Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

December 09, 2016

  • Aubemeyang na kila dalili za kwenda Real Madrid.

    aube

    Real Madrid ina uwezo wa kusajili karibia wachezaji wote kwa gharama yoyote ambayo ni reasonable kwa wachezaji nyota duniani kwa sasa hivi.

    Habari za Aubameyang kujiunga na Real Madrid zimeongelewa sana na kwa kiasi kikubwa mchezaji mwenyewe anaendelea kuzibariki siku hadi siku. Baada ya mechi ya UEFA, Aubemeyang aliulizwa maswali na mwandishi wa habari na majibu yake yaliendelea kuonyesha kwamba yeye ni mchezaji wa Real Madrid kwa muda kadhaa ujao.

    Mwandishi alimuuliza kama atakuja kucheza Real Madrid, Aubameyang alimjibu kwamba alimpa ahadi babu yake kwamba siku moja atakuja kucheza hapo. Babu yake alikua anaishia nje kidogo ya makao makuu ya club ya Real Madrid. Hivyo basi amekua shabiki wa club hiyo kwa muda mrefu.

    Swali lingini mwandishi alimuuliza kwamba "Nimwambie Florentino Perez kwamba unataka kuwa ndani ya Real Madrid?". Mwandishi huyo alisema kamba Aubameyang alijibu ndiyo.

    Pia kupitia instagram account yake Aubameyang aliandika ujumbe wenye utata kidogo na picha ya mechi dhidi ya Real Madrid. Pierre aliandika "Nafikria kitu kimoja tu. Natumaini umeliona lile goli Babu".

    Wachambuzi wa mambo wanasema kumuona Aubameyang ndani ya kikosi cha Real Madrid halitakua jambo la kushangaza ndani ya muda mfupi ujao.



  • October 15, 2016

  • VITENDO VYA KISHIRIKINA DHIDI YA WATUMISHI WA HALMASHAURI VYAMKERA JAFO


    VITENDO VYA KISHIRIKINA DHIDI YA WATUMISHI WA HALMASHAURI VYAMKERA JAFO

    foja1

    Naibu Waziri Ofisi ya Rais , Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, akiwa na Mkuu wa wilaya ya Igunga na viongozi mbalimbali akipewa taarifa juu ya ujenzi wa nyumba za walimu, madarasa na vyoo vya shule za sekondari wilayani humo.

    foja2

    Naibu Waziri Ofisi ya Rais , Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, akipewa maelekezo juu ya matumizi ya mfumo wa kukusanyia mapato.

    foja3

    Naibu Waziri Ofisi ya Rais , Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, akiwa na mbunge wa Nzega Hussein Bashe katika ukaguzi wa bweni la wasichana wilaya ya Nzega.

    KUTOKANA na baadhi ya wananchi kuwafanyia vitendo vya ushirikina watumishi katika Halmashauri mbalimbali nchini, Naibu Waziri Ofisi ya Rais , Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo ameonyeshwa kukerwa na tabia hiyo huku vimesababisha watumishi kupata msongo wa mawazo na wengine kuomba kuhamishwa.

    Jafo alitoa kauli hiyo alipokuwa akikagua zahanati mpya iliyopo kijiji cha Ziba ndani ya Jimbo la Manonga wilayani Igunga mkoani Tabora na alipokuwa akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo.

    Alimuagiza mkuu wa wilaya ya Igunga kutenga muda yeye na kamati yake ya ulinzi na usalama kuwafikishia ujumbe wananchi wa wilaya ya Igunga kuwakemea wenzao wenye tabia hiyo wilayani humo ili kuacha tabia hiyo ovu. 

     Jafo alisisitiza kwamba tabia hiyo imewasababishia baadhi ya watumishi walio tendewa vitendo visivyo kupatwa na msongo wa mawazo na kuomba kuhama maeneo walio pangiwa.

    Naibu Waziri alisema kwamba jamii inapaswa kuwathamini watumishi kwani wametoka maeneo mbalimbali ya nchi ili kuja kuwatumikia wao hivyo wanatakiwa kuwathamini na kuwaheshimu kwa kulinda utu wao.

