Kituo cha kulea na kuendeleza watoto na wanafunzi yatima na wanaotoka katika mazingira magumu Lucy's Hope Centre kimesomesha watoto zaidi ya 400 (mia nne) kuanzia shule za msingi, vyuo vya elimu, vyuo vya ufundi, mpaka vyuo vikuu.
Wanafunzi zaidi ya ishirini ama wako vyuo vikuu au tayari wamehitimu shahada ya kwanza. Ili kukabiliana na changamoto ya ongezeko la wanafunzi wasiopata nafasi ya kuendelea na elimu ya kawaida, Kituo, kwa kushirikiana na wananchi wa Lufilyo, Busokelo, na wafadhili wapenda maendeleo kimejenga kampasi katika eneo la eka zaidi ya kumi,lengo likiwa ni kuanzisha mafunzo ya stadi mbalimbali.
Ili kupanua mawanda ya mafunzo hayo na ili Kituo kiweze kusaidia jamii katika Halmashauri ya Busokelo na Wilaya ya Rungwe na Taifa kwa ujumla, Mama Lucy Mwandosya na jamii ya Lufilyo wametoa Kituo hicho kwa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo.
Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo nayo imekitoa Kituo hicho kwa VETA ( Vocational Education and Training Authority ) ili kianzishwe Kituo cha VETA cha ufundi stadi( Vocational Education Training Centre).
Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo nayo imekitoa Kituo hicho kwa VETA ( Vocational Education and Training Authority ) ili kianzishwe Kituo cha VETA cha ufundi stadi( Vocational Education Training Centre).
Makabidhiano hayo yalifanyika katika sherehe fupi na iliyofana kijijini Lufilyo, mgeni rasmi akiwa Mheshimiwa Stella Manyanya, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia, na Ufundi.Pichani juu Mama Lucy Mwandosya na Prof. Mark Mwandosya wakimkabidhi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Busokelo Mhe. Anyosisye Njobelo ufunguo wa Kituo ili amkabidhi Mheshimiwa Waziri.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundu Mhe. Eng Stella Manyanya akikabidhiwa hati rasmi ya kituo hicho
Mandhari ya kituo cha kulea na kuendeleza watoto na wanafunzi yatima na wanaotoka katika mazingira magumu Lucy's Hope Centre |
0 comments:
Post a Comment