Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

August 29, 2015

  • ANGALIA HAPA MAJINA YA WAHITIMU WA KIDATO CHA 4 NA 6 2014 NA JKT 2015 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI



    ANGALIA HAPA MAJINA YA WAHITIMU WA KIDATO CHA 4 NA 6 2014 NA JKT 2015 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI

    Tangazo la Wito chuo cha polisi moshi kwa wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014, kidato cha nne mwaka 2014 na JKT mwaka 2015 waliochaguliwa kujiunga na jeshi la Polisi.


    AU



  • August 28, 2015

  • TCRA YAIPA ONYO KALI TBC


    TCRA YAIPA ONYO KALI TBC

    Hukumu hiyo ilitolewa leo jijini Dar es Salaam na kamati ya maudhui ya utangazaji, katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Walter Bugoya wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapoBugoya amesema kamati hiyo imebaini TBC one imekiuka sheria ya utangazaji ya mwaka 2005 pamoja na sheria ya uchaguzi ya mwaka 2015 baada ya kufanya upendeleo wa vyama katika taarifa zake kwenye kipindi.
    Amedai katika kipindi cha Jambo Tanzania kilichorushwa tarehe 15 mwezi huu majira ya saa 12 asubuhi hadi saa tatu,katika kipingele cha uchambuzi wa magazeti ambapo mtangazaji wa kipindi hicho alikuwa anayasoma magazeti huku akiruka kusoma habari kuu husika.
    Amesema Mtangazaji huyo alipokuwa anachambua gazeti la Majira na Nipashe alidanya umma jambo ambalo amedai ni kosa.
    Bugoya ametaja makosa hayo ni wakati mtangazaji huyo alipokuwa anasoma Gazati la Majira ukrsa wake wa mbele alisema habari kubwa ni "CCM yazidi wambua wanaomfuata lowassa" wakati habari kubwa ilikuwa inasomeka hapo ni ile inayosema "Mbeya kwafurika"huku picha ya gazeti hilo likionyesha picha ya umati watu pamoja na mgombea wa Urais wa chadema Edward lowassa akihutubia.
    Amesema mtangazaji huyo pia alifanya kosa jengine kama hilo pia wakati akisoma Gazeti la Nipashe ambapo alisema Habari iliyopewa uzito wa kipekee ni "Mbalawa atoa sheria ya mitandao" ambapo habari iliyopewa uzito ilikuwa ni ile ilikuwa "Mafuriko Mbeya" na sio aliyokuwa anaisoma yeye.
    Amesema baada ya Kamati yake kubaini makosa hayo waliwasiliana na mkurugenzi wa TBC one Bwana Mshana ambao mkurugenzi huyo alitoa utetezi wake kwenye kamati hiyo akisema mtangazaji huyo ajafanya kosa kwakuwa alikuwa ajaridhika na taarifa zilizokuwa zimeandikwa kwenye magazeti hayo.
    Sanjari na hayo Mshana alizidi jitetea akidai kuwa hata mtangazaji huyo hata asingesoma habari ile lakini picha iliyokuwa inaonekana kwenye magazeti hayo teyari mtazamaji alikuwa ashajua kwahiyo amedai haikuwa na ulazima wa kusomwa.
    Bugoya amesema baada ya kusikiliza upande wa TBC one ndio wakabaini kituo hicho kilikiukaka sheria ya utangazaji ya Mwaka 2005 ambayo inavitaka vituo vyote vya utangazaji nchini kuripoti taarifa kwa kutokuwa na upendeleo wowote.

    Amesema Kamati imefikia uamuzi wa kuipa onyo kali kwa TBC one na endapo wakiendelea basi Mamlaka hiyo haitasita kuwachukulia hatua kali zaidi.


  • NEC Yakabidhi Polisi Majina ya Watu 52,000 Waliojiandikisha Zaidi ya Mara Moja Katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura



    NEC Yakabidhi Polisi Majina ya Watu 52,000 Waliojiandikisha Zaidi ya Mara Moja Katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
    Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhan (kushoto), akimkabidhi Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Benedict Wakulyamba orodha ya majina 52,078 ya watu waliojiandika katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR zaidi ya mara mbili Dar es Salaam jana, kwa ajili ya uchunguzi na baadae hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika.

    Picha hii ni baadhi ya watu waliojiandikisha zaidi ya mara mbili katika daftari hilo.

    TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imelikabidhi jeshi la polisi orodha ya majina ya watu zaidi ya 52,000 ambao wamebainika kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye daftari la kupigia kura kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR), akiwemo Diwani wa Kata ya Kimara, Pascal Manota (Chadema).

    Idadi hiyo ilibainishwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa NEC, Ramadhan Kailima wakati wa ziara na waandishi wa habari katika bohari ya utayarishaji wa vitambulisho vya kupigia kura kwa mfumo wa BVR


  • UKAWA RUKSA KUZINDUA KAMPENI JANGWANI KESHO



    UKAWA RUKSA KUZINDUA KAMPENI JANGWANI KESHO Mgombea urais kwa tiketi ya          Chadema, Edward

     Hatimaye Chadema imeruhusiwa kutumia Viwanja vya Jangwani kwa ajili ya kuzindua kampeni za mgombea wake wa urais, Edward Lowassa kesho.



