Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

Showing posts with label Picha Hizo. Show all posts
Showing posts with label Picha Hizo. Show all posts

July 18, 2014

  • Dk. Shein aagana na Balozi wa ISRAEL aliemaliza muda wake




    Dk. Shein aagana na Balozi wa ISRAEL aliemaliza muda wake
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Israel Mhe,Gil Haskel aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Israel Mhe,Gil Haskel aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Balozi wa Israel Mhe,Gil Haskel baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]


  • WAJUMBE WA BODI WA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU WAKUTANA LEO KUJADILI MAENDELEO YA OFISI HIYO




    WAJUMBE WA BODI WA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU WAKUTANA LEO KUJADILI MAENDELEO YA OFISI HIYO
    Wajumbe wa Bodi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao chao kilichofanyika leo katika ukumbi wa ofisi hiyo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi Pro. Melline Mbonile kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kulia kwake ni Mary Faini kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Doreen Laurent kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na kushoto kwake ni Paula Tibandebage kutoka REPOA na John Mwilima kutoka Wizara ya Fedha. (Picha na Mpiga picha wa NBS).


  • Rais Kikwete amteua Capt. John Chiligati kuwa Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya MKURABITA




    Rais Kikwete amteua Capt. John Chiligati kuwa Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya MKURABITA
    Capt. John Chiligati




  • Introducing Toto Shine Magazine



    Introducing Toto Shine Magazine



    The Toto Shine Magazine is now looking for drawings, poems or short stories from children ages 6 -14.

    This magazine is for the whole East Africa region and beyond, so we want as many kids from Tanzania as possible to participate. 
     
    I do remember when I was a little kid Mama na Mwana show read something I sent to them on the radio that was one of my best days. Also I answered some questions and they mailed me a congratulatory letter for being one of the winners. That little piece of paper I received was one of my inspirations growing up and I kept it for so many years.....

    Motivate your kids to participate.  Thanks to my very good friends who believe me on this project so far we pay US $20  if we use each drawing, story or poem on our magazine. 


    It is not just funny to earn money while still a kid but its also empowers. That little achievement your child, niece or nephew will receive can be a solid foundation of his/her ambition and determination to do much more in life. 

    The phone app is coming soon to easily update your kid's work direct from your phone or tablet.  

    Tell you kids, nieces and nephews and everyone you know. From abstract art and traditional drawing to sketching, painting, or doodling or perhaps it's something that symbolizes the culture or maybe it's a moment in her/his life that stands out. It could be a character he/she has created, or a drawing of a favorite pet. We are looking for it all. 

    For poems we prefer non-rhyming poetry (free verse poems) though if your kid prefers rhyming poetry don't hesitate to send it to us. 

    For short stories 1500 words or fewer works best for our readers' ages. 

    For a chance your kid to be accepted make sure you or a teacher carefully read his/her writing or look at his/her artwork before submitting, and then consider any suggestions to make it better. Often, there are events in stories that don't make sense, and having someone read it and make suggestions always helps! 

    You or your child/niece/nephew must be 6-14 years old to participate.

    Follow us at @totoshinemag and facebook ID Toto Shine for more updates 
    The website www.totoshine.com is soon coming 

    Also for those who would like to support our effort you can download our media kit at http://www.kwanzapress.com/Toto%20Shine%20media%20kit.pdf

    Best Regards,
    Pauline



  • PICHA NA TAARIFA RASMI KWA UMMA:SOMA TAMKO LA JUKWAA LA KATIBA TANZANIA KUHUSU HALI YA KUTOFAUTIANA KATIKA BUNGE MAALUM LA KATIBA NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA




    PICHA NA TAARIFA RASMI KWA UMMA:SOMA TAMKO LA JUKWAA LA KATIBA TANZANIA KUHUSU HALI YA KUTOFAUTIANA KATIKA BUNGE MAALUM LA KATIBA NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

    Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Bw. Deus Kibamba akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Julai 17, 2014 kuelezea msimamo wa JUKWAA LA KATIBA juu ya mwenendo uliopita wa bunge hilo. Picha na Cathert Kajuna wa Kajunason Blog

    Kiongozi wa Shule Kuu ya Sheria nchini Kenya, Profesa Patrick Lumumba alisisitiza suala la wanasiasa kurudi bungeni na kuhakikisha katiba mpya inapatikana.

    Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.

