Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

Showing posts with label Mahusiano na Mapenzi. Show all posts
Showing posts with label Mahusiano na Mapenzi. Show all posts

June 01, 2014

  • VIJANA WAASWA KUJIEPUSHA NA NDOA KATIKA UMRI MDOGO



    VIJANA WAASWA KUJIEPUSHA NA NDOA KATIKA UMRI MDOGO
    PIX 3 (2)
    Afisa Msaidizi wa Vijana kituo cha UMATI tawi la Dar es Salaam Bi. Upendo Daud akiwaeleza vijana kuhusu mada kuu ya Tamasha ambayo ni "Athari za ndoa za utotoni" wakati wa ufunguzi wa tamasha la mwezi katika kituo hicho.

    PIX 5 (1)Mwenyekiti wa mtaa wa Wailes Bw. Abdul Kidege ambaye ndiye mgeni rasmi katika Tamasha la Jamvi la vijana kituo cha UMATI jijini Dar es Salaam akitoa hotuba yake fupi kwa vijana waliohudhuria tamasha hilo lenye lengo la kuwaeleimisha vijana juu ya athari za ndoa za utotoni.
    PIX 6 (1)PIX 7Vijana wakifuatilia kwa makini hotuba ikiyotolewa na mgeni rasmi kabla ya ufunguzi wa Tamasha la Jamvi la Vijana Kituo cha UMATI jijini Dar es Salaam.
    PIX 17Vijana toka kundi la The Africa wakionesha igizo maalum linalohusu athari ya maradhi mbalimbali yakiwemo TB na Ukimwi yanayoweza kuwakumba vijana katika maisha yao ya ujana endapo hawatakuwa makini na jinsi gani ya kujiepusha nayo.
    Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dar es Salaam
    NDOA nyingi za utotoni husababishwa na tabia ya baadhi ya wazazi na walezi kuwalazimisha watoto wao wa kike kuolewa katika umri mdogo kwa tamaa ya kujipatia fedha ama utajiri katika familia zao jambo ambalo linawanyima haki ya kusoma watoto wengi kwani watoto hawa wanakuwa wako katika umri chini ya miaka kumi na nane.
    Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Wailesi Wilaya ya Temeke Bw. Abdul Kidege wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Jamvi la Vijana linalofanyika kila mwisho wa mwezi katika kituo cha vijana UMATI jijini Dar es Salaam.
    Bw. Kidege amesema kuwa kuna baadhi ya wazee na vijana wenye tabia ya kuwarubuni wasichana wadogo kwa kuwapa pesa na vitu vya thamani kwa lengo la kuwashawishi kuolewa nao na pia kuna baadhi ya wazazi ambao wakati mwingine ushirikiana katika kufanikisha azma hiyo jambo ambalo ni kinyume na haki za watoto katika jamii.
    "Kuna baadhi ya wasichana wenye umri mdogo wamekuwa wakinyanyaswa kijinsia kwa kubakwa na wengine kulazimishwa na wazazi wao wenyewe kuolewa na watu wazima ambao wamewazidi umri, jambo hili halikubariki na vijana nawaasa msikubali kurubuniwa kwa pesa au vitu toka kwa watu wa namna hiyo". Alisema Bw. Kidege.
    Kwa upande wake Afisa Vijana Msaidizi Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI) Bi. Upendo Daud amewaeleza vijana waliohudhuria tamasha hilo kuwa vijana wanapohudhuria matamasha katika kituo cha UMATI wanapata fursa kubwa ya kupata elimu bure juu ya afya ya uzazi, athari za mimba za utotoni, kupima Ukimwi, ushauri nasaha, uzazi wa mpango pamoja na uelimishaji rika jambo ambalo linawafanya vijana wengi waweze kujitambua na kujikinga.
     "Hili ni Tamasha kwaajili ya vijana linaloandaliwa kila mwisho wa mwezi na Youth Action Movement (YAM) kwa lengo la kuwaelemisha vijana juu ya mambo mbalimbali yanayohusiana na afya na mada kuu ya tamasha hili kwa leo ni Ndoa za umri mdogo  na athari zake". Alisema Bi. Upendo.
    Youth Action Movement (YAM) ni kikundi cha Vijana ambacho kilianzishwa na chama cha uzazi na malezi bora Tanzania (UMATI) kwa ufadhili wa Internationa Planned Parenthood Federation (IPPF). Chama hiki cha vijana kinapatikana katika kila tawi la UMATI nchi nzima na kwa tawi la Dar es Salaam ndiyo waandaaji wa Jamvi la vijana kila mwezi ambapo husaidia kutoa huduma bure kwa vijana kuhusu afya ya uzazi, kupima Ukimwi, ushauri nasaha, uzazi wa mpango pamoja na uelimishaji rika


  • May 29, 2014

  • Je Kwa Mwanamke Ndoa Ndiyo Kila Kitu?