    Kampeni za Lowassa, ambaye anaungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya NLD, CUF, NCCR-Mageuzi na Chadema, zilikumbana na kikwazo baada ya juzi, Manispaa ya Ilala kudai kuwa imeshaipa CCM haki ya kutumia viwanja hivyo kwa siku hiyo.
    CCM ilisema ilikodisha viwanja hivyo kwa siku tatu mfululizo kwa ajili ya kuendesha matamasha ya wasanii.
    Lakini jana, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngulumi alisema baada ya majadiliano baina ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na ofisi yake, walikubaliana kuwa mkutano huo ufanyike kesho kama ulivyopangwa, huku CCM ikibaki na siku mbili.
    Mngulumi alisema viongozi wa CCM waliokuwa na haki ya kutumia uwanja huo wamekubali Chadema waendelee na uzinduzi wao kama walivyopanga.
    "Tumekaa pamoja ili kuondoa maneno na tumezungumza na viongozi wa CCM ambao wameafiki kuiachia Chadema siku ya Jumamosi," alisema Mngulumi.
    "Awali, tuliwaomba Chadema wasogeze shughuli yao mbele, lakini wakasema ni lazima waifanye Agosti 29. Hatukuwa na lengo la kuwanyima uwanja ila tatizo lilikuwa kwamba CCM nao walikuwa wameomba."
    Kabla ya Manispaa ya Ilala kutoa tamko hilo, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene alisema chama chake kimesharuhusiwa kutumia viwanja hivyo, maarufu kwa mikutano ya kisiasa na kidini, kama kilivyoomba.
    "Mkutano wetu wa uzinduzi wa kampeni upo palepale. Timu yetu tuliyoituma kuzungumza na vyombo husika leo (jana) asubuhi, imetuthibitishia kuwa kila kitu kinakwenda sawa na tumekubaliwa."
    Wakati Chadema ikiruhusiwa kutumia uwanja huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Kombwey alisema iwapo CCM wasingekubali kuachia eneo hilo, wangetumia Kifungu cha 40 cha Kanuni za Maadili ya Uchaguzi ambacho kinaitaka NEC iitishe kikao cha wadau kujadili mgongano huo.
    Alisema awali, vyama vyote vilikubaliana ratiba za kampeni zao na Chadema walishaonyesha kuwa wangezindua shughuli zao kwenye wilaya zote za mkoani Dar es Salaam, ingawa hawakutaja uwanja.
    Alisema mgongano kama huo ulishatokea Kigoma na baada ya majadiliano, Chadema walikubali kuiachia CCM kuanza kufanya kampeni zake mkoani humo kutokana na NEC kutumia kanuni hiyo.
    Hata hivyo, alisema ili kupata kiwanja cha kuzindulia kampeni, Chadema hawana budi kukubaliana na mamlaka za halmashauri husika kwa kuwa NEC haina uwezo huo ingawa kwa mujibu wa sheria, ni chama hicho pekee ambacho kilitakiwa kifanye kampeni zake Agosti 29 jijini Dar es Salaam.
    Alipoulizwa kuhusu uamuzi huo baadaye jana mchana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema wanaotakiwa kutoa ufafanuzi ni uongozi wa mkoa au wilaya wa chama hicho.
    Katibu Mwenezi wa CCM wa Mkoa, Juma Simba aliwambia waandishi jana mchana kuwa wametumia busara kuwaachia Ukawa ili wazindue kampeni zao.
    "Tumesikia malalamiko mengi ya viongozi wa Ukawa kwamba CCM inawahujumu, hii si kweli, tulichokifanya tulituma maombi na kuulipia uwanja wa Jangwani kwa ajili ya matamasha ya wasanii na kampeni za ubunge na udiwani," alisema.
    Alisema chama hicho kilituma maombi Manispaa ya Ilala tangu Agosti 21 na juzi kililipia Sh150,000 na kupewa kibali namba 00012339.
    Simba alisema chama hicho hakiiogopi Ukawa kwa sababu ndicho kilichoruhusu mfumo wa vyama vingi nchini.
    Msajili wa vyama
    Wakati huohuo, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amekemea tabia ya baadhi ya vyama kuchezeana faulu na kushutumiana kwenye vyombo vya habari katika kipindi hiki cha kampeni.
    Alivitaka vyama vyenye malalamiko dhidi ya vingine kuyapeleka kwenye mamlaka husika na kusubiri uamuzi, badala ya kujibizana kwenye vyombo vya habari.
    "Sizungumzii Chadema na CCM, nazungumzia vyama vyote. Kama vitafuata taratibu za uchaguzi zilizowekwa, shutuma hizi hazitakuwapo," alisema.
    Bavicha yatishia maandamano
    Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi amesema baraza hilo litaongoza maandamano ya vijana nchi nzima iwapo Serikali itaendelea kuminya demokrasia kwa vyama vya upinzani na kuzuia kila jambo analolifanya mgombea urais wa chama hicho, Lowassa.


