legend poses with his degree at Victoria                        Hall in Bolton
    Heshima: Gwiji wa Manchester United akipozi katika picha baada ya kupata digrii yake kwenye ukumbi wa  Victoria Hall mjini Bolton.

    GWIJI wa Manchester United, amezawadia shahada ya heshima ya Udaktari na chuo kikuu cha Bolton kutokana na mchango wake mkubwa aliotoa katika mchezo soka.
    Giggs aliyestaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu uliopita amepokea udaktari wa sayansi kwa mchango wake mkubwa katika michezo kwenye mahafali ya chuo iliyofanyika ukumbi wa Victoria Hall mjini Bolton jana ijumaa mchana. 
    Giggs anaongeza shahada hiyo katika shahada yake ya kwanza ya OBE aliyopata kutoka kwa Malkia mwaka 2007, shahada ya pili (MA) alipewa mwaka uliofuata na chuo cha Salford.
    Recognised: Giggs                        addressed graduate students at the university and                        congratulated them on their degrees
     Giggs aliwapongeza wanafunzi wa chuo kwa kupata digrii zao.


  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.