    " Watani zangu mliopo hapa Wasukuma na Wanyamwezi mmepata zahanati nzuri naomba muitunze. Pia sitaki kusikia daktari au mhudumu  amelala asubuhi anajikuta ng'ambo ya barabara au katika kiwanja cha mpira,"alisema Jafo

    Kadhalika, alikemea kitendo cha sungusungu walio mchapa viboko mwalimu mkoani humo huku akiwaagiza wakuu wa wilaya maeneo yote kupambana na tabia za udhalilishaji wanazo fanyiwa watumishi wa umma katika jamii ili waweze kufanya kazi kwa amani na kujiamini.

    Aliwapongeza viongozi wa mkoa wa Tabora kwa umoja na ushirikiano wao katika kuwaletea maendeleo wananchi wa mkoa huo. (P.T)



  • March 14, 2016

  • MKAPA ANVYOKUBALIKA KUREJESHA AMANI BURUNDI



    MKAPA ANVYOKUBALIKA KUREJESHA AMANI BURUNDI  Rais mstaafu wa Tanzania,          Benjamin Mkapa
    Bujumbura, Burundi. Burundi imeunga mkono kuteuliwa mpatanishi mpya kwa ajili ya kujaribu kutatua mgogoro wa nchi hiyo ambao umesababisha mamia ya raia kufa huku wengine wakikimbilia nchi jirani na kuishi kwenye kambi za wakimbizi.



    Chama tawala cha CNDD-FDD kimesema kuwa kuteuliwa kwa rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa kuwa mpatanishi mpya wa nchi hiyo ni hatua nzuri katika kuharakisha juhudi za kutatua mgogoro unaoendelea kufukuta.