  • August 27, 2015

  • NEC yashtuka


    NEC yashtuka
    UENDESHAJI wa kampeni za urais zilizoanza hivi karibuni umeishtua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hivyo kutoa angalizo kwa vyama kuhakikishia vinazingatia kanuni na sheria.
    NEC imevitaka vyama vya siasa kuzingatia ratiba ya kampeni kwa kuepuka kufanya mkusanyiko wa aina yoyote usio katika ratiba ya kampeni za urais.
    Katika taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhani Kailima, amesema hivi karibuni kumejitokeza baadhi ya vyama vya siasa vinavyoanza mikusanyiko yenye sura ya kampeni ambayo haipo katika ratiba ya kampeni za urais.
    Kailima katika taarifa yake kwa vyombo vya habari alisema mikusanyiko hiyo yenye sura ya kampeni, inaweza kuingiliana na ratiba za kampeni za vyama vingine katika maeneo husika na kusababisha uvunjifu wa amani.
    Alisema, iwapo chama cha siasa kinataka kufanya mikusanyiko yenye sura ya kampeni za uchaguzi, kinapaswa kuwasilisha mapendekezo yake kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi aitishe kamati ya ratiba ya kampeni ya rais inayojumuisha vyama vyenye wagombea wa kiti cha urais ambavyo kwa mujibu wa kanuni vinaweza kukubali au kukataa mapendekezo hayo.
    Aidha, ilisema katika maadili ya uchaguzi ya mwaka 2015 yaliyokubaliwa na kusainiwa na vyama vyote vya siasa, Julai 27, vyama vyote vya siasa vilikubali kuheshimu na kutekeleza maadili hayo na ukiukwaji wowote wa maadili hayo utashughulikiwa kwa mujibu wa kipengele cha 5.11 cha maadili hayo.
    Alisema chama kitakachokiuka maelezo hayo kitakuwa kimekiuka kipengele cha 2.1(a) cha maadili kinachoeleza wajibu wa vyama vya siasa na wagombea kuheshimu na kutekeleza sheria za uchaguzi.
    Alivitaka vyama vyote vya siasa kuzingatia ratiba ya kampeni ya uchaguzi wa rais kwa kufanya mikutano kwa tarehe, sehemu na mahala kwa mujibu wa ratiba.
    Hivi karibuni, mgombea wa Chadema, Edward Lowassa alifanya ziara kwenye maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kwa kile alichoeleza ni kwenda kushuhudia kero za wananchi. Hata hivyo, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ilipiga marufuku ziara hizo kwa kile ilichoeleza ni sababu za kiusalama.
    Kampeni hospitalini
    Wakati huo huo, taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii jana imepiga marufuku hospitali na vituo vingine vya kutolea huduma za afya kutumika kuendeshea shughuli za kisiasa.
    Wizara imesema itakapoonekana kuwa baadhi ya wagombea wa nafasi za uongozi wana haja ya kutembelea hospitali kwa madhumuni tofauti na yale ya kuwajulia wagonjwa hali zao, itabidi waombe kibali maalumu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
    Taarifa iliyotolewa jana na wizara imesema kwa mujibu wa taratibu na miongozo ya huduma za afya, hospitali ni sehemu inayopokea na kulaza wagonjwa wenye matatizo mbalimbali ya muda mrefu na muda mfupi na wanahitaji kuendelea kupata huduma katika mazingira ya amani na utulivu.
    Onyo hilo la Serikali limekuja siku chache baada ya mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan kutembelea vituo vya afya vya Huruma katika wodi ya wazazi na Hedaru.
    Habari hii imeandikwa na Lucy Lyatuu na Sophia Mwambe


  • August 26, 2015

  • MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA YAKATAZA KUTUMIA HELKOPTA BILA KIBALI



    MAMLAYA YA USAFIRI WA ANGA YAKATAZA KUTUMIA HELKOPTA BILA KIBALI Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema kutokana na uzoefu wa nyuma kwamba katika kipindi cha kampeni za siasa, vyama vya siasa hutumia kila aina ya usafiri kuwafikia wananchi ambao ni wapigakura wao. Usafiri huo ni magari, pikipiki, baiskeli pamoja na ndege na helikopta kwa vyama vyenye ukwasi hivi sasa wanatakiwa kufanya yafuatayo.
    Watoa huduma za usafiri wa helkopta au ndege na marubani wake watakaokodishwa kutoa huduma wakati wa kampeni, wametakiwa kuzingatia kanuni za usafiri wa anga na kuomba kibali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania.
    1. UTANGULIZI
      1. Tangazo hili linatolewa kwa lengo la kutoa mwongozo kwa watoa huduma za helikopta, marubani wake na umma kwa ujumla kuhusiana na hatua za kiusalama zinazopaswa kuzingatiwa inapolazimika kutoa huduma ya usafiri wa helikopta hapa nchini, hususan, maeneo ya mbali (vijijini) ambapo huduma za uongozaji ndege hazipo au sio maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya helikopta kutua (mahsusi kwa helikopta au viwanja vya ndege kwa ujumla). Tangazo hili limetolewa baada ya Mamlaka kugundua kwamba kumekuwa na matumizi mabaya ya huduma hizi kinyume na kanuni za usafiri wa anga nchini na weledi unaozingatia taratibu za kitaaalamu na miongozo katika usafiri wa anga.
        .
      2. Mamlaka inatambua kwamba matumizi ya helikopta wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 yanatarajiwa kuongezeka na kuna uwezekano wa kuleta athari za kiusalama kwa maisha ya watu na mali pamoja na watumiaji wa vyombo hivi. Pia vitendo vya kuning'iniza vitu kama mabango ya matangazo mbalimbali kwa kutumia ndege (helikopta ikiwemo) yanaweza kuleta hatari endapo sheria na taratibu zinazohusiana na matumizi hayo hazitazingatiwa.
      3. Tangazo hili linatolewa kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mkuu chini ya Sheria Namba 80 ya Usafiri wa Anga na kanuni zake zinazohusiana na masuala ya usafiri wa anga nchini zilizowekwa kwa lengo, hususan, kuhakikisha usalama katika matumizi ya vyombo vya usafiri wa anga sambamba na kulinda usalama wa umma na mali wakati wa matumizi ya vyombo husika.
      4. Watoa huduma za usafiri wa helikopta au ndege na marubani wake wanaokodishwa kutoa huduma wakati wa kampeni, na mtu yeyote anayetarajiwa kutumia huduma hiyo wanakumbushwa kuhakikisha wanazingatia kanuni za usafiri wa anga na ikibidi kuomba kibali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania. Kanuni zinapatikana kupitia tovuti yetu kwa anuani ya:www.tcaa.go.tz; na endapo utahitaji maelezo ya ziada au miongozo zaidi usisite kuwasiliana na Mamlaka.
    2. CHETI CHA NDEGE KWA USALAMA WA KURUKA – AIRWORTHINESS CERTIFICATE
      1. Helikopta yeyote itakayotoa huduma katika kampeni za kisiasa lazima iwe ina cheti halisi cha usalama wa kuruka kilichotolewa na mamlaka husika ya helikopta ilikosajiliwa. Kwa hapa nchini cheti hicho ni lazima kiwe kimetolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga. Na cheti hicho ni lazima kiwe kimetolewa kwa ajili ya helikopta yenye usajili na mahsusi kwa kazi ya kubeba abiria ambayo inaweza kutumika kwa shughuli nyingine zozote. Kwa tangazo hili helikopta nyingine yeyote ile isiyokuwa na sifa hiyo haiwezi kutumika kufanya biashara ya usafiri wa abiria katika kampeni.
      2. Endapo helikopta itakuwa ina usajili wa nje ya Tanzania, mtu anayetarajia kuitumia hapa nchini ni lazima apate kibali cha kuiingiza nchini na kuitumia kwa usajili wa nchi iliyotoka kama ilivyoainishwa katika Waraka wa Mamlaka unaoainisha taarifa za usafiri wa anga – Aeronautical Information Circular (AIC 08/09). Hakikisha unapoomba kibali uwe umekidhi vigezo vya waraka huu ikiwa ni pamoja na kuwasilisha nakala za nyaraka zinazopaswa kuwasilishwa zikiwemo cheti cha usajili wa ndege, cheti cha ndege kwa usalama wa kuruka, cheti cha leseni za radio za ndege, cheti cha bima, makubaliano/mkataba wa kukodisha ndege hiyo, utaratibu wa kufanya matengenezo ya ndege hiyo, leseni za marubani, na ushahidi wa karibuni wa matengenezo ya ndege hiyo.
    3. TARATIBU ZA USALAMA WA UENDESHAJI
      1. Mahitaji ya jumla ya kiuendeshaji

