Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

July 11, 2015

  • VIDEO: TIZAMA JINSI NAPE ALIVYOKWEPA KUWATAJA WAGOMBEA WATANO WALIOTEULIWA NA kikao cha Kamati kuu.



    VIDEO: TIZAMA JINSI NAPE ALIVYOKWEPA KUWATAJA WAGOMBEA WATANO WALIOTEULIWA NA kikao cha Kamati kuu.


    Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye akiongea na waaandishi wa habari mara baada ya kutoka kikao cha Kamati kuu.

    Mhe. Emmanuel Nchimbi akitangaza mbele ya wanahabari kutangaza kutoridhishwa na maamuzi yao.
    Mama Sophia Simba akizongwa na wanahabari  juu ya Kamati Kuu. 

    Hali si hali ndani ya Makao Makuu baada ya wajumbe wa Kikao cha Kamati Kuu uliomalizika usiku huu kushindwa kufikia maamuzi ya 5 bora na baadae 3 bora.

    Kutoelewana huko kumetokana na wajumbe wakati wa Kamati Kuu ilichokuwa ikiendeshwa na Mwenyetiki wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete kushindwa kuazimia maamuzi yaliyokuwa yameletwa.

    Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho

     Nape, alisema kila kitu kitajulikana asubuhi ya Julai 12, 2015 huku wajumbe watatu wa Kamati hiyo, Mhe. Nchimbi, Adamu Kimbisa na Sophia Simba kukataa maamuzi hao.

    Mhe. Nchimbi akiongea na waandishi alisema wao wamekataa kuafiki kwa vile wamekiuka kanuni kwa kuleta majina machache ili yaweze kijadiliwa jambo ambalo si sawa.

    BOFYA VIDEO HAPA CHINI


  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.