Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

Showing posts with label Siasa. Show all posts
Showing posts with label Siasa. Show all posts

July 16, 2014

  • CHADEMA YATULIZA WANANCHI, YAAHIDI KATIBA MPYA ITAPATIKANA



    CHADEMA YATULIZA WANANCHI, YAAHIDI KATIBA MPYA ITAPATIKANA

    Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Katiba mpya ya Tanzania itapatikana na kusisitiza kuwa suala la kundi la wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba linalounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kurejea bungeni, linategemea utekelezaji wa masharti yao.

    Bunge Maalumu la Katiba linatarajia kuendelea na vikao vyake Agosti 5 mwaka huu baada ya kuahirishwa Aprili 25 mwaka huu, kupisha shughuli za Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano na lile la Wawakilishi, Zanzibar.

    Sambamba na hilo, Chadema baada ya  
    kufuta na kuahirisha uchaguzi wake wa ndani kwa mara kadhaa, imetangaza kuendelea na hatua hiyo na kuweka wazi kuwa, haitasita kufuta uchaguzi pale itakapobaini kuna ukiukwaji wa Katiba yake katika mchakato huo.
    Katika uchaguzi huo, mapema Septemba mwaka huu, nafasi za juu za uongozi ikiwemo ya mwenyekiti inayoshikiliwa hivi sasa na Freeman Mbowe tangu mwaka 2004 na ya katibu mkuu aliyoko Dk Slaa aliyeshika nyadhifa kadhaa za juu tangu mwaka 2000, itapata ama viongozi wapya au wenye nazo kuendelea.
    Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa aliwaambia waandishi wa habari jana katika Makao Makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam kuwa Katiba mpya kwa Watanzania itapatikana lakini ikiwa mchakato mzima hautagubikwa na matakwa binafsi na ubabe.
    "Huwezi kupata Katiba nzuri kwa mfumo unaoendelea sasa, kwa sababu ni ubabe
    unaendelea. Na kuna waraka umeandaliwa kuhusu mwenendo wa katiba..." alisema Dk Slaa bila kufafanua kuhusu waraka huo.
    Alisema suala la Ukawa kurejea bungeni linawezekana, lakini msimamo wao uko pale pale katika kutimiziwa masharti yao waliyotoa.
    Miongoni mwa madai ya Ukawa kutoka nje ya Bunge ni kutoridhishwa na mwenendo mzima wa vikao vya Bunge hilo; kudai Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeteka mchakato wa Katiba; kutaka kujadiliwa kwa rasimu iliyoletwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
    Kumekuwepo na jitihada za kuwasihi Ukawa warudi bungeni zikifanywa na uongozi wa Bunge hilo Maalumu akiwemo Spika wa Bunge hilo, Samuel Sitta, viongozi wa kidini na serikali akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na viongozi wengine.
    Dk Slaa katika mkutano huo wa jana, alisema wanaowataka Ukawa warudi bungeni
    ili wakajenge hoja waelewe kwamba hakuna hoja zinazojengwa.
    "Chadema haitavumilia uongo…, tunaomba viongozi wa madhehebu ya dini watuelewe, sisi hatutavumilia uongo. Tunaamini Katiba ya Tanzania itapatikana hata kama si leo," alisema Dk Slaa.
    Alisema anashangaa kuona viongozi wa Ukawa wakitakiwa kuhudhuria kikao cha kamati ya maridhiano wakati wapo nje na kwamba, kwanza wanatakiwa kufahamu kama watarudi bungeni.
    "Watu wetu wa Ukawa hawatahudhuria kamati hiyo kwa sababu walitakiwa kufahamu kwamba je, watu hao watarudi bungeni au hawatarudi ndio waendelee, lakini msimamo wa watu wetu watarudi endapo masharti yatafikiwa, je yamefikiwa?" Alihoji Dk Slaa.
    Kuhusu uchaguzi ndani ya chama hicho, alisema chama kinaendelea na uchaguzi katika ngazi za majimbo na wilaya hadi taifa.
    Alisema tangu mwaka 2004 wamekuwa wakizunguka nchi nzima na wameweza kuunda kanda 10 zilizofanikisha kupatikana kwa mabalozi wa nyumba kumi nchi nzima na kwamba kwa sasa wana matawi 16,000 na wenyeviti wa vitongoji 196,000 nchini, kuacha  mikoa ya Mtwara na Lindi ambayo hawakuruhusiwa kufika.
    Kwa mujibu wa Dk Slaa, uchaguzi ngazi ya majimbo na wilaya unaendelea tangu Juni 26 hadi Julai 18 mwaka huu na kipindi cha rufaa ni hadi Agosti 2. Agosti 3 ni uchaguzi ngazi ya mkoa na Agosti 22 na 26 ni maandalizi ngazi ya Taifa.
    Dk Slaa alisema Agosti 27 wataanza mchakato wa uchaguzi mkuu ngazi ya Taifa utakaofanyika kwa siku tano. Alisema siku hiyo pia utafanyika uchaguzi wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) na Wazee. Agosti 28 utafanyika uchaguzi wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha).
    Aidha, Dk Slaa alisema Agosti 29 itakutana Kamati Kuu ya kwanza na Agosti 30 litakutana Baraza Kuu linalomaliza muda wake. "Agosti 31 utafanyika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi ambapo atachaguliwa Mwenyekiti Taifa na Makamu Mwenyekiti wawili wa upande wa Bara na wa Zanzibar".
    Alisema Septemba mosi litakutana Baraza Kuu jipya litakalochagua Katibu Mkuu na
    manaibu wake wawili pamoja na wajumbe wa Mkutano Mkuu na Septemba 2 itakutana Kamati Kuu mpya.


