…………………………………………………………………….
Leo Juni 20, 2014 Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania wamezindua mpango maalum wa kutoa mikopo kwa wastaafu ambao unajuliakana kama Wastaafu Loan, ambapo sasa wastaafu wa PSPF wanaweza kunufaika na mikopo hiyo.
Lengo la mkopo huu ni kuwawezesha wastaafu kukidhi mahitaji halisi ya fedha, na hatimaye kuboresha maisha yao. Miongoni mwa mahitaji makubwa ya fedha kwa wastaafu ni pamoja na gharama za matibabu, ada za shule, kuendesha biashara na miradi mbalimbali.
kwa muda mrefu sasa hapa nchini taasisi mbalimbali za fedha zimekuwa hazitoi mikopo mbalimbali kwa wastaafu wakidhani kwamba wastaafu hawana uwezo wa kulipa, na kujenga dhana ya kutokopesheka, kwa kuliona hilo na kwa kutambua mchango wa wastaafu kwa taifa hili. PSPF kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania tumebuni mpango huu wa kipekee nchini wa kuwakopesha wastaafu wa Mfuko wa PSPF.
Katika utafiti tuliofanya umeonesha kuwa wastaafu kwa ujumla wanaingiza kiasi kikubwa sana cha fedha katika uchumi kutokana na mafao wanayolipwa. Mafao hayo yanaweza kuleta athari chanya (multiplier effect) katika nyanja mbalimbali za kiuchumi kama vile kuongeza uwezo wa kifedha katika taasisi za kifedha, kuongeza ajira, kukuza kipato, kupunguza umaskini na kudumisha utulivu wa kisiasa nchini. Hili linawezekana iwapo fedha hizo zitatumika kwa busara na kuwekezwa katika maeneo salama. Ni wajibu wa PSPF kutimiza dhana ya kuwakinga wastaafu na majanga yote ya kiuchumi na ya kijamii yanayotokana na kupungukiwa na kipato. Kwa kuzingatia hili Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania umebuni na kuanzisha Mpango huu wa Mikopo kwa Wastaafu wa Mfuko wa PSPF.
Hivyo tunapenda kuzishawishi taasisi za fedha ikiwemo mabenki na wataalam wa uwekezaji na fedha kubuni njia mbalimbali za kuwasaidia wastaafu ili waweze kuwekeza na kuendelea kufurahia maisha ya ustaafu. Pia wataalam hao waangalie namna kuweka mipango ya kusaidia wastaafu hapa nchini ambao kwa ujumla wao wana kiasi kikubwa cha fedha ambacho kikitumiwa vyema kinaweza kuleta mchago mkubwa katika uchumi wa nchi. Mpaka sasa zaidi ya wastaafu zaidi ya 2000 wamenufaika na mpango huu ambao umeanza miezi mitatu iliyopita.
Mstaafu anayetaka kukopa hatahitaji kuwa na dhamana , pia mkopo huu una bima, hivyo endapo mkopaji atafariki familia yake haitaendelea kudaiwa, aidha, riba inayotozwa kwa mkopo huu ni ndogo ukilinganisha na mikopo mingine, yaani asilimia 12 tu kwa mwaka. Wastaafu wote wa mfuko wa PSPF wanaweza kupata mikopo hii ambayo marejesho yake ni kati ya mwaka moja hadi miaka mitatu.
Ili kukopa unahitajika kwenda kwenye tawi lolote la Benki ya Postalililopo karibu yako

0 comments:
Post a Comment