Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

November 30, 2014

  • HABARI MBAYA KWA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED LICHA YA KUSHINDA KWA KISHINDO JANA!



    HABARI MBAYA KWA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED LICHA YA KUSHINDA KWA KISHINDO JANA!
    Unapozungumzia suala la majeraha ya wachezaji bila shaka mashabiki wa Manchester United wanapata homa ya ghafla .
    Hii ni kwa sababu timu hii imekuwa na orodha isiyoisha ya wachezaji wenye majeraha .
    Mbaya zaidi ni kwamba kila orodha hii inapoonyesha dalila za kungua mchezaji mwingine anaemia na inazidi kuwa ndefu .
    Orodha hii iliongezeka kwenye mchezo dhidi ya Hull City wakati ambapo kiungo mshambuliaji Angel Di Maria alipoumia misuli ya nyonga kwenye dakika ya 14 ya mchezo na kulazimika kutoka.
    Bado haijafahamika Di Maria atakaa nje ya uwanja kwa muda gani lakini kwa kawaida jeraha kama hili huhitaji kati ya siku 7 mpaka 10 ili kupona na wakati mwingine kuendana na ukubwa wake linaweza kuhitaji muda mrefu zaidi .

    Kwa jumla Jeraha la Di Maria ni jeraha la 41 kwa mchezaji wa Manchester United kwa msimu huu tangu kuanza kazi kwa kocha Mholanzi Louis Van Gaal .
    Idadi hii ndio idadi kubwa ya majeraha kwa wachezaji kwa timu yoyote ya ligi kuu ya England msimu huu hali inayowafanya United waamini kuwa huenda timu yao ina mkosi wa aina Fulani.


  • November 29, 2014

  • Habari kwa Kina Kuhusu Vurugu Zilizoibuka Jana Bungeni na kupelekea Bunge Kuvunjika




    Habari kwa Kina Kuhusu Vurugu Zilizoibuka Jana Bungeni na kupelekea Bunge Kuvunjika
    Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana usiku kilivunjika baada ya vurugu
    kutawala ukumbini humo.

    Vurugu hizo zilianza saa 04:42 usiku hadi saa 04:49 usiku wakati Spika Anne Makinda alipolazimika kuahirisha Bunge hadi leo saa tatu asubuhi.

    Chanzo cha vurugu ni kutokana na ugumu wa kutokukubaliana na azimio la tisa, lililolenga kumwajibisha moja kwa moja Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

    Azimio la PAC lilitaka Waziri Muhongo aadhibiwe kwa kufukuzwa kazi kutokana na tuhuma zilizokuwa zinazomkabili ikiwamo kulidanganya Bunge.

    Hata hivyo, baadhi ya wabunge wengi wakiwa wa CCM walitaka waziri huyo asiadhibiwe na Bunge bali achukuliwe hatua na mamlaka iliyomteua.

    Wakati ubishani huo ukiendelea, ikiwa imefika saa 4.42 usiku Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisimama na Spika
    Makinda alimruhusu kuzungumza.
    "Bunge kufikisha saa tano kasoro ni historia, lakini leo (jana) kuna uzito wa kiti na uzito wa wabunge kwa mamlaka ambayo yako ndani yao.

    Panaonekana kuna maamuzi mengine ya kulinda watu. Kwa nini leo tuna kigugumizi. Tunapata wakati mgumu kuendelea kushiriki kikao cha
    kulindana. Kwanini mnalinda wezi," ilikuwa ni kauli ya Mbowe.

    Mara baada ya kutoa kauli hiyo, wabunge wote wa upinzani walisimama na kuanza kupiga kelele kwamba wezi waondoke…tunataka fedha zirudi…
    tunataka fedha zirudi…vijana msilale…vijana msilale.

    Wakati wabunge hao wakiendelea kuimba, wabunge wa CCM wao walikuwa wakizunguka zunguka huku wengine wakitoka ndani ya Ukumbi
    wa Bunge.

    Hata hivyo, wabunge wa upinzani waliendelea kusimama, kuimba na kupiga makofi, huku wabunge wa CCM wakimpongeza Naibu Waziri wa
    Nishati na Madini, Stephen Masele kwa kuruka kihunzi alichokuwa amewekewa na kamati ya PAC.

    Kutokana na hali hiyo wabunge wengine
    walisimama vikundi vikundi, huku Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, na Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka walikuwa wakiwasihi wabunge wa upinzani wasiondoke bungeni.

    Spika Makinda alisimama na kusema,
    "Mheshimiwa Mbowe kuondoka mapema ni mambo ya kitoto, semeni mnataka Bunge lifanye nini."
    Hata hivyo, kauli hiyo ya Makinda haikuwafanya wabunge hao kuacha walichokuwa wakikifanya, bali walibaki ndani ya ukumbi wakiwa wamesimama hadi ilipofika Saa 04:49 usiku
    wakati Spika Makinda aliposimama na kusema, "Waheshimiwa wabunge naahirisha kikao cha bunge hadi pale tutakaposhauriana."