    Katika makuzi yangu kama binti wa Kiafrika nimefunzwa mambo mengi kuhusu maisha na wajibu wangu kama mtoto wa kike.

    Baada ya kuvunja ungo nilianza kuandaliwa kuwa mke mtarajiwa wa mwanaume nisiyemfahamu. 

    Nimefunzwa kupika, nimefunzwa usafi wangu wa mwili, nimefunzwa usafi wa nyumba, nimefunzwa kuvumilia maisha ya ndoa na nikaaminishwa kwamba mwanaume ndiye kichwa cha nyumba na nikafunzwa wajibu wangu katika kumtumikia, lakini pia nikafunzwa kupanga bajeti na kuweka akiba ili huyu mume ambaye ni kichwa cha nyumba akikwama kupata mkate wa kila siku kwa ajili ya familia niweze kumsaidia.

    Kwa kifupi ni kwamba nilifunzwa mambo mengi lakini yote hayo yakiniaminisha kwamba siku isiyo na jina lazima nitaolewa na kuwa chini ya mwanaume ambaye atakuwa ndiye kila kitu kwangu.

    Nakumbuka wakati fulani baada ya mama kuona mabinti ambao nalingana nao umri na wengine nikiwa nimewazidi umri wakiolewa pale mtaani mama alianza kunidodosa kama sijapata mtu kama wenzangu.

    Lakini pia alijaribu kutumia misamiati mbalimbali na mafumbo lakini nilielewa kwamba alikuwa anamaanisha nisiwe mgumu sana kwa wanaume kwani sijui aliyevutiwa na mimi na anayetaka kunioa. 

    Nadhani alikuwa anataka kufikisha ujumbe kuwa umri unasonga na wenzangu wanaolewambona miye sisomeki?

    Naamini si mimi peke yangu, ninayekabiliana na changamoto hizi za wazazi na jamii kwa ujumla.

    Ukweli ni kwamba malezi ya mtoto wa kike yanamuandaa kuwa mke wa mtu, yanamuandaa kuolewa na yanamuaminisha kwamba ndoa ndiyo kila kitu.
  • To All Married Men, Nini Kilikufanya Umchague Yeye Kuwa Mkeo?

    Najua ni mapema sanaaa yani kuwaza habari za mapenzi asubuhi yote hii,ila mara moja moja si mbaya....
    Okay back to topic.....
    Hii ya leo inawahusu wanaume mliooa au ambao mko engaged kuelekea ndoa,vijana ambao bado mna chagua chagua tafadhali acheni kaka zenu waseme au mkisema basi muwe mnasema ya kweli....

    Swali ni hivi....NINI KILIKUFANYA UMCHAGUE MKE/MCHUMBA ULIENAE??...what made you conclude she is the one?...sababu zipi yani,uzuri wake,sura,umbo,tabia,elimu,kip ato?au ulimpa ujauzito au ulijua tangu siku ya kwanza umemuona au??au kuna situation flani ilitokea ndo ukajua ndo yeye...au?.....au?.....
    mi sijui,naomba mtuweke wazi mkiambatanisha na mifano 'practical' kabisaaa itakuwa poa zaidi....

    Mind you,utakaposema hapa utamsaidia rafiki yako ,mdogo wako ama ndugu yako kupata uelewa yakinifu kuhusu wanaume linapokuja swala zima la ndoa.....mana kama mjuavyo waliozidiwa desperado wanazinatafuta hadi kwa waganga eti hhehehe...naamini hii ishu haina uchawi yani...

    Karibuni sana kwa michago,kejeli si mpango,vichekesho ruksa......
  • May 28, 2014

  • Mume amburuza mkewe Mahakamani kwa kosa la kumnyima tendo la Ndoa..!!