    Mwenyekiti wa chama hicho, Pascal Nyabenda amesema Mkapa ana wakati mwingi wa kuzungumza na makundi yote nchini humo na wananchi ili kuandaa mazingira ya kufikiwa matokeo mazuri ya kurejeshwa amani na utulivu.
    Kiongozi huyo wa Burundi amesema kuwa Rais Yoweri Museveni wa Uganda ataendelea kusalia katika nafasi yake ya kusaidia kuboresha mazingira ya mazungumzo ya Burundi, lakini yeye peke yake hawezi kusimamia mazungumzo hayo.
    Katika kikao chao cha hivi karibuni viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) waliokutana mjini Arusha walimteua Mkapa kuwa mwenyekiti wa kundi la upatanishi wa mgogoro wa Burundi.
    Awali, Rais Museveni alikuwa ameteuliwa kuwa mpatanishi wa mgogoro huo. Licha ya kufanya vikao kadhaa vya mazungumzo na viongozi wa Burundi, hakufanikiwa kupata matokeo yoyote ya kuridhisha.
    Baadhi ya wataalamu wa mambo walikosoa kuchaguliwa Rais Museveni kuwa mpatanishi wa mgogoro huo na hivyo tokea mwanzoni walikuwa wametabiri kufeli upatanishi wake.
    Wiki iliyo iliyopita, marais wa nchi tano za Afrika za Mauritania, Uganda, Senegal, Gabon na Waziri Mkuu wa Ethiopia wakiongozwa na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini waliitembelea Burundi na kutaka mazungumzo ya haraka yafanyike ili kutatua mgogoro wa nchi hiyo.
    Hivi sasa kukubaliwa mpatanishi mpya wa mgogoro wa Burundi na viongozi wa Serikali ya nchi hiyo ni ishara nzuri kuwa viongozi hao wako tayari kuchukua hatua ya kutatuliwa kwa amani mgogoro huo ambao ulianza miezi kumi iliyopita kutokana na uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza kugombea tena urais kwa mara ya tatu mfululizo.
    Wengi wanaieleza hatua hiyo ya Rais Nkurunziza ni kwenda kinyume na katiba ya nchi na mazungumzo ya amani ya Arusha Tanzania.
    Mivutano ya kisiasa na ghasia za ndani zimefikia hatua ambayo inaoonekana na wa juzi wa mambo kuwa zinaweza kuanzisha tena vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
    Kutokana na ukweli huo, ndipo jamii ya kimataifa na hasa Umoja wa Afrika (AU) ukaanzisha juhudi kubwa katika siku za hivi karibuni kwa madhumuni ya kutatua kwa amani mgogoro wa nchi hiyo.
    Viongozi wa umoja huo wanasema kuwa vita vya aina hiyo huko Burundi vinaweza kuhatarisha usalama wa nchi nyingine za eneo hilo, na ndiyo maana wakasema kuwa hawataruhusu vita hivyo kutokea. Wanamatumaini kuwa mgogoro huo unaoendelea utapatiwa ufumbuzi.
    Hata kama mazungumzo ya kutatua mgogoro wa Burundi hayajafanikiwa, lakini kufuatia safari ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon na kisha ya viongozi kadhaa wa nchi za Afrika nchini humo, inaonekana kuwa mapatano ya kuhitimishwa mgogoro huo yamefikiwa kwa kiwango fulani.
    Matumaini hayo yanapata nguvu zaidi hasa baada ya Burundi kukubali kutumwa nchini humo waangalizi wa kijeshi 100 wa Umoja wa Afrika.
    Vilevile, imekubali waangalizi 100 wa haki za binadamu.
    Awali, Rais Nkurunziza alikuwa amedai kuwa kutumwa nchini kwake waangalizi hao ni uingiliaji wa mambo ya ndani ya nchi hiyo.
    Wiki iliyopita mkuu wa chama cha upinzani cha Front for Democracy in Burundi, Ngendakumana, LĂ©once alisema baada ya kukutana na ujumbe wa ngazi za juu wa Umoja wa Afrika wamekubaliana kuimarishwa upatanishi wa mgogoro wa nchi hiyo.
    Mgogoro huo hadi sasa umesababisha mamia ya watu kuuawa, kujeruhiwa na maelfu ya wengine kugeuka wakimbizi.
    Kutokana na juhudi zinazofanywa kwa ajili ya kumaliza mgogoro huo, watu wa Burundi na jamii ya kimataifa wana matumaini kwamba mazungumzo ya amani yataanza hivi karibuni kwa shabaha ya kuhitimisha mgogoro huo wa kisiasa, ivyo kurejesha tena nchini humo usalama, amani na utulivu wa kudumu.


  • March 06, 2016

  • WANAWAKE WAHIMIZWA KUSHIRIKI KWENYE MICHEZO



    WANAWAKE WAHIMIZWA KUSHIRIKI KWENYE MICHEZO
    jen3
    Na Fatma Salum  (MAELEZO) 
    Wanawake nchini wamehimizwa kushiriki kwenye michezo mbalimbali kuanzia ngazi ya vijiji hadi taifa ili kuboresha afya zao na kujiongezea kipato.
    Hayo yamesemwa na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Kazi Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama leo jijini Dar es Salaam wakati akihutubia kwenye Tamasha la Michezo kwa wanawake lililoandaliwa na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa Machi 8 kila mwaka. 
    Akihutubia kwa niaba ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Jenista ameeleza kuwa Serikali ina mipango thabiti ya kuboresha sekta ya michezo hivyo ni wakati muafaka kwa wanawake wa rika zote kushiriki kwenye michezo kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla. 
    "Wanawake tunaweza tusisubiri kuwezeshwa tujitokeze kwenye michezo kuanzia kwenye maeneo tunayoishi kwani itatusaidia kuimarisha afya zetu na kuepuka majanga ikiwemo UKIMWI hasa kwa wasichana kwa kuwa wanaposhiriki kwenye michezo wanaepuka kujihusisha na vitendo viovu kama ulevi na uasherati vinavyopelekea maambukizi" alisema Mhe. Jenista.
    Aidha Mhe. Jenista amelitaka Baraza la Michezo Tanzania  (BMT) kuandaa program maalum za kuhamasisha makundi mbalimbali kushiriki kwenye michezo hasa wanawake, watoto na walemavu. 
    Pia Mhe. Jenista ametoa wito kwa wadau wa michezo ikiwemo Mifuko ya Hifadhi za Jamii kushirikiana na BMT kuandaa matamasha mengi ya michezo yatakayohusisha wanachama wa mifuko hiyo ili kuimarisha afya zao na kuepuka maradhi kama Shinikizo la Damu na Kisukari yanayosababisha mifuko hiyo kutumia gharama kubwa kuwatibia kupitia fao la matibabu.
    Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa BMT Mhe. Zainab Vullu  (Mb) ameiomba Serikali kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya michezo ikiwemo kupunguza kodi kwa vifaa vya michezo vinavyoingia nchini na kuboresha mitaala ya elimu ya michezo mashuleni. 
    Tamasha hilo la michezo kwa wanawake limefanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam likibeba kauli mbiu ya mwaka huu inayosema " 50 kwa 50 ifikapo 2030, Tuongeze Jitihada, Maendeleo ya Wanawake kupitia Michezo Inawezekana".