    Kuvunjika kwa kikao hicho kinaweka njia panda hatima ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ambao Bunge lilikuwa halijafikia kufanya maazimio
    ya hatima yao.

    Hoja ya baadhi ya wabunge wa CCM walikuwa wakitaka mapendekezo yaliyotolewa na Mbunge wa Bariadi (CCM), Andrew Chenge kuhusu hatima
    ya Pinda na Werema yapite.

    Chenge alipendekeza kuwa, "Kuhusu suala la Waziri wa Nishati na Madini lifikishwe kwa mamlaka ya uteuzi kwa hatua zaidi (wakimaanisha
    Rais)."

    Pendekezo ambalo lilipingwa na upinzani kwa kile walichoeleza kuwa Bunge linaweza kuwawajibisha
    kama ambavyo limewahi fanya hivyo. 

    Spika Makinda akijibu hoja ya Bunge kuwawajibisha alisema; "Mnajua waheshimiwa wabunge huko
    nyuma mawaziri walikubali wenyewe, lakini hawa wamekataa ndiyo maana tunaona haya yanatokea.

    Awali, Bunge hilo limemwachia Rais Jakaya Kikwete kufanya uamuzi wa kuwawajibisha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi baada ya kuadhimia kuwa suala lake
    lifikishwe kwa Rais kwa hatua zaidi.

    Mjadala wa kuchukuliwa hatua kwa Maswi uliwagawa wabunge na kuwafanya kujadili kwa zaidi ya dakika 30, kufikia uamuzi huo ambao hata
    hivyo ulipingwa na baadhi ya wabunge.

    Hata hivyo, Bunge limemwokoa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele kwa kuona kuwa kauli yake aliyoitoa haikuwa na madhara yoyote hivyo hahusiki kwa vyovyote vile kwenye
    sakata hilo.

    Hatua ya kuwashughulikia viongozi hao na wengine kuokolewa ilifikiwa baada ya mvutano mkali wa pande mbili ndani ya Bunge katika kukubaliana na mapendekezo ya kamati ya PAC.

    Baada ya muda wabunge na mawaziri walioanza kuingia kwenye magari yao na kuondoka bila kujua nini kitaendelea leo.
    Hata hivyo, Spika Makinda ambaye alikuwa amezungukwa na askari wa usalama akisindikizwa ofisini kwake alisikika akiwaambia baadhi ya
    wabunge kuwa kikao kitaendelea leo saa tatu.

    Taarifa kutoka kwa baadhi ya maofisa wa Bunge zimeeleza kuwa kikao cha Bunge kitaendelea leo.

    Awali, Bunge lilikubali mapendekezo ya PAC kwamba viongozi wa umma waliofaidika na fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow akiwamo
    Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wachukuliwe hatua za kinidhamu ya kuvuliwa nyadhifa zao.

    Wengine ni Naibu wake Stephen Masele na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakimu Maswi nao wawajibishwe.

    PAC ilieleza kuwa wakati Jaji Werema
    ameonekana kutoishauri vizuri Serikali na pia kuagiza fedha hizo zitolewe kwenye akaunti hiyo, mwenzake Profesa Muhongo hakuchukua hatua wakati akijua kuwapo kwa sakata hilo, huku Naibu wake, Stephen Masele akitiwa hatiani kwa kulidanganya Bunge.

    Vilevile, Bunge limependekeza kuwa viongozi wa umma waliopewa fedha zitokanazo na Akaunti ya Tegeta Escrow na hawakutangaza kupokea zawadi
    kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma nao wachukuliwe hatua akiwamo Waziri wa
    Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

    Viongozi wengine wanaotajwa kupewa fedha hizo ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na baadhi
    ya majaji na watumishi wa Serikali.



  • November 28, 2014

  • MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 28.11.2014


    MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 28.11.2014



















    .




    .




    .




    .




    .




    .






  • November 27, 2014

  • AJALI MBAYA ILIYOTOKEA LEO ASUBUHI ENEO LA KONA KALI YA MKANYAGENI TANGA

    INASEMEKANA WATU WAMEJERUHIWA  KWENYE AJALI ILIYOTOKEA ENEO LA KONA KALI YA MKANYAGENI IKIHUSISHA GARI YA ABIRIA AINA YA COSTA ILIYOGONGANA USO KWA USO NA SCANIA SEMITRELA
    KWA MUJIBU WA MASHUHUDA WA TUKIO HILO WANASEMA KATIKA AJALI HIYO COSTA IMEKATIKA KATI KWA KATI NA WATU WALIOJERUHIWA WAPO KWENYE COSTA HIYO
    COSTA INAYOFANYA SAFARI ZAKE TOKA TANGA MJINI KUELEKEA LUSHOTO NA SCANIA ILIYOKUWA INATOKA MKANYAGENI,
    HABARI ZINASEMA IDADI HIYO YA MAITI INAWEZA ONGEZEKA MUDA WOWOTE KWANI HALI ZA MAJERUHI NI MBAYA MNO AMBAPO CHANZO CHA AJALI KIMESEMWA KUWA NI MWENDO KASI
  • November 26, 2014