    Kuna kisa kimeibuka nchini Uingereza ambapo mwanamume mmoja kwa jina David Mason, mwenye umri wa miaka 30, alimshitaki mkewe Brenda kwa kumnyima haki yake ya kingono au kukataa kushiriki tendo la ndoa.
    Mwanamke huyo alimfanyia mgao wa wiki moja kila mwezi wa kitendo cha ndoa mumewe kwa hofu ya kushika mimba kwa mara ya tatu.
    Kwa mujibu wa jarida la mtandao la Mirror, la Uingereza, Bwana Mason, ambaye kazi yake ni fundi mitambo alishinda kesi hiyo mwaka 1980.
    mary2
    Lakini mkewe alikataa rufaa ambapo Mason alipoteza kesi hiyo baada ya majaji kusema kuwa mahakama isingeweza kuamua kuwa mkewe Mason alimkosea.
    mary4
    Nini maoni yako kuhusu tukio hili?
  • NIMEMMISS MUME WANGU..MAMA MKWE KAJA ANA MWEZI NA HANA DALILI YA KUONDOKA TUNAISHI CHUMBA KIMOJA


    NIMEMMISS MUME WANGU..MAMA MKWE KAJA ANA MWEZI NA HANA DALILI YA KUONDOKA TUNAISHI CHUMBA KIMOJA
     
    Wapenzi nna mdogo wangu ana kama 26 kaolewa na mtu wa Dodoma. Naishi nae karibu kama nyumba 5 kutoka kwangu amepanga chumba1 self containal.

    Sasa kama mwezi mkwewe alikuja kumsalimu. 

    Na alisema anakaa siku3 jamani hadi leo mumewake analala kwa marafiki zake juzi nasikia anaongea na ndugu zake kuwa atarudi hadi pasaka iishe jamani mwezi na siku kadhaa na analala kitandani bila aibu. 

    Anaogopa kumwambia mumewe atahisi anamchukia mama yake na hivyo anataka jumamosi kuondoka kwenda kwao Morogoro ila mkwe haoneshi hata. Kuondoka kasema kama haukaisana utanikuta.
    Hebu mshauri mdogo angu jamani.



  • May 26, 2014

  • Ndoa ya Milioni 96 ya Vicky Kama Haipo Tena..Hizo Ndio Sababu

    Hadi gazeti hili linaondoka kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza jijini Dar juzi saa 10:00 jioni, ndoa ya Mbunge Vicky Kamata iliyokuwa ifungwe hapo iliyeyuka.

    Vicky Kamata ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya UVCCM, Mkoa wa Geita alikuwa afunge ndoa na mwanaume aliyejulikana kwa jina la Charles wa jijini Dar.

    KATEKISTA AZUNGUMZA NA IJUMAA WIKIENDA
    Baada ya kuona muda unakwenda bila kuwepo kwa dalili za wahusika kufika  kufunga ndoa hiyo ambayo harusi yake ilidaiwa ingetumia shilingi milioni 96, wanahabari wetu walimtafuta Baba Paroko, Cuthbert Maganga ili kumsikia anasema nini kuhusu hilo.

    Hata hivyo, mtu aliyedai ni katekista wa kanisa hilo alisema paroko alikwenda hija, Buguruni, Dar.
    Kuhusu ndoa ya Vicky Kamata, katekista huyo alidai Jumapili ya Mei 18, 2014 ndani ya ibada za kanisa hilo ilitangazwa hadharani ‘laivu’ kwamba haitafungwa.

    SABABU ZA KANISA
    Habari za ndani zilidai kuwa kanisa lilibaini upungufu mkubwa kwa bibi harusi na kumwambia ndoa haitakuwepo.

    Upungufu huo ni pamoja na Vicky Kamata kushindwa kuwasilisha cheti chake cha ubatizo, pia hakuwahi kupata kipaimara. Ilidaiwa kuwa vitu hivyo kwa uchache wake ni kikwazo kikubwa kwa mtu kufikia daraja la Sakramenti ya Ndoa.

    SABABU ZA NDANI
    Ukiachana na sababu hizo za kanisa, Ijumaa Wikienda lilichimbua na kubaini sababu kuu 3 ambazo zilikuwa kisiki cha kufungwa kwa ndoa hiyo.

    SABABU YA KWANZA
    Kwa mujibu wa chanzo, mwanaume aliyetaka kufunga ndoa na Vicky ana ndoa nyingine ya kanisa na imejaliwa kupata watoto kadhaa hivyo isingekuwa rahisi kufungwa kwa ndoa nyingine kwa mujibu wa maandiko ya Biblia. Mume mmoja mke mmoja mpaka kifo kiwatenganishe.