  • BREAKING NYUZZZZ.....: BALOZI KIJAZI ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI, BALOZI SEFUE KUPANGIWA KAZI NYINGINE



    Katibu Mkuu Kiongozi mpya,
    Balozi John William Kijazi.


  • March 05, 2016

  • MAMBO YA TANGA HAYO! KULE MAPENZI YALIZALIWA!!



    MAMBO YA TANGA HAYO! KULE MAPENZI YALIZALIWA!!

  • Mbowe Kuzungumza na Taifa Kupitia Waandishi wa Habari Makao Makuu CHADEMA Leo


    Mbowe Kuzungumza na Taifa Kupitia Waandishi wa Habari Makao Makuu CHADEMA Leo
    Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe leo atazungumza na Taifa kupitia mkutano wa waandishi wa Habari.

    Mkutano huo wa waandishi utafanyika saa 6 mchana makao makuu Kinondoni Ufipa.

    Kiongozi huyo mkuu wa upinzani nchini anatarajiwa kutoa tamko rasmi la maazimio ya Kamati kuu ya chama iliyokutana Machi 1

    Tayari vyombo vya ndani na nje ya nchi vimealikwa kwenye mkutano huo na imetakiwa ifikapo saa 5 asubuhi waandishi wote wawe wamekaa kwenye nafasi zao.

    Mwenyekiti huyo anabashiriwa mbali na mambo kadhaa lakini atatoa msimamo rasmi wa chama kuhusiana na hujuma ya watawala dhidi ya uchaguzi wa meya wa DSM

  • Madiwani wa UKAWA Wavamia Ofisi ya Halmashauri ya Jiji La Dar Wakitaka Kuelezwa ni Lini Uchaguzi wa Meya Utafanyika



    Madiwani wa UKAWA Wavamia Ofisi ya Halmashauri ya Jiji La Dar Wakitaka Kuelezwa ni Lini Uchaguzi wa Meya Utafanyika
    Zaidi ya madiwani 20 wanaotokana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), jana walivamia ofisi za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kumshinikiza Kaimu Mkurugenzi wake, Sarah Yohana kuitisha Baraza la madiwani kwa ajili ya kufanya uchaguzi wa meya na naibu wake.

    Madiwani hao waliovamia ofisi hiyo jana, walisema kikao hicho kinatakiwa kuitishwa ndani ya siku saba kikiwa na ajenda moja ambayo ni uchaguzi wa meya na naibu wake, ambao umekwama mara kadhaa kwa kile walichodai kuwa ni hila na hujuma.

    Uchaguzi huo umeahirishwa mara tatu kwa sababu mbalimbali, Januari 23 uliahirishwa kutokana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene kutoa muda kwa mameya wa manispaa zinazounda Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam; Kinondoni, Temeke na Ilala kuandaa mfumo bora wa kuwapata wajumbe watatu watakaounda Baraza la Jiji.