        Matakwa ya marubani na uendeshaji unatakiwa kufuata maelekezo husika yaliyomo kwenye Kanuni inayohusiana na uendeshaji, yaani, The Civil Aviation (Operation of Aircraft) Regulations. Rubani Mkuu anawajibika kuhakikisha kwamba vituo vya Mamlaka vya kuongoza ndege vinavyohusika katika eneo atakalokuwepo au kwa utaratibu wa uongozaji ndege, wanakuwa na taarifa za mpango wake mzima wa safari husika kwa siku au wakati husika.

        Njia itakayotumiwa na rubani izingatie matakwa ya kuepuka kuruka chini ya kiwango cha umbali unaotakiwa hasa katika maeneo yenye watu wengi yakiwemo maeneo yaliyopangwa kufanyika kwa mikutano husika.

        Tahadhari ni lazima zichukuliwe wakati wa kuelekea kutua, kutua kwenyewe na hata wakati wa kuondoka, hasa ikizingatiwa kuwa kuna uwezekano wa wananchi kuikimbilia helikopta au eneo la utuaji. Katika hali yeyote ile rubani hapaswi kutumia chombo chake kukusanya wananchi kwa ajili ya mkutano au kuitumia kwa utaratibu wowote mwingine kinyume na matakwa ya kiurukaji kwa ndege husika.
      2. Usalama wa eneo la kutua na kuruka

        Maeneo yote yatakayotumika kwa ajili ya kutua ama kuruka ni lazima yafahamike mapema. Maeneo ya kuruka ama kutua ni lazima yawe mbali na eneo mkutano utakapofanyika ili kuweza kutoa eneo salama kwa ajili ya kuruka ama kutua kutoka katika mikusanyiko ya watu.

        Maeneo ambayo yatatambuliwa kama ni ya kuruka ama kutua hasa yale ambayo hayajatambulika kisheria kwa kufanyia shughuli hiyo ni lazima yawekewe alama maalum na uzio ili kuzuia watu wasiohusika kusogelea eneo hilo.

        Eneo husika ni lazima lilindwe; rubani mkuu ahakikishe helikopta itakayokuwa imetua eneo hilo inalindwa dhidi ya uvamizi kutoka kwa watu wasiohusika. Hatua maalum za kiulinzi ni vyema kuchukuliwa endapo kutakuwa na ulazima wa chombo hicho kulala katika eneo husika usiku mzima. Kila wakati rubani anapotaka kuruka ni vyema ahakikishe amekagua chombo chake kwa mujibu wa taratibu zinazohusika kwa umakini kabla ya kuanza safari.
      3. Usiamizi wa Chombo kikiwa ardhini na usalama kwa umma

        Mtu mwenye wajibu wa usimamizi wa chombo kikiwa ardhini lazima awe ni mwenye mafunzo ya kutosha na awe anajua madhara yanayoweza kusababishwa na mapanga ya helikopta yanapozunguka. Kwa marejeo zaidi kuhusiaha na hilo tafadhali zingatia yaliyomo kwenye Waraka wa Mamlaka AIC33/2000 unaoelezea masuala ya madhara yanayoweza kusababishwa na mapanga ya helikopta yanayozunguka.

        Ni wajibu wa Rubani mkuu na mhusika aliyekodisha helikopta kuhakikisha wananchi wanakuwa salama na mbali na helikopta. Matumizi ya kizembe na yasiyo ya kiweledi ya helikopta yatakayohatarisha usalama wa wananchi yatachukuliwa kama ukiukwaji wa kanuni za usafiri wa anga na Mamlaka itawachukulia hatua kama ilivyoanishwa kwenye kanuni hizo.
      4. Kuchukua na kuangusha vitu ardhini na kupeperusha mabango angani

        Huduma hizi zinaweza kufanywa na helikopta na hata ndege zingine za kawaida. Kabla ya kufanya shughuli za namna hiyo, mmiliki wa chombo ni lazima ahakikishe anakidhi vigezo vya Kanuni za Usafiri wa Anga kwa huduma hizi, yaani, The Civil Aviation (Aerial Work) Regulations na pia awe amepatiwa kibali kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga kwa kazi hiyo. Mmiliki wa ndege yeyote anayefanya shughuli za namna hii bila ya kuzingatia vigezo vya Kanuni hizi atachukuliwa hatua.
      5. Kutoa taarifa za matukio

        Rubani Mkuu ni lazima aandike taarifa ya matukio na kuiwasilisha Mamlaka ya Usafiri wa Anga kama ilivyoanishwa kwa mujibu wa kanuni za usafiri wa anga hususan, kanuni za 52, 74,75 na 76 zilizomo kwenye Kanuni ya The Civil Aviation (Operation of Aircraft) Regulations. Wananchi nao wanatakiwa kutoa taarifa ya tukio lolote waliloliona hatarishi kwa mujibu wa kanuni namba 262 ya Kanuni iliyotajwa.