    MKE ATINGA BUNGENI
    Chanzo kilizidi kudai kuwa wiki iliyopita, mwanamke huyo ambaye jina halikupatikana, alitinga bungeni na kuonana na Spika wa Bunge, Anne Makinda ambapo alijitambulisha ndiye mke wa Charles anayetaka kufunga  ndoa na Vicky Kamata.
    “Mke wa bwana harusi alikuja Dodoma juzi, akasaidiwa kuonana na spika na mbunge mmoja (jina tunalo).

    “Alimwambia spika yeye ndiye mke wa ndoa wa Charles, ila walitengana. Lakini alisema pamoja na kutengana huko, ndoa ya Kikristo haifungwi mara mbili labda mmoja afe. Kwa hiyo mumewe hawezi kufunga ndoa na Vicky,” kilisema chanzo.

    SABABU YA PILI
    Sababu ya pili ilielezwa kuwa, Vicky asingeweza kufunga ndoa hiyo kwani mwanaume huyo alishatoa mahari kwa msichana mmoja (jina tunalo) wa jijini Dar na ukweni anajulikana.
    “Alishatoa mahari kwa msichana mwingine mbali na Vicky, ukweni anajulikana.


    “Sasa ilipotoka ile picha yake kwa mara ya kwanza kwenye Gezeti la Ijumaa (Mei 16, 2014) yenye kichwa cha habari ndoa ya Vicky itatumia shilingi milioni 96 ikawa kasheshe kwa yule msichana na ukweni, ndiyo jamaa akaamua kutangaza kubatilisha ndoa na Vicky,” kilisema chanzo.

    SABABU YA TATU
    Sababu ya tatu ilitajwa ni kitendo cha kuumwa. Wikiendi iliyopita, Vicky aliugua ghafla na kulazwa katika Hospitali ya Tabata General jijini Dar kwa hiyo isingekuwa rahisi ndoa kufungwa Jumamosi kutokana na hali yake kuwa mbaya.

    WAANDISHI WATINGA HISPITALI
    Ijumaa iliyopita, waandishi wetu walitinga kwenye hospitali hiyo na kukutana na daktari mmoja ambaye alikiri Vicky kulazwa hapo lakini alikataa waandishi wasimuone kwa sababu hayuko katika hali nzuri kiafya. “Ni kweli Vicky kalazwa hapa lakini hamuwezi kumwona, hayuko katika hali nzuri, anahitaji kupumzika jamani, please,” alisema daktari huyo.

    HATIHATI ILISHAKUWEPO
    Katika Gazeti la Uwazi la Mei 20, 2014 ukurasa wa mbele kulikuwa na habari ndogo yenye kichwa kisemacho; NDOA YA MIL. 96 YA VICKY KAMATA HATIHATI KUFUNGWA.
    Katika habari hiyo ilielezwa kuwa ndoa  hiyo isingefungwa kutokana na kuibuka kwa mizengwe kibao.
    Habari za ndani zilisema mizengwe hiyo iliibuka katika hatua za mwisho na kusababisha mwanaume kuamua kubatilisha ndoa hiyo ambayo ilikuwa ifungwe Mei 24, mwaka huu jijini Dar.

    KIONGOZI MKUBWA SERIKALINI
    Ilidaiwa kuwa baada ya kuibuka kwa zengwe na mume kutangaza ndoa basi, Vicky aliumia na kuzifikisha habari hizo kwa Spika Makinda ambapo naye alizifikisha kwa kiongozi mmoja mkubwa serikalini, hasa bungeni.

    Kiongozi huyo alichukua jukumu la kumvutia waya bwana harusi na kumsihi kutochukua mawazo hayo na ikibidi ndoa ifungwe lakini mwanaume huyo alikataa katakata akisema mambo hayo ni ya kifamilia zaidi kwa hiyo yaachwe kwenye familia.

    MAMA SITTA ASIKITIKA
    Habari zinazidi kusema kuwa kati ya watu ambao wamehuzunishwa na kutofungwa kwa ndoa hiyo ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta ambaye aliposikia kuyeyuka kwa ndoa hiyo alisikitika si kwa sababu alikuwa kwenye vikao vya harusi, bali pia aliuona wakati mgumu atakaoupata Mhe. Vicky.

    WABUNGE WAULIZIA MICHANGO YAO
    Pamoja na yote yaliyojitokeza, habari zinadai kwamba baadhi ya wabunge waliochanga pesa ili kufanikisha harusi hiyo tangu juzi wameanza kuulizia michango yao wataipataje kwa vile harusi basi tena!

    “Huku Dom (Dodoma) hakukaliki bwana. Baadhi ya wabunge wameanza kuulizia michango yao, wanasema kama harusi haipo basi na chao wakipate,” alisema mbunge mmoja akiomba kuhifadhiwa jina.