    Februari 8, uliahirishwa kutokana na kubainika kwa nyongeza ya majina 14 yaliyopenyezwa kutoka halmashauri za Kinondoni na Ilala ambao hawakustahili kushiriki kikao hicho, pia Februari 27 uliahirishwa kutokana na zuio feki la mahakama.

    Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana baada ya kukaa zaidi ya saa tatu bila kuonana na Yohana, madiwani hao na wabunge walisema wamechoshwa na uongozi wa jiji kuwahadaa kama watoto wadogo.

    Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee alisema wamechoka kupigwa danadana na kwamba wanachohitaji ni uchaguzi wa Meya wa Dar es Salaam kufanyika ndani ya siku saba siyo vinginevyo.

    "Tumekaa zaidi ya saa tatu wametwambia Yohana hayupo, sasa akija mfikishieni taarifa kuwa Ukawa hatuna maelezo na Jumatatu tutatia timu tena hapa ofisini kwake," alisema Mdee akimpa maagizo Ofisa Utawala wa Dar es Salaam, Iman Kasagara.

    "Narudi tena, mfikishieni salamu, Jumatatu hatutaki kusikia longolongo za aina yoyote kutoka kwake. Tunataka majibu ya kueleweka vinginevyo hatutamuelewa," alisema Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha).

    Kasagara aliahidi kufikisha ujumbe huo kwa mhusika ambaye ilidaiwa alikuwa nje ya ofisi kikazi.

    Mwenyekiti wa Madiwani wa Ukawa Dar es Salaam, Manase Mjema alisema uvumilivu umewashinda kutokana na figufigisu zinazofanywa na Jiji la Dar es Salaam kuhusu uchaguzi huo.

    Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara alisema ajenda kuu ya Ukawa ni uchaguzi wa meya na wameacha shughuli zote hadi suala hilo lipatiwe ufumbuzi.

    "Sasa hivi wakurugenzi akiwamo wa Dar es Salaam, wamepeleka bajeti zao hazina bila kushirikiana na meya kwa sababu hajapatikana, hivi hapo kuna maendeleo kweli?" alihoji Waitara.

    "Kimsingi utaratibu wa kisheria ulishapita, sasa tunaelekea siku 90 bila meya tumechoka na hali hii," alisema Waitara.

  • Jamii Media yafungua kesi Mahakama Kuu kupinga vifungu Sheria Makosa ya Mtandao



    Jamii Media yafungua kesi Mahakama Kuu kupinga vifungu Sheria Makosa ya Mtandao
    Mkurugenzi                  Mtendaji wa Jamii Media, Maxence M. Melo (katikati)                  akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufungua                  kesi Mahakama Kuu Dar es Salaam kutaka Sheria ya Makosa                  ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa                  kuwa vinavunjwa kwa haki za msingi za Watanzania                  watumiao mitandao ya kijamii. Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence M. Melo (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufungua kesi Mahakama Kuu Dar es Salaam kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinavunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao ya kijamii.Baadhi ya wanasheria wa Jamii Media wakieleza kwa                  wanahabari dhumuni la kufungua kesi namba 9 ya mwaka                  2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32                  na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinasababisha kuvunjwa                  kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao. Baadhi ya wanasheria wa Jamii Media wakieleza kwa wanahabari dhumuni la kufungua kesi namba 9 ya mwaka 2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao.]Baadhi ya wanasheria wa Jamii Media wakieleza kwa                  wanahabari dhumuni la kufungua kesi namba 9 ya mwaka                  2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32                  na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinasababisha kuvunjwa                  kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao. Baadhi ya wanasheria wa Jamii Media wakieleza kwa wanahabari dhumuni la kufungua kesi namba 9 ya mwaka 2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao.
    --------------------------------------------------
      KAMPUNI ya Jamii Media, waendeshaji wa mitandao ya JamiiForums.com na FikraPevu.com wametinga Mahakamani kufungua kesi ya kikatiba wakipinga baadhi ya vifungu vya sheria ya makosa ya mtandao kwa kile kuingilia Uhuru wa Maoni na Kujieleza wa wananchi. Jamii Media imefungua kesi hiyo Mahakama Kuu leo jijini Dar es Salaam, kesi namba 9 ya mwaka 2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao ili kulinda maslahi ya umma kwa kuzingatia vifungu 26(2) na 30(3) vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

     Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence M. Melo mara baada ya kesi hiyo kufunguliwa mahakamani, alisema kampuni hiyo imelazimika kufungua kesi hiyo baada ya kushinikizwa mara kadhaa na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za baadhi ya wateja wao.

     Alisema takribani miezi mitatu iliyopita, Jeshi la Polisi limekuwa likiushinikiza mtandao huo kwa njia ya barua kutoa taarifa za baadhi ya wateja wake wanaoonekana kutoa taarifa zile ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaibua ufisadi mkubwa na ukwepaji wa kodi. 

     Aliongeza kuwa JamiiForums katika kuhakikisha inasimamia usiri (privacy) wa wateja wao, wamekuwa wakihoji mashinikizo hayo yanazingatia sheria gani na kutaka kujua ni vifungu gani vya sheria ambavyo wadau wa mtandao huo wamevivunja lakini wamekuwa hawapewi maelezo yanayoridhisha zaidi ya kuelezwa kuwa hatua zaidi zitachukuliwa kama hautatolewa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi. 

     "...Baada ya kupata mashinikizo takribani manne yanayoashiria kuwa haki ya watanzania watumiao mtandao wa intaneti na hasa watumiaji wa mtandao wa JamiiForums, Jamii Media imeshauriana na Wanasheria wake na kuona ni wakati sasa wa Kuilinda haki ya wananchi kupata taarifa na kulindwa kwa Uhuru wao wa Maoni na Kujieleza inayolindwa kwa mujibu wa Katiba ya Nchi ibaraya 18 ambapo imefungua Shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Kesi namba 9 ya mwaka 2016); kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinapelekea kuvunjwa kwa haki za msingi za watanzania watumiao mitandao ili kulinda maslahi ya umma kwa kuzingatia vifungu 26(2) na 30(3) vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano," alisema Melo. Alibahinisha kuwa mtandao wa JamiiForums utaendelea na shughuli zake kama kawaida na utaendelea kuwahakikishia watumiaji wake kuwa mahala salama pa kutolea madukuduku yao na hata kuisaidia Serikali kuonyesha nyufa zilipo kwa maslahi mapana ya Taifa (wakizingatia mwongozo wa ushiriki wa mijadala anuai). 

     Alisema JamiiForums itaendelea kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika jitihada zake za kupambana na ufisadi kwa kutoa uwanja/fursa salama na rahisi kwa wananchi kuweza kuyaainisha yale wanayoyabaini kuwa yanachelewesha maendeleo ya Taifa lao. 

     Mtandao wa JamiiForums ni mtandao mkubwa wa Kiswahili kwa Afrika Mashariki na Duniani ukiwa na wasomaji wasiopungua Milioni 4 kwa mwezi ambapo kwa mwaka 2016, mtandao huu unatimiza rasmi miaka 10 tangu uanzishwe. Mtandao huu unasifika kwa kutoa fursa ya kipekee kwa watumiaji wake kutoa yaliyo mioyoni mwao huku wengine wakijifunza mbinu kadha wa kadha za kijasiriamali, afya, elimu na hata kuibuka wanasiasa wapya waliofundwa na wana JamiiForums. "Pamoja na kuendelea kutoa huduma hata katika nyakati ngumu, mtandao wa JamiiForums unakumbana mara kwa mara na changamotonyingi zinazopelekea waanzilishi na waendeshaji wake kuwa katika misukosuko mara kwa mara." Anasema Melo.


