February 22, 2016

  • MKURUGENZI WA MANISPAA ATOA UFAFANUZI WA UCHANGIAJI WA UJENZI WA SHULE ZA SEKONDARI.



    MKURUGENZI WA MANISPAA ATOA UFAFANUZI WA UCHANGIAJI WA UJENZI WA SHULE ZA SEKONDARI.
    Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
    BAADA ya Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Boniface Jacob kuhoji misaada mbalimbali inayotolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari za manispaa  hiyo ambao unasimamiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Ando Mwankuga amesema kuwa misaada  ujenzi wa shule hizo,unasimamiwa na manispaa chini ya Afisa Ugavi.

    Mwankuga ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya misaada inayotolewa na wadau mbalimbali juu ujenzi wa Shule za sekondari saba katika manispaa hiyo.

    Amesema kuwa  Desemaba mwaka jana baada ya kuonekana na upungufu wa vyumba vya madarasa katika manispaa hiyo ambapo wanafunzi 3000 wangeweza kukosa nafasi hiyo Mkuu wa Wilaya alianzisha mpango wa uchangiaji kwa wadau mbalimbali katika kuweza kufanikisha ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa.

    Kaimu Mkurugenzi ameongeza kuwa katika msaada wadau waliochangia ujenzi huo wameweza kupata mifuko ya saruji 3190 na bati 100 na vitakwenda kufanya kazi iliyopangwa baada ya kupata taarifa kwa maafisa mipango miji.

    Amesema  kuwa ni shule za kata mbili zinaendelea kujengwa kati  saba zenye mahitaji ya kuongeza vyumba vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi 3000 kupata nafasi ya kusoma na sio kubaki nyumbani.
    Aidha amesema katika ukusanyaji wa michango hiyo hakuna fedha iliyotolewa na wadau ,akaunti yake haina fedha yeyote na vitu vyote viko salama.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.