    Wajumbe wa JUKWAA LA KATIBA wakisisitiza jambo.
    --
    Na Hellen Kwavava, Dar es Salaam.
    Ushauri Umetolewa kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba kuwa na Mtazamo mpya utakaoiletea nchi maslahi pindi watakaporudi bungeni katika mchakato wakutafuta katiba mpya unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.
    Hata hivyo kundi la Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) limezidi kushauri wakirudi bungeni na kuendelea na majadiliano kwa msingi wa rasimu ya katiba.
    Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam jana Julai 17, 2014 na mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Bw. Deus Kibamba ambapo ameeleza kwamba wabunge wanatakiwa kuachana na mtazamo wa kisiasa pamoja na lugha zisizo na staa kwenye bunge hilo kwani wanatakiwa kuzingatia uzalendo kwanza.
    Aidha Bw. Kibamba amesema kwamba licha ya muda kuwa mfupi kuelekea katika uchaguzi wa mwaka 2015 wao wanapendekeza juhudi zaidi zifanyike ili kukamilisha upatikanaji wa katiba hiyo.
    Naye Kiongozi wa shule kuu ya Sheria nchini Kenya Profesa Patrick Lumumba amewasihi wanasiasa wa nchini kuhakikisha katiba inapatikana kutokana na matakwa ya wananchi kwani nchini jirani zimekuwa zikiiga mambo mengi kutoka huku.Bunge Maalum la katiba linatajiwa kuanza tena Agosti 5, 2014 mwaka huu.



  • Picha:Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu Akutana Kwa Mazungumzo na Balozi wa heshima Mhe. Ahmed Issa Beverly Hills California




    Picha:Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu Akutana Kwa Mazungumzo na Balozi wa heshima Mhe. Ahmed Issa Beverly Hills California
     Balozi wa heshima Mhe. Ahmed Issa akifanya mazungumuzo na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu Beverly Hills California mapema jana  mazungumuzo yaliyohusu kutangaza Utalii wa Tanzana nchini Marekani pia Waziri Nyalandu alimpongeza Balozi wa Heshima kwa kuendelea kutangaza utalii wa Tanzania kwenye magari yake ya mizigo.



  • Picha Kutoka IKULU:Rais Jakaya Kikwete Aelekea Mkoani Ruvuma Kwa Ziara ya Kikazi ya wiki moja ambapo atakagua na kuzindua miradi ya maendeleo na kuongea na wananchi.


    Picha Kutoka IKULU:Rais Jakaya Kikwete Aelekea Mkoani Ruvuma Kwa Ziara ya Kikazi ya wiki moja ambapo atakagua na kuzindua miradi ya maendeleo na kuongea na wananchi.


    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na Kamishna wa Polisi Msaidizi Mwandamizi (SACP) Mary Nzuki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Jana Julai 17, 2014  wakati akipanda ndege kuelekea mkoani  Ruvuma kuanza ziara ya Kikazi ya wiki moja ambapo atakagua na kuzindua miradi ya maendeleo na kuongea na wananchi. Kati kati ni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)  Hamisi Selemani, Kamanda wa Polisi katika Uwanja huo wa ndege. PICHA NA IKULU



  • PICHA:SHABIKI WA SKYLIGHT BAND AWADATISHA JONIKO FLOWER NA ANETH KUSHABA KWA KUCHEZA MA-STYLE YA BENDI HIYO BILA KUKOSEA!



    PICHA:SHABIKI WA SKYLIGHT BAND AWADATISHA JONIKO FLOWER NA ANETH KUSHABA KWA KUCHEZA MA-STYLE YA BENDI HIYO BILA KUKOSEA!
     DSC_0155
     Aneth Kushaba AK47 akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.
     DSC_0046
     So how do you expect me to live alone with just me ...'Cause my world revolves around youIt's so hard for me to breathe...No air ...air...Bonge moja la Kolabo ni Sam Mapenzi na Aneth Kushaba AK47 wakitoa burudani.