  • Maalim Seif awasili Zanzibar



    Maalim Seif awasili Zanzibar leo hii
     
     Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad, amewasili Zanzibar alasiri YA LEO akitokea nchini India na Oman. Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege alilakiwa na viongozi kadhaa wa CUF na baadaye kuelekea kwenye makaazi yake, Mbweni.
      


  • WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA ITILIMA MKOANI SIMIYU


    WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA ITILIMA MKOANI SIMIYU
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Maabara katika shule ya Sekondari ya Budalabugija wilayani Itilima akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 4, 2016. 
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Machi 4, 2016. (P:icha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua bwawa la umwagiliaji na maji ya kunywa la kijiji cha Mkoma na Mwalushu wilayani Itilima akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu, Machi 4, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwsalimia wananchi baada ya kukagua bwawa la maji ya kunywa na umwagiliaji la vijiji vya Mkomana Mwalushu wilayani Itilima Machi 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwsalimia wananchi baada ya kukagua bwawa la maji ya kunywa na umwagiliaji la vijiji vya Mkomana Mwalushu wilayani Itilima Machi 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Askofu wa Jimbo la Shinyanga, Liberatus Sangu wakati alipoitembelea shule ya Sekondari ya Mwamapalala wilayni Itirima akiwa katika zira ya mkoa wa Simiyu Machi 4, 2016. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)


  • SUMATRA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI MADEREVA NA MAKONDAKTA WOTE WATAKAOWATOZA ABIRIA NAULI KUBWA TOFAUTI NA ZILIZOPANGWA



    SUMATRA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI MADEREVA NA MAKONDAKTA WOTE WATAKAOWATOZA ABIRIA NAULI KUBWA TOFAUTI NA ZILIZOPANGWA

    Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi Usafiri wa Majini na Nchi Kavu  (SUMATRA) Mkoa wa Kilimanjaro  kuwafikisha mahakamani madereva wote na makondakta wanaowatoza abiria nauli kubwa tofauti na zilizopangwa na ofisi hiyo.

    Hayo yamesemwa leo na Kaimu Afisa Mfawidhi Bw.Tadei Mwita alipokuwa akijibu kero ya mkazi wa mkoa huo kwa njia ya simu iliyotolewa na Gazeti  la Mwananchi Machi 04, mwaka huu,iliyozungumzia  daladala zinazofanya safari zake kati ya Moshi Mjini - Himo kuwatoza nauli ya shillingi 1000 abiria wanaoshuka maeneo ya Kiboriloni, Sango Pumuani na Kawawa road tofauti na nauli iliyopangwa na SUMATRA katika vituo hivyo.  

    "Kuanzia wiki ijayo wadau wote  watakao kuja kuomba leseni kwa ajili ya usafirishaji wa abiria ndani ya mkoa huu watahitajika kuonyesha nauli watakazo toza abiria katika vituo vya katikati kabla ya kufika kituo cha mwisho cha safari zao,"alisema Bw.Mwita.

     Bw.Mwita alisema hivi sasa SUMATRA Mkoa wa Kilimanjaro  imeanzisha utaratibu wa kuwataka wadau wote wanaotarajia kuanza kutoa huduma za usafiri wa daladala mkoani hapo kuonyesha nauli watakazo toza katika  vituo vya katikati kabla ya kufika kituo cha mwisho.

     Hata  hivyo Afisa huyo aliwashauri wakazi wa maeneo kama kiboriloni kwa sasa kupanda daladala za Kiboriloni kwa kuwa zipo nyingi ili kuepuka usumbufu unaojitokeza.