        Mamlaka itafuatilia na kuchunguza taarifa inazozipokea na kuchukuwa hatua stahiki ili kuhakikisha kuwepo kwa usalama wa kiuendeshaji, watu na mali.
    4. HITIMISHO
      Ili kulinda usalama wa wananchi, wamiliki na marubani wote wanapaswa kuhakikisha wanazingatia Sheria ya Usafiri wa Anga pamoja na Kanuni zake. Rubani anayeendesha chombo ni lazima ahakikishe anatumia weledi wa hali ya juu katika matendo yake.

      Mamlaka inawahakikishia wananchi/umma kwa ujumla kwamba haitosita kuchukuwa hatua stahiki kama zilivyoanishwa kisheria na kanuni za usafiri wa anga iwapo mapungufu ya usalama yatajitokeza.

    Imetolewa na
    Charles M. Chacha
    Kaimu MKURUGENZI MKUU
    MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA


  • PROFESSOR JAY: SIENDI BUNGENI KUTETEA WASANII



    PROFESSOR JAY: SIENDI BUNGENI KUTETEA WASANII
    Wasanii wasitegemee msaada wa maana pindi Professor Jay akiingia bungeni. Rapper huyo anayewania ubunge kwenye jimbo la Mikumi mkoani Morogoro amesema atatumia wadhifa huo kuwahudumia wananchi wa Mikumi.
    Professor amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa atakuwa mbunge wa watu wa Mikumi hivyo atatumia muda kuwatumikia watu wake.
    "Nimewaambia wasanii wangu na wanajua nimechaguliwa kupeperusha bendera ya CHADEMA kwenye jimbo la Mikumi, lakini wengi wamesema watanisaidia kwa maneno lakini bado sijalaunch kampeni yangu rasmi. Natarajia kulaunch natarajia rasmi tarehe 5 mwezi wa tisa, sasa tunaangalia nani atani-support," amesema.
    "Mimi ni kijana na mimi ni mwanamuziki, watu waelewe naingia bungeni kwenda kuwawakilisha wananchi wa jimbo la Mikumi, kwahiyo tutafanya kazi sawa za wananchi wa jimbo la Mikumi na Professor atakuwa anaishi Mikumi na nitakuwa napatikana huko Mikumi."
    "Watu wasitegemee nitaingia bungeni kwenda kuongea masuala ya wasanii sana kuliko hata kuwawakilisha watu wa Mikumi. Watu wajue Professor Jay atakuwa mbunge wa watu wa Mikumi ni vile ni mwanamuziki nitapigania kwa hali na mali maslahi ya muziki ili kuweka sanaa katika level za juu zaidi.


  • RAIS MUGABE AZOMEWA NA WANANCHI WAKE HUKO NCHINI AKIWA ANAHUTUBIA HUKU WAKISEMA HIVII...



    RAIS MUGABE AZOMEWA NA WANANCHI WAKE HUKO NCHINI AKIWA ANAHUTUBIA HUKU WAKISEMA HIVII...

    Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe.
    Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amezomewa na wabunge wa upinzani alipokuwa anahutubia nchi kupitia bunge la nchi hiyo.
    Wakati wa hotuba hiyo kulikua na kelele za wabunge kiasi cha sauti ya kiongozi huyo kutosikika vizuri.
    Wabunge hao wanadai kuwa hakukua na jipya katika mipango aliyoeleza Rais Mugabe kuisaidia nchi hiyo kuondoka katika mgogoro wa kiuchumi unaoukabili.
    Pia waliimba nyimbo kuhusu chama tawala nchini humo kupoteza mvuto.
    Wabunge wa chama tawala cha ZANU-PF walijibu kwa kuimba kuwa kiongozi huyo mwenye miaka tisini na moja ataendelea kuwa madarakani.
    Hotuba yake iliisha kwa kipindi cha chini ya nusu saa,ni miongoni mwa hotuba fupi sana kuwahi kutolewa na kiongozi huyo.
    (Chanzo: BBC Swahili)


  • UKAWA WATAKA MAGUFULI AONGEZEWE ULINZI



    UKAWA WATAKA MAGUFULI AONGEZEWE ULINZI

    East Africa Radio
    Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Bw. Salum Mwalimu, amewataka CCM, kumwongezea ulinzi mgombea urais wao wa Jamhuriya Muungano, Dkt. John Magufuli ili asijiunge UKAWA. Alisema hivi sasa viongozi wa CCM wameimarisha ulinzi kwa makada wao wote maarufu ili wasijiunge UKAWA. "CCM wamwongezee ulinzi Dkt. Magufuli, wakimwachia dakika tano watasikia naye amejiunga UKAWA." Bw. Mwalimu aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi Kibandamaiti visiwani Zanzibar. source: MAJIRA