     DSC_0302
     Baadhi ya mashabiki wa Skylight Band wakipata Ukodak wa nguvu.
    DSC_0106
     Vijana wa JembeniJembe wa Skylight Band wakitikisa jukwaa kutoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo Ijumaa iliyopita kwenye viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.
    DSC_0130
    Digna Mbepera, Mary Lucos na Sony Masamba wakiwajibika jukwaani.
    DSC_0025
    Vijana watanashati, nadhifu wanastahili kila sifa kupewa wao....si wengine ni wa Skylight Band ambayo ndio habari ya mujini kwa sasa haina mfano wake...Divas wa bendi hiyo Kutoka Kulia Digna Mbepera, Mary Lucos na Aneth Kushaba AK47 wakipewa sapoti na mkongwe wa muziki wa dansi nchini Joniko Flower Ijumaa iliyopita.
    DSC_0164
    Sam Mapenzi akiongoza kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita huku akipewa back vocal na Joniko Flower, Hashim Donode na Sony Masamba ndani ya viunga vya Thai Village.
    DSC_0170
    Taratibu mdogo mdogo amsha amsha hiyo kwa raha zetu......Njoo ujinafasi kwenye viunga vya Thai Village na Skylight Band leo usiku kuanzia saa tatu.DSC_0132
    Mary Lucos akiwaburudisha mashabiki wa Skylight Band huku akisindikizwa na Digna Mbepera Ijumaa iliyopita.
    DSC_0251
    Sugua sugua mpaka kitakate....! Unakaribishwa usiku wa leo usugue kiatu chako na SKYLIGHT BAND ndio habari ya mujini kwa sasa!
    DSC_0247
    Mashabiki nao hawakubaki nyuma mule mule tu kama inavyoonekana pichani.
    DSC_0230
    Mguu wa kushoto mbele wa kulia nyuma......!
    DSC_0228
    DSC_0225
    Ya chuma chuma nataka mukanda ya Chuma chuma.....! mashabiki waliofuzu kucheza moja ya style za Skylight Band....Njoo na wewe leo tujumuike pamoja.
    DSC_0338
    PICHA HII ITAKUWA USHAHIDI TOSHA: Mmoja wa mashabiki wa Skylight Band ambaye jina lake halikuweza kupatikana akionyesha uwezo wake wa kusakata ma-style mbalimbali ya bendi hiyo baada ya Joniko Flower kuvutiwa na uchezaji wake kama inavyoonekana pichana jamaa alivyo COPY na KU-PASTE miondoko hiyo.
    DSC_0339
    KWANINI TUANDIKIE MATE WAKATI WINO UPOOO...? Hebu jione mwenyewe utafikiri hawa jamaa mapacha mpaka Style ya kuweka vidole jamaa kaiga.

    DSC_0342
    Joniko Flower alichemka na kuamua kumshangaa tu jamaa anavyosakata mangoma...Wewe Je unakipaji kama hichi...? Basi usikose Ijumaa ya leo uje utuonyeshe ufundi wako, na SKYLIGHT BAND wanazawadi maalum ikiwemo usafiri wa bure wa kukurudisha nyumbani kwako na vingine kibao kwa shabiki atakayesakata miondoko kama hii jukwaani.
    DSC_0347
    Aneth Kushaba AK47 mwenye alisalimu amri kwa huyu jamaa....!
    DSC_0050
    Birthday Girl Renatha Mushi akifurahi burudani ya Skylight Band na wadogo zake wapendwa walioamua kumfanyia surprise ya nguvu.
    DSC_0194
    Baadhi ya members wa WANAMANYOYA wakijumuika na mashabiki wa Skylight Band kuonyesha style mbalimbali za uchezaji wao.
    DSC_0191
    DSC_0190
    DSC_0278
    Hiki ni kiungo muhimu sana katika muziki wa LIVE Band....Idrissa Drum alihusika kupika ladha nzuri ya muziki wa Skylight Band.
    DSC_0253
    Kikuku huyo ana manyoya huyooo......Dunda dunda pasua twende...!
    DSC_0322
    Mashabiki wa Skylight wakicheza na kupiga mayowe ya furaha kutokana na kukunwa na burudani nzuri ya bendi hiyo.
    DSC_0325
    Kumbe ni Aneth Kushaba AK47 ndio alikuwa akiwachizisha mashabiki wa Skylight Band kwenye show ya aina yake Ijumaa iliyopita ndani ya viunga vya Thai Village.
    DSC_0276
    Mambo ya mduara yalikhusika pia Ijumaa iliyopita ndani ya viunga vya Thai Village leo pia kama kawaida tupo hapo kuanzia saa tatu usiku....No where else to go rather than SKYLIGHT BAND...JUST FOLLOW THE LIGHT!
    DSC_0271
    Kinyau nyau kikiacha Pweza....!Eeeeh mambo ya pwani hayo shurti ulegeze vidole ndio raha yake ati....! Joniko Flower akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band.
    DSC_0180
    WANAMANYOYA wakipata Ukodak na Birthday Girl dada yetu mpendwa kabisa Renatha Mushi aliyetimia miaka kadhaa hivi na kuja kusheherekea na Skylight Band.
    DSC_0317
    Divas wa Skylight Band Mary Lucos na Digna Mbepera wakipata Ukodak na wadau wa ukweli wenye mahudhurio ya kuridhisha kila Ijumaa ndani ya kiota cha Thai Village.
    DSC_0203
    Mratibu wa Skylight Band Lubea akishow love na mdogo wake All the way from Zanzibar....!
    DSC_0200
    Back stage.
    DSC_0312
    Mmoja wa Masuperstar anayeunda kundi la Wadananda akipata Ukodak na mremboz mkareeee!!
    DSC_0320
    Wamependeza hawajapendeza.



  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.