  • July 12, 2014

  • Ahadi za JK 2010 - 2015 - Tufanye Tathmini Ndogo zipi zimetekelezeka?

    Ni Takribani mwaka mmoja tu sasa umebaki ili kutimia ile miaka mitano ya utawala wa JK. Na nilipojaribu kuingia kwenye kumbu kumbu zangu, nikaamua kuibuka na vitu vilivyowafanya watanzania wakaamua kumchagua JK kuongoza tena. TUjadili, ni ahadi ipi kati za hizi imetimia, na kwa ubora gani? Maana kutimia tu si hoja, hoja ni ufanisi, na ubora wake kwa waahidiwa!

    AHADI - ALIITOA AKIWA WAPI...

    1.      Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora

    2.      Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini

    3.      Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga

    4.      Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga

    5.      Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma

    6.      Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini

    7.      Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma

    8.      Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera

    9.      Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera

    10.  Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini

    11.  Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini

    12.  Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera

    13.  Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera

    14.  Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera

    15.  Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya

    16.  Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera

    17.  Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali

    18.  Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza

    19.  Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza

    20.  Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita

    21.  Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba

    22.  Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro

    23.  Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini

    24.  Kujenga bandari Kasanga – Rukwa

    25.  Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea

    26.  Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya

    27.  Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga

    28.  Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa

    29.  Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro

    30.  Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini

    31.  Kuboresha barabara za Igunga - Tabora

    32.  Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu

    33.  Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini

    34.  Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara

    35.  Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma

    36.  Kulinda haki za walemavu - Makete

    37.  Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini

    38.  Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha

    39.  Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini

    40.  Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora

    41.  Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini

    42.  Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma

    43.  Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido

    44.  Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga

    45.  Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini

    46.  Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma

    47.  Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido

    48.  Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro

    49.  Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara

    50.  Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini

    51.  Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini

    52.  Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa

    53.  Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa

    54.  Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa

    55.  Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda

    56.  Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara

    57.  Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa

    58.  Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar

    59.  Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar

    60.  Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti

    61.  Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma

    62.  Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma

    63.  kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma

    64.  Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma

    65.  Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam

    66.  Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara

    67.  Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha

    68.  Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha

    69.  Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha

  • July 11, 2014

  • BancABC YAFUTURISHA WADAU WAKE JIJINI DAR



    BancABC YAFUTURISHA WADAU WAKE JIJINI DAR
    Sheikh Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum(kulia) akizungumza na wageni waalikwa wakati futari iliyoandaliwa na BancABC kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jana.
    Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa wakimsikiliza mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum(hayupo pichani) wakati wa futari iliyoandaliwa na BancABC kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jana.
    Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa wakichukua futari iliyoandaliwa na BancABC kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jana.
    Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa wakila futari iliyoandaliwa na BancABC kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jana.