  • Waliotangazwa kupita bila kupingwa CCM wakatiwa rufaa



    Waliotangazwa kupita bila kupingwa CCM wakatiwa rufaa
    Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema), kimekata rufaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kwa majimbo ya Mlalo, Bumbuli, Ludewa na Peramiho yaliyotangazwa kuwa wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wamepita bila kupingwa kwa madai kuwa waliotangaza hawana mamlaka hiyo.
    Akizungumza Dar es Salaam jana, Wakili wa Chadema, Peter Kibatala alisema tayari utaratibu wa kuandaa rufaa hizo umeshakamilika.
    “Ninasimamia rufaa ya kesi tatu. Tunapinga wakurugenzi wa halmashauri kutangaza majimbo yao kuwa yana wagombea waliopita bila kupingwa wakati sheria haiwaruhusu kufanya hivyo.
    “NEC pekee ndiyo wanaweza kusema lolote baada ya kusikiliza kilichoamuliwa na mkurugenzi,” alisema Kibatala.
    Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa wagombea watano wa ubunge kupitia CCM wamepita bila kupingwa baada ya wawakilishi wa vyama vya upinzani kushindwa kujitokeza au kuwekewa pingamizi kutokana na makosa kadhaa ya kikanuni.
    Mgombea wa Chadema Jimbo la Bumbuli, David Chanyezhea alisema baada ya kupokea barua ya kuenguliwa na mkurugenzi wa uchaguzi wilayani kwa maelezo kuwa amekosa vigezo, amekata rufaa NEC kupinga uamuzi huo.
    Chanyezhea alisema hatua hiyo imechukuliwa baada ya jitihada za kumtaka ajiondoe kwenye kinyang’anyiro hicho na wapambe wa mgombea mwenzake wa chama kingine.
    “Nimeshaandika barua ya kukata rufaa na kuituma NEC. Ninaamini haki itatendeka kwani sheria inaruhusu mtu kugombea udiwani na ubunge kwa wakati mmoja na wapo wabunge wa namna hiyo kwenye mabunge yaliyopita,” alidai mgombea huyo.
    Hata hivyo, Wakili Kibatala alisema kutokana na makosa hayo, ana imani kuwa NEC itakuwa makini na kutoa majibu sahihi dhidi ya rufaa hizo.
    Alipoulizwa kuhusu mustakabali wa majimbo mawili yaliyosalia, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu alisema tayari hatua zimeshachukuliwa kwa lile la Peramiho na la Nanyamba.
    Mwalimu alisema hawawezi kulizungumzia Jimbo la Nanyamba kwa kuwa mgombea aliyesimamishwa alikuwa wa CUF
    “Huko kwingine yalikuwa masuala ya kiufundi pekee ndiyo yaliyoleta changamoto, lakini hali imekuwa ya kushangaza kidogo… mgombea hakurudisha fomu,” alisema Mwalimu.
    Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Shaweji Mketo zilieleza kuwa kuna harufu ya rushwa kwenye jimbo la Nanyamba ambako mgombea wa chama hicho hakurejesha fomu na kumfanya yule wa CCM kukosa mpinzani.


  • 11 Mbaroni kwa Tuhuma za Kuchoma Moto Kituo cha Polisi Morogoro



    11 Mbaroni kwa Tuhuma za Kuchoma Moto Kituo cha Polisi Morogoro

    POLISI mkoani Morogoro wanashikilia watu 11, wakazi wa Kijiji cha Mpofu wilayani Kilombero kwa tuhuma za kuvamia na kuchoma moto kituo kidogo cha polisi na ofisi ya serikali ya kijiji hicho.

    Watuhumiwa hao ni sehemu ya zaidi ya watu 100 wanaodaiwa kufanya uhalifu huo katika kituo hicho cha polisi Mbingu, katika taarifa ya Mgeta.

    Watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya tukio hilo wakishinikiza polisi wamwachie mtuhumiwa aliyewekwa mahabusu katika kituo hicho, Bashiri Kadugula (25), kwa tuhuma za kumshambulia mkewe, Veronica Chabula (21) ili wamwadhibu.

    Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, alisema jana kuwa, Kadugula aliwekwa ndani kwa kumkata mkewe kwa panga sehemu mbalimbali za mwili kutokana na wivu wa mapenzi.

    Alisema katika tukio hilo ni la Agosti 20, mwaka huu saa 4:00 usiku, mtuhumiwa huyo baada ya kufanya kitendo hicho kwa mkewe akitoroka na ndugu wa Veronica walifanikiwa kumkamata na kumfikisha kituo kidogo cha Polisi Mbingu, ili hatua za kisheria zichukuliwe.

    Alisema baada ya ndugu kuondoka kituo cha polisi, kitambo kidogo kulitokea kundi la watu wakirusha mawe kituoni hapo, wakitaka wamuue mtuhumiwa huyo kwa kukerwa na kitendo chake cha kinyama. Kamanda Paulo alisema, askari waliokuwepo kituoni hapo walijitahidi kuwazuia watu hao lakini walizidiwa nguvu.

    Alisema polisi walifanikiwa kumtoa mtuhumiwa mahabusu na kumwokoa sambamba na kuokoa silaha za kituo hicho.

    Alisema, watu hao waliokadiriwa kuwa zaidi ya 100, walivamia kituo hicho kidogo cha Polisi na kukichoma moto ambapo nyaraka mbalimbali zilizokuwa ndani ya kituo hicho ziliungua na kuteketea kabisa.

    Kamanda wa Polisi wa mkoa alivitaja vitu vilivyoteketea kwa moto kuwa ni pamoja na pikipiki tano zenye usajili T 979 BGA aina ya Sky Mark, T901 BUJ aina ya Sanlug, T801 BQA aina ya Sanlug, mali ya Askari Wilson, T194 BVR aina ya T-Better, mali ya Askari Isaya na T904 BUJ aina ya Tianda.

    Alisema, kundi la watu hao baada ya kukichoma moto kituo kidogo cha polisi, lilivamia pia Ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Mpofu na kisha kuchoma moto nyaraka mbalimbali, ambapo katika matukio hayo watuhumiwa 11 walikamatwa.

    Amewataja waliokamatwa kutokana na tukio hilo kuwa ni Imani Mwampombe (40), Geofrey Mwaikambo (46), Eugen Kikoti (41), Janken Mwaikambo (55), Meshack Kikoti (42), Eliud Chumbula (52) na Shukrani Lukimo (35) ambao ni wakulima na wakazi wa kijiji hicho cha Mpofu.

    Wengine waliokamatwa ni madereva wawili wa bodaboda ambao ni Ramadhani Hussein (29), mkazi wa Kitongoji cha Ngajengwana, Salum Ngala (36), John Mtikila (55) na Rodrick Mwaikambo (36) wote wakulima na wakazi wa Kijiji cha Tandale- Igima.