    WABUNGE WATAJWA KUINJINIA
    Mbunge huyo alikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa kuna wabunge wametajwa ‘kuinjia’ zengwe la kutokufungwa kwa ndoa hiyo kwa sababu wanazozijua wao ambazo Ijumaa Wikienda haikupewa lakini inaendelea kuzichimba.

    VICKY KAMATA
    Vicky alipotafuwa kwa njia ya simu Jumamosi iliyopita ili azungumze lolote kuhusu kuyeyuka kwa ndoa yake hakupatikana hewani.

    Imeandaliwa na Chande Abdallah, Nyemo Chilongani na Mayasa Mariwata.      
  • Joyce Kiria Amfariji Vicky Kamata Baada ya Ndoa/Harusi yake Kuahirishwa

    Mtangazaji wa kipindi cha Wanawake Live, Joyce kiria amefunguka ya moyoni na kumpa pole mwanamuziki wa zamani na mbunge Vicky Kamata baada ya ndoa yake kudaiwa kuzuiliwa kufungwa baada ya kubainika kuwa mwanaume aliyetaka kufunga ndoa naye ana ndoa nyingine ya kanisa.

    Kupitia Facebook, Joyce ameandika:

    Hii habari imenihuzunisha sana. Ninachoweza kusema ni kwamba (1) Tuwe waaminifu kwenye mahusiano tuliyonayo. (2) Endapo tumeshindwa kuelewana au kuishi pamoja basi tumalizane kiutu uzima au kistarabu kila mtu achukue 50 zake kwa Amani. (3) Tusikomoane pale mtu anapoanza maisha yake mengine na mtu mwingine. Tatizo lipo kwa wahusika Hasa hasa suala la “Uaminifu” au suala la “kukomoana”, Kanisa limesimama kwa nafasi yake. Mh Vicky kama hili tukio ndo sababu ya kuumwa kwako, nakupa pole sana, yaliyokukuta ni sehemu ya Maisha, usiumie kiasi cha kuhatarisha uhai wako. Wewe mshukuru Mungu kwa kila jambo. Mungu akupe wepesi kwa jambo hili mengine yatajiseti mbele kwa mbele….jamani tumuombee maana mahusiano ya siku hizi ni hatari tupu! Yasipokukuta wewe yanaweza kumkuta mwanao!! Usijione wewe ni mjanja sanaaaa ila mshukuru Mungu.”

    Habari zimedai kuwa sababu zilizofanya ndoa hiyo isifungwe ni kutokana ni mwanaume aliyetaka kufunga ndoa na Vicky kuwa na ndoa nyingine ya kanisa na amejaaliwa kupata watoto kadhaa hivyo isingekuwa rahisi kufungwa kwa ndoa nyingine kwa mujibu wa taratibu za kidini.

    Kwa mujibu wa Global Publisher, mwanaume huyo alishatoa mahari kwa msichana mmoja wa jijini Dar na ukweni anajulikana, na ya mwisho ni Vicky aliugua ghafla na kulazwa katika Hospitali ya Tabata General jijini Dar kwahiyo isingekuwa rahisi ndoa kufungwa Jumamosi kutokana na hali yake kuwa mbaya.      
  • Sumu ya Mwanamke ni Mwanamke Mwenzie




    Sumu ya Mwanamke ni Mwanamke Mwenzie
    Usemi huo nilikutana nao kijiweni, wazee wakipongeza uamzi wa dini kuwa na wake wanne, kwamba mwanamke akijua kuna mwanamke mwenzake basi ananyoka vizuuuuriiii, hutasikia habari za usawa katika familia.

    Maneno haya nimeyaamini baada ya kisa hiki kunitokea, nipo na mpz wangu nampenda sana na nimejiapiza ndo atakuwa mke wangu, kuna wakati akaanza kunisumbua, nilichokifanya ni kujenga mazingira nataka kurudiana na x wangu, kwamba ananibembeleza sana na hata anatumia ndugu zangu kunishawishi turudiane, kwa kweli nampiga fix tu, tokea nioneshe hivyo mpenzi wangu kanyooka kama mti wa muashoki, ule usumbufu wake wa mwanzo umekwisha kabisa, ananibembeleza kama mfalme. 

    Nimeamini SUMU YA MWANAMKE NI MWANAMKE MWENZIE.