  • WARUNDI KORTINI KWA MENO 18 YA TEMBO


    WARUNDI KORTINI KWA MENO 18 YA TEMBO

    RAIA watatu wa Burundi akiwemo mwanamke wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu mkazi wa Wilaya ya Morogoro, wakikabiliwa na mashitaka matatu ya kuhujumu uchumi baada ya kukamatwa na meno ya tembo 18, na mikia mitano ya twiga, vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni 357.



    Watuhumiwa hao walipandishwa mahakamani jana na kusomewa mashitaka matatu na Wakili wa Serikali, Edgar Bantulaki, mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Alisile Mwankejela.
    Wakili huyo aliwataja watuhumiwa walioshitakiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukutwa na nyara ni John Lazaro Yantoro (55), Ibrahim Nena Yantoro (28) na Scolastica Aron (27), wote walikuwa wakiishi katika Kambi ya Wakimbizi ya Katumba Mpanda mkoani Katavi.
    Wakili huyo alidai watuhumiwa hao walikamatwa Novemba 13, mwaka huu eneo la Bwawani mkoani Morogoro wakiwa na meno 18 ya tembo, yenye thamani ya dola za Marekani 135,000, sawa na Sh milioni 229.5.
    Pia, walikamatwa na nyara nyingine za mikia mitano ya twiga, ikiwa na thamani ya dola 75,000 sawa na Sh milioni 127.5. Alidai watuhumiwa hao walikuwa wakifanya biashara ya kununua na kuuza nyara hizo, zitokanazo na wanyama, mali ya Serikali.
    Alidai kutokana na kesi hiyo kuwa ni ya uhujumu uchumi, mahakama hiyo haina uwezo wa kuiendesha, isipokuwa kuwasomea mashitaka yao na wao kutotakiwa kujibu lolote. Upelelezi wa kesi hiyo unaendelea.
    Kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilishwa, Wakili wa Serikali aliiomba Mahakama kuipangia tarehe nyingine, ambapo hakimu wa mahakama hiyo aliiahirisha hadi Desemba 10 mwaka huu, itakapofikishwa tena mahakamani hapo kwa kutajwa.
    Aliamuru watuhumiwa hao kurudishwa rumande.

    HABARI LEO.

  • VYUO VYA TANZANIA VYAFELI KATIKA MJADALA



    VYUO VYA TANZANIA VYAFELI KATIKA MJADALA
    Chuo kikuu cha Ruaha nchini Tanzania ni miongoni mwa vyuo vitatu vikuu vilivyofeli katika mjadala wa kimataifa uliofanyika katika mahakama maalum ya ICTR mjini Arusha.

    Vyuo vikuu vitatu vya Tanzania ambavyo vilishiriki katika mashindano ya mjadala wa Afrika kuhusu Sheria za kimataifa za haki za kibinaadamu yalioandaliwa na kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu ICRC vimeshindwa kufika katika raundi ya mwisho.
    Badala yake vyuo hivyo viliondolewa katika raundi za mapema ambapo mataifa manane ya Afrika yalishiriki.
    ICRC imekuwa ikiandaa hafla kama hizo kwa kipindi cha miaka 14 sasa mjini Arusha.
    Kulingana na gazeti la the Citizen nchini Tanzania, vyuo vilivyoiwakilisha Tanzania ni chuo cha kanisa katoliki cha Ruaha kutoka Iringa,Chuo cha Iringa na Chuo kikuu cha Zanzibar.
    Katika raundi ya mwisho ya mashindano hayo yaliofanyika mwishoni mwa wiki katika mahakama maalum ya kimataifa inayochunguza mauaji ya kimbari nchini Rwanda ICTR mjini Arusha,chuo cha Strathmore University kutoka Kenya kiliibuka mshindi na kufuatiwa na chuo cha Christian University kutoka Uganda huku chuo cha Kunduyi pasi kutoka Zimbabwe kikiibuka mshindi wa spika bora.
    Raundi ya mwisho ya mjadala huo ilisimamiwa na jaji wa mahakama hiyo Vagn Joensen,jaji wa mahakama kuu ya Tanzania Stella Mugasha,jaji wa mahakama ya haki katika Afrika mashariki Fanstin Ntezilyayo,John Joseph Wamwara na Mutsa mangezi kutoka ICRC.
    Judge Joensen, ambaye alitoa zawadi kwa washindi aliyapongeza mashindano hayo kama kifaa cha kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanaofanya sheria na kwamba itasaidia kuimarisha maono yao katika siku za usoni.


  • MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 26.11.2O14



    MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 26.11.2O14
    .

    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .



  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.