  • March 04, 2016

  • MENGINE KUTOKA KWA "KIM JONG-UN" RAIS WA KOREA KASKAZINI YAKO HAPA


    MENGINE KUTOKA KWA "KIM JONG-UN" RAIS WA KOREA KASKAZINI YAKO HAPA
    Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amevitaka vikosi vya taifa hilo vijiandae kutumia silaha za nyuklia "wakati wowote", vyombo vya habari vya serikali nchini humo vimesema.
    Ameambia viongozi wa kijeshi kwamba North Korea itabadilisha hali yake ya kijeshi na kuwa tayari hata kutekeleza mashambulio ya kuzuia hatari, shirika la habari la KCNA limesema.
    Lakini licha ya madai hayo, bado haijabainika taifa hilo limepiga hatua gani katika kuandaa silaha zake za nyuklia.
    Umoja wa Mataifa umewekea taifa hilo vikwazo vikali zaidi baada ya Prongyang kufanya majaribio ya nyuklia na makombora ya masafa marefu.
    Baada ya kuwekewa vikwazo, Korea Kaskazini ilijibu kwa kufyatua makombora sita ya masafa mafupi baharini.
    KCNA imesema Kim alikuwa akizungumza wakati wa zoezi la kijeshi Alhamisi. Inaaminika huo ulikuwa wakati ambao makombora hayo yafyatuliwa.
    Alisema Korea Kaskazini "lazima iwe tayari kufaytua silaha za nyuklia wakati wowote" kwa sababu maadui wanaitishia Korea Kaskazini.
    "Katika wakati huu wa hatari ambapo Wamarekani … wanahimiza vita na maafa kwa nchi nyingine na watu wengine, njia pekee ya kulinda uhuru wetu na haki ya kuendelea kuwepo ni kuimarisha uwezo wetu wa nyuklia," amenukuliwa akisema


  • BREAKING NEWZZZ....KIWANDA CHA RANGI CHA SADOLINI CHA TAZARA KINAUNGUA MOTO MUDA HUU



    BREAKING NEWZZZ....KIWANDA CHA RANGI CHA SADOLINI CHA TAZARA KINAUNGUA MOTO MUDA HUU


  • Serikali yamkabidhi Cheka Cheti cha pongezi kutokana na ushindi wake


    Serikali yamkabidhi Cheka Cheti cha pongezi kutokana na ushindi wake
    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia) akiwa ameambatana na Bondia Francis Cheka (wapili kulia) alipotembelea Wizarani leo jijini Dar es Salaam na Serikali imemkabidhi Cheti cha pongezi. Kushoto ni Rais wa Chama cha ngumi Tanzania (TPBO) Yassin Adballah (Ustadh).
    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa zoezi la kumkabidhi Cheti cha pongezi kutokana na ushindi Bondia Francis Cheka (kushoto) leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge.
    Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge (aliyesimama) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa zoezi la kumkabidhi Cheti cha pongezi Bondia Francis Cheka (wa pili kushoto) kutokana na ushindi wake leo jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na wa mwisho kushoto ni Rais wa Chama cha Mchezo wa Ngumi Tanzania (TPBO) Yassin Adballah (Ustadh).
    Bondia Francis Cheka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa zoezi la kupokea Cheti cha pongezi kutoka kwa Serikali leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye,Rais wa Chama cha ngumi Tanzania (TPBO) Yassin Adballah (Ustadh) na Meneja wa Bondia huyo Chifu Ndambile Juma Ntinginya.
    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wapili kushoto) akimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa BMT Mohamed Kiganja (aliyesimama) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa zoezi la kumkabidhi Cheti cha pongezi Bondia Francis Cheka (kushoto) kutokana na ushindi wa Mkanda wa Uzito wa Super Middle wa Mabara wa WBF leo jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge.
    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akimkabidhi Cheti cha pongezi Bondia Francis Cheka kutokana na ushindi alioupata katika pambano baina yake na Bondia Mserbia anayeishi Uingereza Geard Ajetovic (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) na Bondi Francis Cheka wakiwaonyesha waandishi wa Habari Mkanda wa uzito wa Super Middle wa Mabara ambao Cheka ameunyakuwa baada ya kushinda pambano la tarehe 27 Februari baina yake na Bondia Mserbia anayeishi Uingereza Geard Ajetovic (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa Bondia huyo Chifu Ndambile Juma Ntinginya. Picha na Frank Shija, WHUSM.


  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.