  • Ishara tano za Mwanamke anayekuzimia



    Ni muhimu sana kwako mwanaume kujua kwa uhakika kuwa mwanamke anakupenda kweli kweli,utajuaje kuwa mwanamke anakupenda? Zifuatazo ni ishara ambazo wewe kama mwanaume unapaswa uwe makini ili uweze kuziona na haraka kumtolea uvivu huyo mwanamke.

    *Mwanamke anaekupenda  she appreciates the little things you do hata kama sio cha maana sana na pia anapenda kushare nawe her time.....

    * Mwanamke anayekupenda atahangaika juu yako, atahangaika juu ya usalama wako,raha yako,heshima yako na maendeleo yako.Hii ni moja kati ya ishara kubwa kuwa mwanamke huyo anaupendo na wewe.

    * Mwanamke anayekupenda atakuonea wivu mara kadhaa,Wivu ni ishara kuwa anakupenda wewe na anataka akulinde usiibiwe au asije akakupoteza,anaogopa usije ukatoka katika maisha yake,au kwa maneno mengine usije ukamtoa moyoni mwako na nafasi yake ikachukuliwa.Japo wivu ukizidi sana pia inaweza kuleta tatizo.

    * Mwanamke anayekupenda atakapokuwa mbele ya marafiki zake au watu wengine atacheka nao lakini atakugeuzia ww macho/uso wake haraka sana. Kufanya hivi ni kuonyesha kuwa anakuhesabia ww kuwa utaweza kumletea furaha katika maisha yake,zaidi ya hilo ni kwamba anatumaini kuwa utamuona kuwa yeye ni mtu aliye rahisi kufurahishwa kwa kuwa yeye ni mtu wa furaha.

    * Mwanamke anayekupenda ataendelea kukuangalia usoni kwa muda mrefu kuliko ilivyo kawaida ya wanawake wengine,mara nyingi atakuangalia na kutabasamu vizuri. Hii huenda ni ishara moja muhimu sana ya kukuambia  kimoyomoyo kuwa “NJOO NIKO KWAAJILI YAKO.”


    Hivyo kama ulikuwa unahisi unamhitaji basi ni wakati mwafaka wa kumfuata na kumweleza ukweli na kirahisi nakuhakikishia unabeba mzigo kwani ni mtu tayari aliyekuwa anahisia kali za mahaba juu yako...

    KUMBUKA: WASICHANA WANAAIBU SANA NA USITEGEMEE ATAKUFUATA NA ATAKWAMBIA KUWA ANAKUPENDA KWANI NI WACHACHE WENYE UJASIRI HUO... ILA UKIONA DALILI HIZO HAPO JUU USILAZE DAMU .. CHANGAMKA UTAMMILIKI KIULAINI ......
  • May 25, 2014

  • JINSI YA KUSHIKA MIMBA HARAKA




    JINSI YA KUSHIKA MIMBA HARAKA


    1. Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, angalau siku tatu kwa wiki, ikiwezekana on alternate days.


    2. Tumia ovulation prediction kit, hiki ni kifaa ambacho kitakusaidia kujua wakati hasa mwanamke ameengua yai na ndio kipindi ambacho mwanamke ana uwezo wa kushika mimba akikutana na mumewe. Ni rahisi kutumia. 
    3. Fanya tendo la ndoa kabla ya kuengua yai (kabla ya ovulation), huongeza uwezekano wa kushika mimba kuliko kusubiria ovulation au kufanya baada ya ovulation.
    Kutaneni siku mbili au tatu kabla ya ovulation. Ukitumia ovulation test kit, mkutane kuanzia siku itakapokuwa positive kwani huwa inapredict ovulation kutokea 48 hrs after it tests positive. 
    4. Usitegemee njia ya kalenda kutabiri uenguaji yai, njia hii kwa kiasi fulani huweza kuwasaidia wale wenye mzunguko wa siku 28, lakini pia haina uhakika wa 100%, wengi wa wanawake hawaengui yai siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi, kwa hiyo kutegemea kalenda kutakuchelewesha kupata ujauzito. 
    5. unapotaka kushika mimba, acha au punguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe, sigara au dawa za kulevya. 
    6. unapotaka kupata mimba, tendo la ndoa liwe kitu 'enjoyable' na sio tendo 'mechanical' kwa ajili ya kutafuta mtoto.
    Kama hizi njia hazijakusaidia basi utakuwa na matatizo na unaweza kumuona daktari kwa msaada wa vipimo na matibabu. Natumaini uzi huu unaweza kuwa msaada kwa watafutao watoto.
    JINSI YA KUSHIKA MIMBA HARAKA



  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.