  • Attention- Weruweru Alumni in the Diaspora


    Attention- Weruweru Alumni in the Diaspora
     Now, we have been receiving lots of inquiries on how the Weruweru Alumni community living outside of Tanzania, can get access to the Khanga, Tshirts and Mugz of Weruweru Alumni?! ...Today,let me help you all with the answer.
     Our Alumni Association leaders and Steering Committee will be traveling in different countries for their personal and official duties... What they will be doing is, CARRYING a number of Khanga, Tshirts and Mugs for those Alumni who will be ready to buy them. How would you get them?
     Get in contact with ME through missiepopular@gmail.com and place your order. Your email should include the number of pairs of Khanga you need and the city you are from and I will do the needful to ensure the package reaches you!
     Yes...it is as simple as that!... Don't let the movement pass you, grab your memorabilia and feel the Weruweru love wherever you are!

     Oooooh I love these women! My Weruweru family...
     The Prices for these items are GPB 5 for those in UK and 10$ for the rest...
    Share the Weruweru experience with the world ....Grab your memorabilia Today



  • PICHA ZIARA YA VIONGOZI WA TANZANIA SINGAPORE



    PICHA ZIARA YA VIONGOZI WA TANZANIA SINGAPORE
     Kutoka kushoto ni mkurugenzi wa taasisi ya biashara ya kimataifa iliyo chini ya wizara ya viwanda na biashara Singapore, Rahul Ghosh akibadilishana mawazo na Denis Rweyemamu na Linda Manu kutoka taasisi ya Uongozi ya Tanzania ambayo ndiyo iliyoandaa ziara ya mafunzo kwa makatibu wakuu na vionzoi waandamizi wa serikali ya Tanzania nchini Singapore.
     Baadhi ya makatibu wakuu walioko kwenye ziara ya mafunzo nchini Singapore yaliyoandaliwa na taasisi ya uongozi Tanzania, kutoka kushoto ni Dk Shabn Mwinjaka- Katibu mkuu wizara ya uchukuzi, Dk Ffolens Turuka- Katibu mkuu ofisi ya Waziri Mkuu,Dk Philip Mpango- Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Mipango na Dk Sivvacius Likwelile- Katibu Mkuu wizara ya Fedha.
    Ujumbe wa makatibu wakuu na viongozi waandamizi wa serikali ya Tanzania wakiwa katika mafunzo nchini Singapore, kuhusu uendeshaji wa shughuli za serikali kwa ushirikiano na sekta binafsi PPP mfumo ambao umeisaidia kimaendeleo nchi ya Singapore, Ziara hii inaratibiwa na taasisi ya Uongozi ya Tanzania- Uongozi Institute. (Picha zote na Vedasto Msungu Singapore)


  • PICHA ZA VIONGOZI WALIOKO SINGAPORE KWA MAFUNZO



    PICHA ZA VIONGOZI WALIOKO SINGAPORE KWA MAFUNZO
     Picha ya pamoja ya viongozi waandamizi wa serikali ya Tanzania walioko nchini Singapore kwa mafunzo yaliyoandaliwa na taasisi ya Uongozi ya Tanzania. Picha hii imepigwa nje ya jengo la taasisi ya HYFLUX ya nchini Singapore, taasisi binaffsi inayojishughulisha na kusafisha maji ya baharini na maji machafu kwaajili ya matumizi ya majumbani. Singapore haina chanzo cha maji ya mito wala visima kwahiyo maji yake kwa matumizi ya majumbani huagizwa kutoka nchini Malayisia
     Nchi ya Singapore ni miongoni mwa nchi zenye majengo marefu duniani, nchi hii ni ndogo yenye ukubwa wa kilomita za mraba 716 tu eneo ambalo ni dogo hata kuliko ukubwa wa baadhi ya vijiji vya Tanzania hivyo inalazimika kujenga majengo yake kwenda juu yaani maghorofa kama yanavyoonekana na kuna majengo yenye ghorofa mpaka 72 kwenda juu.
    Baadhi ya viongozi waandamizi wa Tanzania walioko kwenye ziara ya mafunzo nchini Singapore wakipata maelezo ya namna mitambo ya kuchuja na kusafisha maji ya baharini kwaajili ya matumzi ya majumbani inavyofanya kazi,. Ziara ya viongozi hawa wa serikali ya Tanzania iliyoandaliwa na taasisi ya Uongozi inalenga kujifunza kuhusu uendeshaji wa serikali chini ya mfumo wa ubia kati ya serikali na sekta binafsi ambao umesaidia kuharakisha maendeleo ya nchi ya Singapore.