    Kamanda huyo wa Polisi wa mkoa alisema kwamba watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika na kwamba polisi wanaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine waliotoroka na kusisitiza kuwa wananchi wanapaswa kutii sheria na kuacha kujichukulia sheria mkononi.


  • Polisi wavamia msafara wa Lowassa




    Polisi wavamia msafara wa Lowassa
    Mgombea Urais wa tiketi ya              UKAWA, Edward Lowassa akizungumza na wafanyabiashara wa soko              la Tandale. Kushoto kwake ni Mgombea Mwenza, Juma Duni Haji
    Mgombea Urais wa tiketi ya UKAWA, Edward Lowassa akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Tandale. Kushoto kwake ni Mgombea Mwenza, Juma Duni HajiJESHI la Polisi Dar es Salaam leo limevamia na kuuzuia msafara wa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa kuingia sokoni Kariakoo.
    Polisi hao walikuwa kwenye magari aina ya Land Rover huku wakiwa na silaha za moto tayari kukabiliana na hali yoyote, walimzuia Lowassa ambaye alikusudia kwenda Kariakoo shimoni.
    Lowassa alifika Mtaa wa Swahili saa 6:09 mchana ikiwa ni mtaa mmoja kabla ya kuingia sokoni shimoni ambapo alikusudia kusalimia wafanyabiashara hao kama alivyofanya Tandale na Tandika.
    Kabla ya kufika Mtaa wa Swahili, msafara wa Lowassa ulianzia katika Soko la Tandale na baadaye alikwenda Tandika kusalimia wafanyabiashara na wakazi wa maeneo hayo.
    Polisi walimvamia na kuamuru msafara wake kuishia Mtaa wa Swahili kwa kile walichoeleza kutokuwepo kwa taarifa ya ujio wake pamoja na kuepusha msongamano ambao tayari ulianza kutokea.
    Msafara wa Lowassa ulisindikizwa na wafanyabiashara wa Kariakoo waliojitokeza kumpoke huku wakiimba nyimbo za kumsifu, ambao pia walinyimwa fursa ya kumuona.
    Waliimba "si si si… si mnaona, mziki wa Lowassa kuutuliza hamuwezi," maneno waliyoyarudia mara kwa mara.
    Polisi wamesema, Lowassa ambaye alikuwa ameongozana na kundi kubwa la vijana hakutoa taarifa mapema ili waimarishe ulinzi. Hata hivyo kulikuwa na majadiliano kati ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Lucas Mkondya na maofisa wa Chadema.
    Makubaliano yalihitimishwa kwa Lowassa na maofisa wake kukubali kutofika sokoni mahala alipotarajia kukutana na kuzungumza na wafanyabiashara hao.
    Alipokuwa Tandale
    Lowassa alitoka nyumbani nyumbani kwake Masaki saa 2:35 asubui na kuelekea katika Soko la Tandale.
    Kabla ya kufika sokoni Tandale, wananchi waliomwona kwenye gari walianza kumfuata, hata hivyo alikwenda mpaka sokoni ambapo alifika saa 3:20 ambapo alizungumza na wafanyabiashara wa hapo.
    Said Omary ambaye ni mfanyabiashara wa nafaka alimwomba Lowassa kuwa, akifanikiwa kutwaa nchi awaboreshee miundombinu ya barabara ili kurahisisha kuingiza bidhaa zao.
    "Soko halina ubora wowote maana CCM wanachangisha ushuru lakini hawalihudumii. Ni bora tuachiwe wenyewe tuliendeshe maana tunalipa ushuru wa bure."
    Omary alisema hayo baada ya kuulizwa na Lowassa kwamba, endapo ataingia madarakan, angependa amfanyie nini?
    Kabla ya kuondoka Lowassa alinunua maharage kwa Sh. 30,000 kutoka kwa mfanyabiashara huyo. Baadaye alikwenda kwa mfanyabiashara wa miwa aliyejitambulisha kwa jina la Gerard.
    Gerard amemwambia Lowassa "tunaomba ukiingia madarakani utukumbuke sisi vijana wako kwa kutupatia ajira ya kutosha maana hii biashara haina faida." Alipofika kwa muuza maziwa Lowassa alinunua kikombe kimoja na kunywa fundo moja.
    Alimaliza sokoni hapo saa 3:50 gari lake likisindikizwa na mamia ya watu pia akisindikizwa na vijana wa bodaboda.
    Kwenda Tandika
    Msafara uliingia katika Barabara ya Morogoro saa 4:01 asubuhi na kufuatiwa na pikipiki huku zikiwa zimebeba watu ambao walikuwa wakiimba nyimbo za kumsifu.
    Msafara uliingia Barabara ya Mandela na kukuta wananchi wakiwa wamejipanga kumsalimia kwa kumpungia mikono huku na yeye akifanya hivyo.
    Alifika Soko la Tandika saa 4:33 asubuhi ambapo shughuli zilisimama kwa muda huku mamia ya watu waliojaa sokoni hapo wakitaka kumuona.
    Lowassa bila ya kujali hali ya soko kuwa chafu, aliingia ndani na kuangalia bidhaa mbalimbali na bei zake.
    Lowassa akiwa ndani ya soko hilo alipata fursa ya kuzungumza na muuza maji ya kufunga maarufu kama 'kandoro' ambaye hakutaja jina lake.
    Alimuuliza kijana huyo kiasi gani anapata kutokana na biashara hiyo? alimjibu "hakuna faida yoyote, tunaganga njaa tu ilimradi mkono uende kinywani."
    Aidha, wananchi wengine waliokuwa wamefurika sokoni hapo walisikika wakisema "Baba tunakuomba uingiapo madarakani, utujengee soko letu maana halina hadhi, ni chafu na linanuka. CCM wameshindwa kazi, wanakula pesa zetu tu."
    Hata hivyo, wananchi wengi wa sokoni hapo walipoulizwa ni kwanini wameacha shughuli zao na kumsikiliza Lowassa, wamejibu "huyo ndio rais tunayemuhitaji ambaye akiwa madarakani atajua aanzie wapi kutatua shida zetu. Rais anatakiwa kuwa mtu wa watu kama huyu, hapa kashapita."


  • Afariki kwa kufukiwa na kifusi akichimba Madini.



    Afariki kwa kufukiwa na kifusi akichimba Madini.
    Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Kutiba Amani mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa kijiji cha Luegu wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,amekutwa akiwa amefariki Dunia na mwili wake kuharibika vibaya mara baada kufukiwa na kifusi akichimba madini aina ya Quamalin katika machimbo ya Mtwara.




    Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma,Bw.Mihayo Msikhela amesema mtu huyo aliondoka nyumbani kwake wiki mbili zilizopita kwenda katika machimbo hayo ya kijiji cha mtwara Wilaya ya Namtumbo kwa lengo la kuchimba madini aina ya Quamalin yanayo patikana katika machimbo hayo lakini siku chache zilizopita eneo hilo lilianza kutawaliwa na harufu kali ikitokea kwenye moja ya shimo alimokua akichimba.
     
    Hata hivyo siku mbili baadaye hofu ya wananchi kwamba kulikua na mwili zaidi ya mmoja ilianza kutanda zaidi kutokana na harufu kuendelea kuwa kali,na ndipo kamanda Msikhela akiongozana na daktari wa wilaya ya namtumbo na maafisa wa madini mkoa wa Ruvuma kuendesha upya zoezi la ufukuaji na kufanikiwa kupata mabaki ya eneo la mdomo wa chini ya mwili wa awali na kwamba hakuna miili mingine.
     
    Uchimbaji wa madini hayo kwa staili ya "FONKA" unaofanywa na wachimbaji wadogo katika maeneo mengi hapa mkoani ruvuma ni moja ya uchimbaji hatari ambapo wizara inayoshughulikia masuala ya madini imepiga marufuku.

    CHANZO:ITV.


  • NEC YAONYA VYAMA VYA SIASA VITAKAVYOKIUKA RATIBA ZA KAMPENI



    NEC YAONYA VYAMA VYA SIASA VITAKAVYOKIUKA RATIBA ZA KAMPENI
    Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, kuhakikisha vinafuata na kuheshimu ratiba ya uchaguzi waliyojiwekea.
    Katika taarifa kwa njia ya video iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani amesema kuwa vyama vyote vilishiriki katika kuandaa ratiba hiyo na kuwa viliiridhia hivyo hawana budi kuhakikisha wanaifuata.
    “Tulikaa na vyama, mimi sikuamua hii ratiba, wao walipendekeza na wakakubaliana na wakatoa ratiba hii, cha kwanza kabisa vyama vya siasa wazingatie waliyoyaweka humu,” alisema Kailima.
    Aliongeza kuwa utaratibu huo upo kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Uchaguzi ya 2015 na kuwa wakikiuka, sheria itawakamata.
    “Kwenye maadili (Sheria ya Maadili ya Uchaguzi 2015) kuna eneo ambalo vyama vya siasa na wagombea wanakubaliana kuzingatia muda wa kuanza kampeni na muda wa kumaliza kampeni,” alisema.
    Aliongeza kwa chama au wanasiasa watakaokiuka wataitwa kwenye kamati ya maadili na kuhojiwa na wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
    Agizo hilo la NEC linakuja siku chache baada ya CCM kuzindua kampeni zao siku ya Jumapili katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam ambapo shughuli hiyo ya uzinduzi ilihitimishwa majira ya saa 12.34 jioni, ikiwa ni nusu saa zaidi ya muda unaotakiwa kisheria


  • August 25, 2015

  • VIFAA VYA HALI YA HEWA TATIZO AFRIKA


    VIFAA VYA HALI YA HEWA TATIZO AFRIKA

    Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba 
    Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi amesema nchi za Afrika zina upungufu wa vifaa vya kutambua mvua zitakazonyesha kama ni El Nino.


    Kijazi alisema hayo jana alipokutana na wataalamu wa mamlaka ya hali ya hewa kutoka nchi za Afrika waliokutana kujadili na kuchukua hatua ya kukabiliana na majanga yatakayoambatana na mvua hizo.
    Dk Kijazi alisema wataalamu hao wanashindwa kuendesha kwa ufanisi shughuli za utabiri kutokana na vifaa kushindwa kutambua athari za mvua zitakazonyesha.
    "Tumekutana nchi 11 za Afrika ili kila nchi iweze kuchukua tahadhari ya mvua za El Nino... na tunasisitiza Serikali za nchi husika ziongeze vifaa vya kutosha vya kupima na kuchambua taarifa za hali ya hewa ili utabiri uwe wa ufanisi," alisema Dk Kijazi.
    Alisema hadi jana kipimo cha utabiri wa hali ya hewa kilikuwa kinaonyesha joto halijaongezeka katika Bahari ya Hindi, endapo kutakuwa na mabadiliko watatoa taarifa ili Serikali ichukue tahadhari.
    Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba alisema mkutano huo unahusu mashirika ya hali ya hewa kutoka nchi za pembe za Afrika kujadili msimu wa mvua utakaoanza Septemba hadi Desemba mwaka huu.
    Dk Tizeba alisema watazishauri Serikali za nchi husika kuchukua tahadhari kwenye mamlaka za miji kuhusiana na mvua hizo.
    Alisema mabadiliko ya hali ya hewa yatagusa kwenye sekta ya miundombinu na kilimo, hivyo Serikali itajipanga kuchukua hatua.
    "Tunasubiri majadiliano ya wataalamu wa hali ya hewa yanayofanyika siku mbili watuambie cha kutufanya," alisema Dk Tizeba.


  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.