  • PINDA ASAFIRI KWA TRENI KWENDA READING KUZUNGUMZA NA WATANZANIA


    PINDA ASAFIRI KWA TRENI KWENDA READING KUZUNGUMZA NA WATANZANIA

    Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akipanda treni kutoka Reading kwenda London Uingereza baada ya kuzungumza na watanzania waishio Reading Julai 10, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  • WAZIRI NYALANDU AMWAGA MSAADA WA MILIONI 10 WA MABATI 420 SHULE ZA SEKONDARI KWA AJILI YA MAABARA



    WAZIRI NYALANDU AMWAGA MSAADA WA MILIONI 10 WA MABATI 420 SHULE ZA SEKONDARI KWA AJILI YA MAABARA
    mwenyekit
    Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Iddy Mnyampanda akizungumza shule ya sekondari Kinyeto.

    Na Hillary Shoo, SINGIDA.
    Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Mkoani Singida, Lazaro Nyalandu ametoa mchango wa mabati 420 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 kwa shule mbili za sekondari za Kata za Mtinko na Kinyeto.
    Mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Jimbo hilo kuchangia katika ujenzi wa maabara mbalimbali kwenye shule za sekondari za Jimbo hilo.

    Akikabidhi msaada huo kwa Niaba ya Nyalandu ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Narumba Hanje aliwataka wananchi kuheshimu michango ya Mbunge wao na kuachana na porojo za siasa za mitaani.
    kinyeto
    Diwani wa Kata ya Kinyeto, Francisco Ng'eni akizungumza kwenye shule ya sekondari Kinyeto wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mabati 200.
    "Nataka niwaulize swali hivi ni wananchi ndio wenye matatizo au ni sisi viongozi, jibu ni rahisi ni sisi viongozi ndio wenye matatizo, haiwezekani Mbunge anatoa msaada mkubwa namna hii halafu watu wanajipitishapitisha wakitukana." Alisema Hanje kwa hasira.

    Aidha alisema wapo watu wanaompaka matope Waziri Nyalandu, lakini matunda yake yanaonekana na anaendelea kutekeleza ahadi zake.
    "Mimi inanishangaza sana kuna watu wameanza kujipitisha pitisha huko na wengine wanatukana kisa eti ni kaligi sijuji Mpombo Cup, fanya vitu vionekane sio maneno maneno kaka, na mimi ndiye mtekelezaji mkuu wa Ilani ya Chama Willaya hii." Alisema Hanje kwa kujiamini.
    diwani
    Diwani wa Kata ya Kinyeto, Francisco Ng'eni akipokea msaada wa mabati 200 kutoka kwa Mwenyekiti Hanje kwa niaba wa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe, Lazaro Nyalandu.



  • MGOMBEA URAIS WA MSUMBIJI KWA TIKETI YA FRELIMO AKUTANA NA RAIS KIKWETE



    MGOMBEA URAIS WA MSUMBIJI KWA TIKETI YA FRELIMO AKUTANA NA RAIS KIKWETE
     Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya chama cha Ukombozi cha FRELIMO Filipe Nyusi akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Ndogo mjini Tanga, mgombea huyo alipokwenda kumsalimia na kuwa na mazungumzo na Rais leo.
    Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma, wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mgombea huyo kwa tiketi ya FRELIMO Filipe Nyusi, Ikulu Ndogo mjini Tanga. Kushoto ni Mwenyeji wa Mgomba huyo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Picha na Adam Mzee wa CCM Blog.


  • MKURUGENZI WA SEKRETARIETI YA DUNIA YA NISHATI AKUTANA NA BALOZI KAMALA




    MKURUGENZI WA SEKRETARIETI YA DUNIA YA NISHATI AKUTANA NA BALOZI KAMALA
    Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Dunia ya Nishati Bwana. Steivan Defilla (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) baada ya kumaliza kikao ofisini kwake. Kulia ni Bwana. Nodal Tayel Mratibu wa Taasisi hiyo. Ujumbe huo ulifika Ubalozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya, Brussels kueleza faida za nchi kuwa mwanachama wa Taasisi ya Nishati Duniani.


  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.